2025
Bwana Hutazama Moyo
Novemba 2025


10:41

Bwana Hutazama Moyo

Simulizi hii hutufundisha kwamba yote ambayo Mungu anahitaji kukamilisha kusudi lake na kutusaidia kuwa tunavyopaswa kuwa ni kwa kila mmoja wetu kugeuza kikamilifu mioyo yetu kumulekea Yeye.

wakati alipoamriwa kumchagua mfalme mpya wa Israeli kati ya wana wa Yese, nabii Samweli, baada ya kuwa amemwangalia Eliabu, mwana mkubwa wa Yese, alistaajabu kwa ari, “Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.” Lakini Eliabu hakuwa mtumishi aliyeteuliwa wa Bwana. Mwokozi alimwambia Samweli: “Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa: Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.”

Wakati Daudi akiwa si mwenye umbo la mtu mwenye nguvu sana au mwenye ujuzi zaidi ya kaka zake, moyo wake ulikuwa imara mbele za Mungu. Alimpenda Mungu kwa moyo wake wote na alikuwa na hamu kubwa sana ya kumtii. Alikuwa na imani isiyotikisika kwenye upendo wa Mungu, nguvu na baraka zilizoahidiwa kama baadae alivyodhihirisha wakati kwa ujasiri alipopambana na kumshinda Goliati kwa msaada wa Bwana.

Simulizi hii hutufundisha kwamba yote ambayo Mungu anahitaji kukamilisha kusudi lake na kutusaidia kuwa tunavyopaswa kuwa ni kwa kila mmoja wetu kugeuza kikamilifu mioyo yetu kumulekea Yeye. Kwa mwana sheria, Aliamuru, “Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote.” Kwa Nabii Joseph Smith, Alisema, “Tazama, Bwana anahitaji moyo na akili yenye kukubali.” Na kwa Wanefi, Mwokozi aliyefufuka alitoa mwaliko huu: “Na mtatoa kwangu dhabihu ya moyo uliopondeka na roho iliyovunjika.”

Je, kwa nini hivyo? Mwokozi alifundisha kwamba ikiwa mioyo yetu itamgeukia yeye kikamilifu, kwa sababu ya dhabihu Yake ya kulipia dhambi, tunaweza kubarikiwa kwa nguvu na vipawa vya kiroho ambavyo tunahitaji ili kushinda changamoto za maisha yetu duniani, kukinzana na majaribu na kupokea mwongozo na uelewa, na kuhisi shangwe na amani maishani mwetu. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu.” Alisema Yeye anaweza “kuvifanya vitu vidhaifu kuwa vyenye nguvu” na kutubariki kwa kila kitu tunachohitaji ili kufanikiwa katika maisha haya na kupokea uzima wa milele. “Wamebarikiwa wasafi wa moyo, “ Alisema “kwani watamwona Mungu.”

Ninaamini hii ndio sababu, angalau kwa sehemu fulani, Yesu Kristo mara kadhaa aliwasahihisha waandishi na Mafarisayo wakati wa huduma yake duniani. Ingawa walikuwa mahiri kwenye kushika sheria Zake, walifanya hivyo kwa sababu zisizo za kweli. Aliwaonya, akisema, “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.”

Huu ni ukumbusho wa muhimu kwa wafuasi Wake wote kuwa si kuhusu tunayofanya pekee—maneno na matendo yetu— lakini pia kuhusu kwa nini tunafanya ambacho Yesu Kristo ametuamuru kufanya—tamanio na nia zetu. Alisema, “Kwani Mimi, Bwana, nitawahukumu watu wote kulingana na matendo yao, kulingana na tamaa za mioyo yao.” Baba yetu wa Mbinguni anatamani zaidi ya matendo ya kukaririwa ya utiifu na huduma kutoka kwa watoto Wake. Anatutaka tufanye vitu vyema kwa nia ya dhati, kwa sababu tunampend Yeye kwa mioyo yetu yote. Anatutaka tutamani kuwa kama Yeye.

Sasa, ikiwa afya yetu ya kiroho ni kitu ambacho Mwokozi anajali—anachokitazama kwa mfuasi wa kweli—basi tunawezaje kuichunguza mioyo yetu na kujua ikiwa iko sahihi mbele za Mungu?

