Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Anguko: Adamu na Hawa
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Hadithi kutoka Agano la Kale

Angukol: Adamu na Hawa

Musa 2–4; Mwanzo 2-3

Anguko: Adamu na Hawa

Pakua PDF

Vielelezo na Katy Dockrill

Hadithi Yao

Bustani

Adamu na Hawa waliishi katika Bustani ya Edeni—bustani nzuri ambapo hawatapata maumivu, magumu, kifo, au shangwe. Wangeweza pia kufurahia uwepo wa Mungu.

Majaribu

Baba wa Mbinguni aliwaamuru kuwa na watoto na wasile tunda kutoka “mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” Shetani aliwajaribu Adamu na Hawa kula lile tunda.

Uchaguzi

Hawa na Adamu walichagua kula lile tunda. Wangelazimika kuondoka bustanini na kwenye uwepo wa Mungu, kupitia magumu, na hatimaye kufa. Lakini pia wangeweza kuwa na shangwe, kushika amri ya Mungu ya kuwa na watoto, na kuendelea kuelekea uzima wa milele.

Mpango

Mwanzoni, Adamu na Hawa walijificha. Lakini wakijifunza kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni, walijua kwamba uchaguzi wao uliwaruhusu watoto wa Baba wa Mbinguni kuja duniani. Walijifunza kwamba Baba wa Mbinguni angemtuma Yesu Kristo kuwaokoa wao (na sisi) kutokana na dhambi zetu na kifo.

Hadithi Yako

Kama Adamu na Hawa, wewe unaishi katika ulimwengu wenye shida na majaribu, na wakati mwingine unaweza kuhisi kama kujificha au kuhisi hofu. Lakini kwa sababu ya Yesu Kristo, unaweza kutubu na kubadilika. Siku moja utafufuliwa na unaweza kurudi kuishi naye.