Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ahadi za Thamani za Mpango wa Baba
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Ahadi za Thamani za Mpango wa Baba

Nafsi zetu zinapaswa kuvimba kwa shukrani tunapofikiria mpango mkuu wa Mungu kwa ajili yetu.

mvulana kwa umakini mkubwa akiunganisha miisho miwili ya daraja pamoja

Vielelezo na Alyssa Petersen

Mpango wa Baba wa Mbinguni unaelezea “ahadi kubwa mno na za thamani” (ona 2 Petro 1:3–4) na kweli zinazofafanua utambulisho na dhumuni letu la milele.

Kama ilivyoelezwa katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu”: “Wanadamu wote—wanaume na wanawake—wameumbwa katika mfano wa Mungu. Kila mmoja ni mwana au binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni, na, kwa hivyo, kila moja ana asili takatifu na takdiri.”

Baba wa Mbinguni anatuahidi kwamba tukifuata mpango Wake na mfano wa Mwanawe Mpendwa, kushika amri Zake, na kuvumilia kwa imani hadi mwisho, “tutapata uzima wa milele, kipawa ambacho ni kikuu zaidi ya vipawa vyote vya Mungu” (Mafundisho na Maagano 14:7).

Kazi ya Mungu imefokasi juu ya maendeleo na kuinuliwa kwa watoto Wake. Kila sehemu ya mpango Wake imesanifiwa ili kutubariki sisi kwa sababu “thamani ya nafsi ni kuu [mbele Yake]” (Mafundisho na Maagano 18:10).

Mpango wa Baba

Katika baraza kabla ya kuja duniani, Baba wa Mbinguni aliwasilisha kwa watoto Wake wa kiroho mpango Wake kwa ajili ya maendeleo na furaha yao ya milele. Yeye alituambia angetupeleka duniani ili kutujaribu, ili kuona kama tutamtii Yeye na kustahili “kuongezewa utukufu juu ya vichwa [vyetu] milele na milele” (ona Ibrahimu 3:24–26).

Na kisha Yeye akasema: “Nimtume nani? Na mmoja aliyekuwa mfano wa Mwana wa Mtu akajibu: Niko hapa, nitume mimi. Na mwingine akajibu na kusema: Niko hapa, nitume mimi. Naye Bwana akasema: Nitamtuma wa kwanza.

“Na wa pili akakasirika, … na, siku ile, wengi walimfuata” (Ibrahimu 3:27–28).

Mpango mmoja tu uliwasilishwa—mpango wa Baba. Baba yetu wa Mbinguni hakuuliza swali, “Je, Tutafanya nini?” Hakutafuta mchango wa mawazo, kuomba mapendekezo, au kuomba maoni. Kiini cha swali Lake kililenga kwa nani anapaswa kutumwa kutekeleza vigezo na masharti ya mpango Wake.

dunia pamoja na jua, mwezi, na nyota

Lusiferi hakuwasilisha mpango ambao ulipigiwa kura na wengi wa washiriki katika baraza kabla ya kuja duniani. Aliasi! Alitafuta kuangamiza haki ya kujiamulia ya mwanadamu, akatupwa chini, na “akawa Shetani, … ibilisi, baba wa uongo wote, ili kudanganya na kuwapofusha wanadamu, na kuwaongoza utumwani kadiri apendavyo” (ona Musa 4:1, 3–4). Kiburi, majivuno, na ubinafsi vilichochea uasi wake dhidi ya mpango wa Baba.

mvulana, Yesu Kristo, na mpango wa wokovu

Mpango wa Baba na Injili ya Mwokozi

Mpango unaelezea kazi za Baba na Mwana ambazo zinafanya baraka za uzima wa milele zipatikane kwa wanadamu wote.

Injili ya Yesu Kristo ndiyo njia ambayo kwayo tunapokea baraka zilizoahidiwa katika mpango wa Mungu, hata mafundisho, kanuni, ibada, na maagano ambayo lazima tuyaamini na tuyafuate. “Hakuna jina lingine ambalo limetolewa chini ya mbingu ila tu awe huyu Yesu Kristo … ambalo kwamba mwanadamu anaweza kuokolewa” (2 Nephi 25:20). Hakika, Bwana Yesu Kristo “ndio njia, kweli, na uzima: mtu haji kwa Baba, ila kwa njia [Yake]” (Yohana 14:6; mkazo umeongezwa).

kitabu kikiwa na mpango wa wokovu uliochorwa ndani yake

Majina ya Mpango huo katika Kitabu cha Mormoni

Tunajifunza kweli muhimu kwa kutambua na kujifunza majina mengi tofauti ya mpango wa Baba katika Kitabu cha Mormoni: Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo. Kwa mfano, fikiria sampuli ifuatazo zilizochaguliwa za majina hayo:

Kila moja ya majina haya hutusaidia kuelewa kwa uwazi zaidi ahadi za thamani za mpango wa Baba na unarutubisha mtazamo wetu kuhusu madhumuni na maana ya maisha yetu ya duniani.

Cha muhimu, ni kwamba jina litumikalo mara kwa mara kwa ajili ya mpango wa Mungu katika Kitabu cha Mormoni (“mpango wa ukombozi”) linafokasi kwenye ukombozi kutokana na dhambi na kifo uliofanywa uwezekane kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Alma 12:25; 33:22).

Njia Hii Imeandaliwa.

Nafsi zetu zinapaswa kuvimba kwa shukrani tunapofikiria mpango mkuu wa Mungu. Ufahamu wa mpango Wake unatoa mtazamo wa thamani, unarutubisha furaha yetu, na kutuimarisha ili tuzishinde changamoto na dhiki zetu.

Baba wa Mbinguni anatamani sisi turudi nyumbani kwake Yeye. Yeye anatualika na kuahidi baraka, lakini Yeye kamwe hatatulazimisha, hatatushurutisha, au kuzuia matumizi yetu ya maadili ya haki ya kujiamulia aliyotupatia. Lazima tutende na kuchagua kurudi Kwake kwa kufuata mfano wa Mwanawe Mpendwa.

Njia imetayarishwa, na ikiwa tutaangalia tutaishi milele” (Alma 37:46; mkazo umeongezwa).

Kwa shangwe ninatoa ushahidi kwamba Baba wa Mbinguni ni mtunzi wa mpango mtakatifu kwa ajili ya watoto Wake. Yesu Kristo ni Mkombozi na Mwokozi wetu. Na kama mmoja wa Mitume Wake wa siku za mwisho ninatoa ushahidi kwamba hakika Yeye ndiye “ njia, kweli, na uzima” (Yohana 14:6; mkazo umeongezwa).