Hivi karibuni, wakati mke wangu pamoja nami tuliporudi kutoka kwenye misioni yetu huko Ureno, tulifanya vipimo vya afya kutathimini hali zetu. Baadhi ya vipimo hivyo vilifokasi kwenye afya ya moyo—kama vile vipimo vya damu, vipimo vya kuonyesha ndani ya moyo na uwezo wa moyo wa usukumaji damu. Ninaamini kwamba Mwokozi pia ametupatia seti ya vipimo vya kiroho ili kutathimini hali za kiroho za mioyo yetu. Acha nishiriki nanyi baadhi ya hivyo.

Tathimini Moyo Wako kwa Vipimo vya Kiroho

Kwanza, Fokasi yetu, vipaumbele, na kusudi

“Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwa na moyo wako,” Yesu alifundisha. Hazina ni kitu fulani chenye thamani kwetu, kitu fulani ambacho tunaweka uwezo na umakini. Sehemu tunayochagua kutumia muda na umakini wetu, pia kile ambacho hutuhamasisha kufanya tunayofanya, huzungumza zaidi kuhusu mioyo yetu. Mwokozi alionya kwamba wengi Amewaita, lakini wateule ni wachache. “Kwa sababu mioyo yao imekuwa juu ya mambo ya ulimwengu huu, na [wanatafuta] kupata heshima kutoka kwa wanadamu.” Je, ninamuweka Mwokozi kipaumbele kwenye maisha yangu? Je, jicho langu liko kwenye utukufu Wake kwenye vyote nifanyavyo?

Pili, utayari wetu kutii amri za Mungu

Kote kwenye maandiko, Bwana na manabii Wake wamehusisha majivuno na kutotii ikiwa ni pamoja na kushupaza moyo. Nefi aliwasihi kaka zake, akisema: “Kwa nini hamtii amri za Bwana? Kwa nini muangamie, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu?” Kwa waumini huko Missouri, Bwana aliwaonya “Lakini yule asiyefanya lolote mpaka ameamriwa, na kupokea amri kwa moyo wenye mashaka, na kuzishika kwa uvivu, huyo amelaaniwa.” Wakati Mwokozi hategemei ukamilifu katika kutii amri Zake, Yeye hatuamuru tutamani na kujitahidi kuzishika kwa mioyo yetu yote.

Tatu, bidii yetu katika kujifunza maandiko na kutafuta ufunuo

Bwana alimsisitiza Olive Cowdery “kuyatunza maneno haya katika moyo wako” Tunaalikwa kupekua maandiko kwa bidii na, kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, kutafuta kuelewa na ushahidi wa ukweli wa injili katika mioyo yetu.

Nabii Abinadi aliwakanya makuhani waovu wa Mfalme Nuhu kwa kutofanya hili, akisema, “Hamjajitolea mioyo yenu kwa ufahamu; kwa hivyo, hamjawa wenye hekima.” Je, ninafanya juhudi za dhati kujifunza maandiko kila siku na kujitolea moyo wangu kwenye uelewa kupitia sala?

Nne, maneno na mawazo yetu

Mwokozi alifundisha kwamba “moyoni hutoka mawazo mabaya” na kwamba “kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.” Kiwango cha usafi wa mawazo na maneno yetu ni kiashiria cha usafi wa mioyo yetu. Je, ninafurahia mawazo hasi kuhusu matendo au nia za wengine, au hata kuhusu mimi mwenyewe? Je, ninatoa hukumu ya haraka na kulaani wengine? Je, ninatafuta sababu au njia za kuhalalisha makosa yangu? Na vipi kuhusu maneno yangu? Je, yanawainua na kuwapa msukumo wale wanaonizinguka? Au mara zote yanatengeneza mgogoro na msuguano?

Baada ya uchunguzi wa afya yangu kukamilika, daktari wangu aliniambia kwamba, kiujumla, moyo wangu ulikuwa sawa—lakini kulikuwa na vitu vichache ambavyo vilihitajika kushughulikiwa sasa, kabla havijaleta madhara makubwa. Kisha alifafanua baadhi ya mabadiliko kwenye mfumo wa maisha. Vivyo hivyo, wakati unapofanya tathimini hii ya kiroho ya moyo wako na kugundua baadhi ya dalili hasi zikianza kunyemelea, tafadahali usihamaki! Mwokozi ametoa dawa bora zaidi ya kiroho na matibabu ili kukusaidia. Hata ameahidi kukupa moyo mpya! Haya ni baadhi ya matendo ambayo yanaweza kuboresha nguvu ya kiroho ya moyo wako.

