Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Mwaka Mpya
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Mwaka Mpya

Emily Belle Freeman

Ni Januari! Mwaka mpya. Wakati wa mwanzo mpya.

Labda utaweka lengo kwa mwaka huu mpya. Baadhi ya watu huchagua neno ili kuwakilisha nia yao kwa mwaka ulio mbele. Mwaka huu, vijana kote ulimwenguni watakuwa wanafokasi kwenye aya hii hii ya maandiko: Musa 6:34, “Tembea pamoja Nami.” Huu ulikuwa ni mwaliko uliotolewa kwa nabii Henoko.

Henoko alipokuwa akisafiri katika nchi, Roho wa Mungu alitulia juu yake. Kisha Bwana aliongea naye. Alimfundisha kuhusu mpango Wake wa furaha, ambao ungetoa madhumuni na maana ya maisha. Bwana alipomaliza kuelezea Mpango Wake, alimpatia Henoko mwaliko: “Tembea pamoja nami.”

Unaposafiri katika mwaka huu mpya, pengine utajikuta unatafuta furaha, lengo, na maana. Ungeweza kujifunza kutoka kwenye hadithi ya Henoko na kumwalika Bwana kuwa sehemu ya safari yako mwaka huu.

Ungeweza kuchagua kutembea pamoja Naye. Unapofanya hivyo, baraka zinakusubiri.

Utakuwa mwaka mzuri.

Kwa upendo,

Emily Belle Freeman

Rais Mkuu wa Wasichana