Na Sasa Ninaona
Matokeo ya Kitabu cha Mormoni maishani mwangu ni ya muujiza sawa na matumizi ya mate na udongo vilivyowekwa kwenye macho ya mtu kipofu.
Kwa upendo wa dhati sote tunatambua heshima ya Rais Oaks kwa Rais Russell M. Nelson ambaye amefariki. Na kwa upendo sawa na huo na majonzi mengi, sote tunatambua majanga huko Michigan hivi karibuni na karibia kila siku kote ulimwenguni. Tunatambua mambo haya kwa upendo na tumaini katika Bwana Yesu Kristo.
Kwenye Sura ya tisa ya kitabu cha Yohana inaelezea uzoefu wa Yesu na wanafunzi Wake wakipita karibu na omba omba, kipofu tangu kuzaliwa. Hii ilipelekea wanafunzi kumuuliza Yesu baadhi ya maswali magumu ya kidini kuhusu kiini na mapungufu ya mtu huyu. Bwana alijibu kwa kufanya kitu fulani rahisi na cha kushangaza. Alitema mate chini akafanya tope kwa yale mate. Kisha akaweka kwenye macho ya mtu huyu, akimwelekeza kwenda kunawa kwenye birika la Siloamu. Mtu huyu kipofu kwa utiifu alifanya hivyo na “[akarudi] akiwa amepona,” maandiko yanasema. Ni jinsi gani jambo hili lilivyo la muhimu, kuliko matamanio au mabishano au hata kinyongo vinavyopinga ukweli.
Ndio, kwa kuhofia kwamba muujiza huu ungeongezea kwenye kutetereka kwa mamlaka ambayo walikuwa wanadhani wanayo, maadui wa Mwokozi walimfuata aliyekuwa ameponywa na kusema kwa hasira, “Tunajua [Yesu] ni mtenda dhambi.” Mtu huyu aliwasikiliza kwa muda, kisha akajibu, “Kama yeye ni mwenye dhambi … , mimi sijui: [lakini] [nina] hakika na jambo moja: nilikuwa kipofu na sasa naona.”
Yesu alitoa maana ya kwanza kwenye mazungumzo yale, akiwaambia wanafunzi Wake kwamba haya yote yametendeka ili kwamba “kazi za Mungu zidhihirishwe.” Kumbuka kwamba mara mbili katika maelezo haya kitendo cha Mwokozi kilirejelewa kama “kupaka” macho ya mtu kipofu, kitendo ambacho kilikamilishwa na uoshwaji. Maelezo haya ya “kazi za Mungu [kuweza] kudhihirishwa” yangeweza kupendekeza kutendeka kwa ibada.
Ukweli mwingine ambao ni wazi hapa ni kuhusu vyombo ambavyo Muumba wa mbingu na nchi alivitumia kufanya muujiza huu: mate na kiasi cha udongo! Vitu hivi ambavyo si vya kudhaniwa vinaonyesha kwamba Mungu anaweza kutubariki kwa njia yoyote anayochagua. Kama Naamani akiukataa Mto Yordani au watoto wa Israeli wakikataa kumwangalia nyoka wa shaba kwenye fimbo, huwa ni rahisi kiasi gani kwetu kukataa chanzo cha ukombozi wetu kwa sababu vyombo vinavyotumika ni vya kawaida kabisa.
Lakini tunakumbuka kutoka katika Kitabu cha Mormoni kwamba baadhi ya vitu ni vya wazi na vya thamani na kwamba kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, ungetolewa unabii kwamba “Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.” Ni mara ngapi Mungu ametuma ujumbe Wake mkuu kupitia rais wa Muungano wa Usaidizi mpya na mwenye hofu au mvulana asiye na elimu huko shamba la new York au mtoto aliyelala horini.
Basi, vipi ikiwa jibu la sala zetu linakuja katika uwazi, au kwa kukanganya? Je, tuko tayari kustahimili, kuendelea kujaribu kuishi injili ya Kristo bila kujali ni kiasi gani cha mate na udongo kitatumika? Inaweza isiwe bayana daima kwetu namna inavyofanyika au kwa nini, kadiri muda unavyoenda, sote tutahisi kwa kiasi kama alivyohisi dada aliyesema, “Bwana vipi kuhusu baraka ambayo haijafichwa?”
Zingatia ushahidi wa ukweli mwingine, ukweli huu unahusiana na ukuhani mtakatifu. Katika kuandika mpangilio wa Kanisa la wakati wa Yesu, mstari wa kwanza wa Luka unasema, “Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka,” vipawa ambavyo havitolewi kulingana na hadhi za kuvutia wala kuamuliwa kulingana na tamaduni au haki ya uzaliwa. Havitolewi kupitia shule ya dini au seminari ya teolojia. Vinatolewa kwa kuwekewa mikono na mtu ambaye naye aliwekewa mikono na mtu aliyeidhinishwa katika mpangilio wenye mwendelezo mpaka kwenye chanzo cha mamlaka matakatifu yote, Bwana Yesu Kristo.
