2025
Usiache Rehema Yako Mwenyewe
Novemba 2025


10:43

Usiache Rehema Yako Mwenyewe

Unaweza kupata msaada wa kiungu na uponyaji mara moja licha ya dosari zako za kibinadamu.

Wakati fulani mwalimu mmoja alifundisha kwamba nyangumi—hata ingawa ni mkubwa—hawezi kumeza binadamu kwa sababu nyangumi wana koo ndogo. Msichana mmoja alipinga, “Lakini Yona alimezwa na nyangumi.” Mwalimu akajibu, “Hilo haliwezekani.” Akiwa bado hajasadiki, msichana huyo alisema, “Naam, nitakapofika mbinguni, nitamuuliza.” Mwalimu alidhihaki, “Itakuwaje kama Yona alikuwa mdhambi na hakwenda mbinguni?” Msichana akajibu, “Basi unaweza kumuuliza.”

Tunacheka, lakini hatupaswi kukosa uwezo ambao hadithi ya Yona inampa kila “mtafutaji mnyenyekevu wa furaha,” hasa wale wanaotatizika.

Mungu alimwamuru Yona “aende Ninawi” kutangaza toba. Lakini Ninawi ilikuwa adui mkatili wa Israeli ya kale—kwa hiyo kwa haraka Yona alielekea hasa upande mkabala, kwa mashua, hadi Tarshishi. Akiwa safarini kukwepa wito wake, tufani ya kuvunjika meli inatokea. Bila shaka sababu ya kutotii kwake ndiyo chanzo, Yona anajitolea kutupwa baharini. Hili linatuliza bahari iliyochafuka, ambayo inawaokoa wasafiri wenzake.

Kimuujiza, Yona anaepuka kifo wakati “samaki mkubwa” ambaye Bwana “alimtayarisha” anammeza. Lakini anateseka katika mahali hapo penye giza na panaponuka kwa siku tatu, hadi hatimaye anatapikwa nchi kavu. Kisha anakubali wito wake wa kwenda Ninawi. Hata hivyo, jiji hilo linapotubu na kuepushwa na uharibifu, Yona anachukizwa kwa rehema iliyoonyeshwa kwa adui zake. Mungu anamfundisha Yona kwa subira kwamba anawapenda na anatafuta kuwaokoa watoto Wake wote.

Akijikwaa zaidi ya mara moja katika majukumu yake, Yona anatoa ushuhuda wa wazi kwamba katika maisha ya duniani, “wote wameanguka.” Mara nyingi hatuzungumzii ushuhuda wa Anguko. Lakini kuwa na ufahamu wa kimafundisho na ushuhuda wa kiroho wa kwa nini kila mmoja wetu anapambana na changamoto za kimaadili, kimwili na hali ni baraka kubwa. Hapa duniani, magugu mabaya hukua, hata mifupa yenye nguvu huvunjika, na vyote “kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Lakini hali hii ya kufa—matokeo ya maamuzi yaliyofanywa na Adamu na Hawa—ni muhimu kwa ajili ya uwepo wetu: “ili [tuwe] na shangwe”! Kama wazazi wetu wa kwanza walivyojifunza, ni kwa kuonja tu uchungu na kuhisi uchungu wa ulimwengu ulioanguka ndipo tungeweza kupata, si tu shangwe, hata furaha ya kweli.

Ushuhuda wa Anguko hauhalalishi dhambi au kulegalega katika majukumu ya maisha, ambayo daima huitaji bidii, wema na uwajibikaji. Lakini Anguko linapaswa kupunguza kufadhaika kwetu wakati mambo huenda mrama au tunapoona kukosekana kwa maadili kwa mwanafamilia, rafiki au kiongozi. Mara nyingi vitu kama hivi hutusababisha kuingia kwenye ukosoaji wa ubishi au vinyongo ambavyo hukwapua imani yetu. Lakini ushuhuda imara wa Anguko unapaswa kutusaidia kuwa kama Mungu zaidi kama ilivyoelezwa na Yona, yaani, “mwenye rehema, si mwepesi wa hasira, na mwenye fadhili nyingi” kwa wote—ikijumuisha sisi wenyewe—katika hali yetu isiyoepukika ya mapungufu.