Boresha Afya ya Kiroho ya Moyo Wako

Kwanza, Imarisha uhusiano wako na Kristo

Tunapotoa muda kila siku kumkaribia Kristo, mioyo yetu inabadilishwa. Kujifunza maandiko kila siku, kunakosindikizwa na sala ya dhati na kufunga mara kwa mara, kutaongeza upendo wako kwa Mwokozi na kuimarisha imani yako na hamu ya kutubu na kwa unyenyekevu kuutoa moyo wako kwa Mungu. Zingatia mfano huu kutoka kwa Nefi: “Nilimlilia Bwana, na tazama akanijia mimi, na akanigusa moyo wangu kwamba nikaamini maneno yote ambayo baba yangu alikuwa ameyazungumza.”

Tunapoendelea kuikuza mbegu ya imani kupitia hamu na matendo yetu matakatifu, tutapata uzoefu sawa wa utakaswaji wa moyo kama wa Wanefi: “Walakini walifunga na kuomba kila wakati, na wakapokea nguvu kwa wingi katika unyenyekevu wao, na wakawa imara zaidi na imara katika imani kwa Kristo, hadi nafsi zao zikajazwa na shangwe na faraja, ndiyo, hata kwenye kusafishwa na utakaso wa mioyo yao, utakaso ambao huja kwa sababu ya wao kumtolea Mungu mioyo yao.”

Pili, Weka Mapenzi Yako Sawa na ya Yake.

Mwokozi alifundisha, “ Mkinipenda, mtazishika amri zangu.” Anatualika tuonyeshe upendo wetu kwa kufanya na kushika maagano Naye. Tunapojitahidi kila siku kushika amri Zake, kwa dhati kutubu dhambi zetu, na kuvumilia kwenye kujichukulia juu yetu jina lake na kuweka mapenzi yetu kuwa sawa na Yake, tunaweza kubarikiwa na uwepo wa daima wa Roho Mtakatifu.

Nefi alishuhudia: “Najua kwamba kama mtamtii Mwana, kwa moyo wa lengo moja, bila unafiki na udanganyifu mbele yake Mungu, lakini kwa kusudi kamili, na kutubu dhambi zenu, mkishuhudia kwa Baba kwamba mnataka kujivika juu yenu jina la Kristo, kwa ubatizo … , ndipo mtapokea Roho Mtakatifu.” Roho Mtakatifu atakuongoza na kukusaidia kujua mapenzi ya Bwana na kufanya chaguzi njema.

Mwisho, Mtumikie Mungu na Wengine kwa Moyo Wako Wote

Mwokozi anawaalika wote “kumtumikia kwa moyo wote.” Wakati tunapochagua kufanya kila kitu ambacho Bwana anatuamuru kufanya—kama vile kutii amri zake, kushiriki sakramenti, kuabudu hekaluni, na kuwatumikia wengine—kwa moyo wa dhati na kwa nia ya dhati, kila tendo la huduma na kuabudu huwa uzoefu wa kiroho wenye nguvu ambao utaimarisha imani yetu na ushuhuda na kujaza mioyo yetu kwa shangwe na upendo kwa Mungu na wenzetu.

Swali la nabii Alma bado linatoa mwangi hivi leo: “Je, mmezaliwa kiroho katika Mungu? Mmepokea mfano wake katika nyuso zenu? Mmeshuhudia mabadiliko haya makuu katika mioyo yenu?”

Akina kaka na dada, ninawaalika kuutoa moyo wako wote kwa Mwokozi hivi leo. Acheni kila tendo la kuabudu na huduma liwe la dhati na la kusudi jema. Ondoa vivuta mawazo vya ulimwengu na jitahidini kuwa na muda maalum kwa ajili ya Bwana kila siku za maisha yako. Tubu na mrudie Yeye kwa moyo wote, na Yeye atakusamehe na atakuzingira kwa mikono Yake ya upendo. Usitafute mambo ya ulimwengu huu, lakini chagua kuwa na jicho lako kwenye utukufu Wake pekee na tafuta vitu bora zaidi. Yeye anajua mawazo yako na hamu za moyo wako, na unapomwendea Yeye, Atakubariki kwa nguvu, ujasiri, amani, na shangwe katika maisha haya na sehemu kwenye ufalme Wake wa selestia milele yote.

Ninajua Yesu Kristo yu hai. Yeye ni Mkombozi wetu. Na Anakupenda wewe na mimi kwa moyo wote. Katika jina la Yesu Kristo, amina.