Na katika kanisa linaloelewa kipawa cha rehema, je hautakuwa ushahidi mwingine mkuu wa unyoofu wa kanisa ili kuona baraka hizi na maagano vikienda kwa uzao wetu wa walio wafu, wale wa familia zetu ambao wametutangulia? Je, wanapaswa kupata adhabu kwa sababu hawakuweza kuisikia injili au kwa sababu walizaliwa katika kipindi au mahali ambapo ibada takatifu na maagano havikupatakina kwao? Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lina nyumba takatifu za Bwana zilizowekwa wakfu ambamo kazi ya rehema na uokozi inafanyika kwa uwakilishi kila asubuhi mchana na jioni kwa niaba ya wafu hawa, vile vile utoaji wa fursa za kuabudu na ibada kwa walio hai. Kwa uelewa wangu, ushahidi huu hasa wa ukweli wa Mungu, upendo Wake kwa wote usio na kikomo kwa ajili ya wanaoishi na wafu, hauonekani popote ulimwenguni—isipokuwa kwenye kanisa moja ambalo linadai ukweli kwenye jambo hili hasa: Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
uzoefu wangu wa kwanza wa kuona, wa maisha wa uthibitisho wa ukweli halisi, haukuja kwa kuwekewa tope au katika birika la Siloamu. Hapana, chombo cha ukweli ambacho kilileta uponyaji wangu kutoka kwa Bwana kilikuja kama kurasa za kitabu, ndio, Kitabu cha Mormoni: Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo! Madai kuhusu kitabu hiki yameshambuliwa na kupuuzwa na wasioamini, hasira yao mara nyingi ikilinganishwa na lugha ya upinzani ya wale waliomwambia mtu aliyeponywa kuwa asingeweza kuwa na uzoefu wa alichokijua kuwa alikipitia.
Nimetupiwa hayo kwamba njia ambazo kwazo kitabu hiki kilikuja zilikuwa si za kujulikana, zisizoaminika, za kuudhi na hata zisizo takatifu. Sasa, hiyo ni lugha kali kutoka kwa mtu yoyote anayedhania anajua njia ambazo kwazo kitabu hiki kilikuja, ingawaje maelezo pekee yalitolewa kuhusu njia hizo ni kwamba kilitafsiriwa “kwa kipawa cha Mungu.” Hivyo ndivyo ilivyo. Hayo ndio yote. Katika hali yoyote, matokeo ya Kitabu cha Mormoni maishani mwangu ni ya muujiza sawa na matumizi ya mate na tope vilivyowekwa kwenye macho ya mtu kipofu. Kimekuwa, kwangu mimi, fimbo ya usalama kwa ajili ya nafsi yangu, nuru ya ufunuo ya muujiza na yenye kupenyeza, mwangaza kwenye njia ninayotembea wakati ukungu wa giza unapokuja. Na hakika ukungu huo upo, na hakika utakuja.
Na kwa uelewa ambao kimenipa kuhusu upendo usio na kikomo wa Mwokozi na neema ya kuokoa, ninashiriki nanyi ushuhuda wangu, uliothibitishwa kwa njia sawa na vile wazazi wa mtu mbarikiwa walivyosema kwamba mwana wao angepaswa kusikilizwa kwa sababu yeye ni “mtu mzima.” Basi, nami pia ni mtu mzima. Walimaanisha, alikuwa mtu mzima vya kutosha kusikilizwa. Vivyo hivyo, mimi pia. Nimebakiza miezi miwili kabla ya kufikisha miaka 85. Nimewahi kuwa kwenye ukingo wa mauti na nikarejea. Nimetembea na wafalme na manabii, maraisi na mitume. Zaidi ya yote, wakati mwingine nimezidiwa na Roho Mtakatifu wa Mungu. Ninatumaini kwamba ushuhuda wangu angalau ungepaswa kupewa tafakuri hapa.
Sasa, akina kaka na dada, nimeshawishika kwa nafsi yangu yote kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni urejesho wa kweli wa Kanisa la Agano Jipya—na zaidi—kwa sababu nisingeweza kukataa ushahidi wa urejesho huo. Tangu uzoefu ule wa kwanza, nafikiri nimekuwa na maelfu—makumi elfu?—ya ushahidi mwingine kwamba kile nilichoongelea leo ni cha kweli. Hivyo, ninafurahia sasa kuungana na rafiki yangu aliyejibana kwenye mitaa ya Yerusalemu ambapo ninaimba na sauti yangu hafifu:
Katika jina la Yesu Kristo, amina.