Sauti za Vijana
Kujifunza Baada ya Kumpoteza Bibi Yangu
Kielelezo na Katelyn Budge
Kumpoteza bibi yangu ilikuwa changamoto kwangu. Tulikuwa karibu sana. Nilihisi kuwa mwenye huzuni sana. Nilihisi kuwa tumaini nililohitaji lilikuwa limetoweka.
Kabla hajafariki, sikuwa na nguvu sana katika injili ya Yesu Kristo. Nilikuwa nikitegemea shuhuda za wengine. Lakini katika wiki hiyo ya kwanza ya huzuni, nilienda kwenye darasa la dini ambapo mwalimu alifundisha kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo na mpango wa Baba wa wokovu. Niligundua kwamba nitaweza kumwona bibi yangu tena. Tunaweza kuungana tena katika maisha yajayo kupitia ibada za hekaluni.
Hii iliimarisha ushuhuda wangu. Nilianza kufokasi zaidi juu ya Mwokozi wangu Yesu Kristo na kujifunza zaidi kuhusu injili Yake. Sasa ninatafuta majibu kupitia maandiko na Njoo, Unifuate. Ninapenda kusikiliza hotuba za mkutano mkuu, hasa kutoka kwa nabii, Rais Russell M. Nelson. Ninaposikiliza hotuba, kutegemea maandiko, kusali na kutafakari, na kumwomba Roho Mtakatifu, ushuhuda wangu unaweza kuwa imara.
Seminari pia imenisaidia kujifunza kuhusu na kujitahidi kuwa kama Mwokozi wetu, Yesu Kristo, kadiri nilivyotenda kwa imani, kutazama vitu kwa mtazamo wa milele, na kutafuta ufahamu zaidi kupitia vyanzo vilivyoteuliwa.
Kuwamini Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo Usitegemee tu ufahamu wako mwenyewe bali Wao. Wanaweza kutusaidia na kutuongoza kupitia majaribu au taabu yo yote tunayoweza kukabiliana nayo.
Suzanne Q., umri miaka 17, Central Division, Fiji
Anapenda kuchora, kuchonga sanaa, kupaka rangi, kusanifu, kujifunza kuhusu historia, na kucheza mpira wa kikapu.