“Mkumbuke Rais Nelson,” Liahona, Nov. 2025.
Habari za Kanisa
Kumkumbuka Rais Nelson
Familia, marafiki, na viongozi wanatoa heshima kwa Rais wa 17 wa Kanisa kwa upendo wake, huduma, na kujitolea kwake kwa dhati kwa Yesu Kristo.
Siku mbili baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu, viongozi wa Kanisa na wanafamilia walisoma wasifu wa Rais Russell M. Nelson kama baba mwenye upendo na mume, rafiki mpendwa, mfuasi mwaminifu wa Bwana Yesu Kristo, na nabii wa Mungu aliyekuwa na mwongozo wa kiungu.
Maisha ya Rais Nelson “yanatoa ushahidi wa ushuhuda wake wa dhati kabisa kama nabii na mtumishi wa Bwana Yesu Kristo,” Rais Dallin H. Oaks alisema wakati wa ibada za mazishi kwa ajili ya Rais Nelson mnamo Oktoba 7, 2025, katika Kituo cha Mikutano. Rais Oaks alimwita Rais Nelson, ambaye alifariki kwa amani akiwa nyumbani kwake Septemba 27, 2025, “rafiki yangu mpendwa na mwalimu mwenye tija zaidi.”
Rais Oaks pia alimwita Rais Nelson “mmojawapo wa wamisionari wa Israeli wenye nguvu katika matendo.” Alisema, “Tabasamu lake, joto la sauti yake, na nguvu ya uwepo wake viliyeyusha mioyo” ya mataifa na viongozi wa imani.
Rais Oaks na wasemaji wengine watano walitoa heshima kwa Rais Nelson kwa upendo wake, huduma, na kujitolea kwa dhati kwa Bwana Yesu Kristo na watoto wa Mungu ulimwenguni kote.
Pamoja na wazungumzaji wengine, alimshukuru Dada Wendy Watson Nelson kwa kumtunza na kumsaidia Rais Nelson katika miaka 19 ya ndoa yao. Pia alielezea shukrani kwa marehemu Dantzel White Nelson mke wa kwanza wa Rais Nelson, na watoto wao 10 kwa uaminifu wao kwa “kile alichohubiri na kuishi.”
Mzee Henry B. Eyring, ambaye alihudumu pamoja na Rais Oaks na Rais Nelson katika Urais wa Kwanza, alishuhudia juu ya wito wa kinabii wa Rais Nelson na uwezo wake na hamu ya kuwabariki wengine.
“Kadiri nilivyo hudumu naye bega kwa bega katika Urais wa Kwanza kuanzia Januari 2018, nimekuwa shahidi binafsi kwenye ukweli kwamba Bwana anampa mwongozo wa kiungu nabii wake,” alisema Eyring. “Ninayo shukrani ya kumjua Rais Russell M. Nelson.”
Katika hotuba zao, Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Rais Camille N. Johnson, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi, walimsifu Rais Nelson kwa ukarimu wake usio shindwa kwa watu ndani na nje ya Kanisa.
“Kupata fursa ya kuona akipenda watu na watu wakimpenda yeye vilifanya kumbukumbu zilizo nzuri zaidi,” alisema Mzee Holland. Yeye alimkumbuka Rais Nelson kama “mshika mikono na mponyaji wa mioyo.”
Rais Johnson aliongezea, “Rais Nelson kiuhalisia ameubadilisha ulimwengu mtu mmoja na mwingiliano mmoja kwa wakati mmoja, na ametualika sisi kufanya vivyo hivyo kwa kuvuta nguvu za Mungu kama wanawake na wanaume wa agano.”
Wawili miongoni mwa watoto wa Rais Nelson, Laurie N. Marsh na Russell M. Nelson Jr., walisema baba yao aliishi kwa furaha kwa sababu aliyaweka maisha yake kwa Mwokozi Yesu Kristo na kufanya utumishi kwa wengine kuwa kipaumbele.
“Tulilelewa katika nyumba ambayo kitovu chake ni Mwokozi na kujazwa na shangwe,” alisema Dada Marsh. Alisema lengo la familia lilikuwa kuwa familia ya milele.
Kaka Nelson aliongeza kuwa baba yake hakuwa na kuchoka katika huduma yake. “Rais Nelson alituonyesha moja kwa moja kwamba hakuna ‘kupumzika’ katika toleo lake la Urejesho.” Alisema kwamba wakati alipoitwa kuongoza Kanisa, baba yake aliahidi kumtumikia Baba na Mwana hadi siku yake ya kufa. “Amefanya hivyo tu.”
Marjorie N. Lowder na Gloria N. Irion, mabinti wa Rais Nelson, walitoa sala katika ibada hii. Kwaya ya Tabenakulo huko Temple Square iliimba muziki.
Mazishi ya Rais Nelson yalikuja juu ya visindiko vya heshima iliyofanyika kwa heshima yake Oktoba 1 na matangazo kutoka Tabenaklo huko Temple Square. Rais Oaks, Wazee Holland na Eyring, Askofu Kiongozi Gérald Caussé, Mzee Carl B. Cook wa Urais wa Sabini, na Rais Mkuu wa Watoto Susan H. Porter walitoa heshima, wakishiriki uzoefu mwema wa kibinafsi wa kuhudumu na Rais Nelson na hisia zao kuhusu maisha yake ya mfano, huduma kama ya Kristo, na mafundisho yenye mwongozo wa kiungu.
Katika shukrani zake, Rais Oaks alimwita Rais Nelson “nabii wa upendo” ambaye “alihubiri injili ya upendo.”
Kwa ziada kuhusu maisha na huduma ya Rais Nelson, ona In Memoriam: President Russell M. Nelson, 1924–2025, iliyochapishwa kama nyongeza kwenye majarida ya Kanisa ya Novemba 2025.