Darasa Jipya, Fursa Mpya
Kuhamia katika darasa jipya au akidi mpya? Hapa kuna mambo machache tu ya kutazamia!
Vielelezo na Cinta Fosch
Mwanzo wa mwaka mpya mara nyingi huleta mabadiliko makubwa—ikijumuisha uwezekano wa kufanya mabadiliko kwenye darasa tofauti au akidi tofauti kanisani! Iwe unaondoka kwenye darasa la Watoto, ukiingia kwenye Muungano wa Usaidizi au akidi ya wazee, au kuhamia tu kwenye darasa linalo fuata la Wasichana au akidi ya Ukuhani wa Haruni, hapa kuna mambo matatu ya kutazamia.
1 Watu Wapya
Inaweza kuonekana ya kutisha kuwa katika darasa pamoja na watu ambao ni wakubwa kuliko wewe, lakini mnayo mengi mnayofanana kuliko unavyofikiria. Ninyi nyote ni wanafunzi wa Yesu Kristo ambao mnajaribu kumfuata Yeye. Kubadili madarasa ni fursa ya kusikia utambuzi mpya kutoka kwa watu wenye uzoefu tofauti na wewe—na nafasi ya kufanya marafiki wapya.
2 Shughuli Mpya
Programu za Wavulana na Wasichana ni za kuburudisha! Unaweza kuwa na njia mpya za kuunganika na vijana wengine, ikijumuisha shughuli za darasa za akidi na za makambi. Mara unapokuwa na miaka 14, unaweza pia kuwa na mikutano ya KNV, dansi, na seminari.
Kama kijana mkubwa, unaweza kuhudhuria chuo na shughuli zilizopangwa na Muungano wa Usaidizi, akidi ya wazee, au vijana wakubwa waseja katika kata au mahali pa kukusanyika.
3. Faida Mpya
Unapozidi kukua, unakuwa na fursa zaidi za kuhudumu katika Kanisa, kama vile kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu, kubariki sakramenti, au kutimiza wito (ikijumuisha kupangiwa kuwa mtumishi). Tumia fursa hizi kwa ajili ya ukuaji wa kiroho na furahia jinsi zinavyoimarisha uhusiano wako na Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na watu unao wahudumia.
Unapofanya mabadiliko ndani ya darasa jipya, kumbuka kwamba“ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu” (Wagalatia 3:28). Unapoweka uzoefu wa kanisa lako kumzunguka Yeye, Yeye atakusaidia kupata shangwe popote ulipo.