Mbali zaidi na kudhihirisha athari za Anguko, hadithi ya Yona inatuelekeza kwa nguvu Kwake ambaye anaweza kutukomboa kutokana na athari hizo. Kujitoa dhabihu kwa Yona ili kuokoa wasafiri wenzake ni jambo la dhahiri kama Kristo. Na mara tatu wakati Yesu anapoombwa ishara ya muujiza ya uungu Wake, Yeye asema kwa sauti kwamba “hakuna ishara itakayotolewa … bali ishara ya Yona,” akitangaza kwamba kama vile Yona alivyokuwa “siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi; ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.” Kama ishara ya dhabihu ya kifo cha Mwokozi na Ufufuo mtukufu, Yona anaweza kuwa na dosari. Lakini hii pia ndiyo inafanya ushuhuda wake wa kibinafsi na dhamira kwa Yesu Kristo, iliyotolewa katika tumbo la nyangumi, enye kutia uchungu mwingi na kutia moyo sana.

Kilio cha Yona ni cha mtu mwema aliye katika hali ngumu, ambaye kwa kiasi kikubwa alijiletea mwenyewe. Kwa mtakatifu, maafa yanapoletwa na tabia, maoni, au uamuzi wenye kujutia, licha ya nia nyingine nyingi nzuri na jitihada za dhati za uadilifu, inaweza kuwa mbaya sana na kumwacha mtu ahisi mpweke. Lakini licha ya chanzo au kiwango cha msiba tunaobeba, daima kuna mahali pakavu kwa ajili ya tumaini, uponyaji na furaha. Msikilize Yona:

“Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu … ; toka tumboni mwa kuzimu nililia. …

“Kwa maana ulinitupa kilindini, katikati ya bahari. …

“[Na] nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; lakini nitalitazama tena hekalu lako takatifu.

“Maji yalinizunguka, hata nafsi: vilindi vilinifunika pande zote, Magugu yalinizunguka kichwa changu.

“Nilishuka mpaka chini ya milima; … lakini umeyatoa maisha yangu kutoka katika uharibifu. …

“Nafsi yangu ilipozimia … nalimkumbuka Bwana; maombi yangu yakafika … katika hekalu lako takatifu.

“Wale wanaozingatia ubatili wa uongo waache rehema zao wenyewe.

“Lakini nitakutolea dhabihu kwa sauti ya shukrani; nitalipa kile nilichoweka nadhiri. Wokovu unatoka kwa Bwana.”

Ingawa ilikuwa miaka mingi iliyopita, ninaweza kukuambia hasa mahali nilipokuwa nimeketi, na hasa kile nilichokuwa nikihisi wakati, ndani kabisa ya tumbo la kuzimu ya kibinafsi, niligundua andiko hili. Kwa mtu yeyote leo anayehisi kama nilivyohisi wakati huo—kwamba umetupwa, unazama kwenye kina kirefu cha maji, ukiwa umezungukwa na magugu ya bahari juu ya kichwa chako na milima ya bahari ikikuangukia—ombi langu, lililoongozwa na Yona, ni Usiiache rehema yako mwenyewe. Unaweza kupata msaada wa kimungu na uponyaji mara moja licha ya dosari zako za kibinadamu. Rehema hii ya kuvutia huja kutokana na, na kupitia Yesu Kristo. Kwa sababu Yeye anakujua na anakupenda kikamilifu, Yeye anakupatia kama ya kwako “mwenyewe,” kumaanisha kwamba inafaa kabisa kwako, iliyoundwa ili kupunguza maumivu yako binafsi na kuponya maumivu yako hasa. Hivyo, kwa sababu yako na mbingu, usilipe kisogo hilo. Likubali. Anza kwa kukataa kusikiliza “ubatili wa uwongo” wa adui ambaye angekujaribu kufikiria kwamba unafuu unapatikana kwa kuondoka kutoka kwenye majukumu yako ya kiroho. Badala yake, fuata mwongozo wa Yona aliyetubu. Mlilie Mungu. Geukia hekalu. Shikamana na maagano yako. Mtumikie Bwana, Kanisa Lake, na wengine kwa dhabihu na shukrani.

Kufanya mambo haya huleta ono la upendo wa pekee wa Mungu wa kimaagano kwako—kile ambacho Biblia ya Kiebrania huita hesed. Utaona na kuhisi nguvu za uaminifu, zisizokoma, zisizochoka na “rehema nyororo” za Mungu zinazoweza kukufanya kuwa “hodari … hadi … ukombozi” kutoka kwa dhambi yoyote au kizuizi chochote. Uchungu wa mapema na mkali unaweza kuficha maono hayo mwanzoni. Lakini unapoendelea “kulipa ulichoweka nadhiri,” maono hayo yatang’aa zaidi na zaidi katika nafsi yako. Na kwa maono hayo hautapata tu tumaini na uponyaji, lakini, kwa kushangaza, utapata furaha, hata katikati ya majaribio yako. Rais Nelson alitufundisha vizuri sana: “Wakati lengo la maisha yetu likiwa kwenye mpango wa Mungu wa wokovu … na Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kuhisi furaha bila kujali kile kinachotokea—au kutofanyika—katika maisha yetu. Shangwe inakuja kutoka Kwake na kwa sababu Yake.”

Iwe tunakabiliwa na janga kubwa kama la Yona au changamoto za kila siku za ulimwengu wetu usio mkamilifu, mwaliko ni ule ule: Usiache rehema yako mwenyewe. Tazama ishara ya Yona, Kristo aliye hai, Yeye aliyefufuka kutoka katika kaburi Lake la siku tatu akiwa ameshinda yotekwa ajili yako. Mgeukie Yeye. Mwaminini Yeye. Mtumikie Yeye. Tabasamu. Kwa maana ndani Yake, na Yeye pekee, hupatikana uponyaji kamili na wa furaha kutokana na Anguko, uponyaji ambao sisi sote tunauhitaji kwa uharaka na kuutafuta kwa unyenyekevu. Nashuhudia hii ni kweli. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Alma 27:18. Kikiwa na mistari 48 tu kwa jumla, kitabu cha Yona ni kitabu cha kishairi kilichobanwa cha ukweli mwingi wa mafundisho na masomo ya kiroho. Ona Ellis T. Rasmussen, A Latter-Day Saint Commentary on the Old Testament (1993), 653–57; D. Kelly Ogden and Andrew C. Skinner, Verse by Verse: The Old Testament, vol. 2, 1 Kings Through Malachi (2013), 133–38. Ogden and Skinner note that due to the power of the teachings of repentance in the Book of Jonah, it is “read in synagogues on the holiest day of the year for the Jewish people—the Day of Atonement, or Yom Kippur—which also centers on repentance and forgiveness.”

  2. Ona Ogden and Skinner, Verse by Verse: The Old Testament, 134.

  3. Ona Yona 1–4).

  4. Alma 34:9.

  5. Warumi 3:23.

  6. Ona 2 Nefi 2:17-25.

  7. Yona 42.

  8. Ona Luka 11:29–30; ona pia Mathayo 12:39–41; 16:1–4.

  9. Jonah 2 is a later testimony and psalm of thanks, much of which describes Jonah’s prayer from the belly of the whale.

  10. Kwa njia hii, Yona anatofautiana na mtu kama Ayubu, anayeonekana kuwa hana hatia. Zote mbili ni hadithi za imani na uthabiti katika uso wa janga, lakini za Yona zinaweza kuwa na uhusiano zaidi kwa wale wanaohisi matendo yao wenyewe ndio chanzo cha maumivu na kufadhaika.

  11. Hakika ilikuwa ni kwa Joseph Smith wakati huruma yake ya dhati na shukrani kwa Martin Harris ilimwongoza kushiriki kurasa 116 za thamani za kwanza za Kitabu cha Mormoni ambazo zilipotea na kusababisha Joseph kuomboleza, “Yote yamepotea.” (Ona Saints: The Story of the Church of Jesus Christ in the Latter Days, vol. 1, The Standard of Truth, 1815–1846 [2018], 43–53).

  12. Yona 2:2–9; msisitizo umeongezewa.

  13. 1 Nefi 1:20; ona Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Okt. 2022,6, 10. Neno la asili la Kiebrania la rehema katika Yona 2 ni hesed, ambalo Rais Nelson anaelezea ni “aina maalum ya upendo na rehema” kwa wale ambao wamefanya maagano—rehema anayoeleza ambayo ni mwaminifu, isiyochoka, na isiyoisha.

  14. Russell M. Nelson, “Shangwe na Kunusurika Kiroho,” Liahona,, Nov. 2016, 82.