Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ramani Yako ya Kurudi Nyumbani
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Ramani Yako ya Kurudi Nyumbani

Kwa Nini Ni Muhimu sana Kuelewa Mpango wa Wokovu?

ramani

Kielelezo na Mackenzie Alexander

Katika Kitabu cha Mormoni, nabii Yoramu alianza kumbukumbu yake kwa kusema, “Kwani naweza kuandika nini zaidi ya yale baba zangu waliyoandika? Kwani si wamefunua kuhusu mpango wa wokovu? (Yaromu 1:2)

Kama yeye alifikiri hayo ndiyo yote tuliyohitaji, mpango wa wokovu lazima uwe muhimu sana!

Na ndivyo ilivyo! Ni ramani kamili kwa ajili ya maisha yetu. Rais Russell M. Nelson wakati mmoja alisema, “Uelewa juu ya mpango wa Mungu wenye kupendeza huondoa sintofahamu katika maisha yetu na kutokuwa na uhakika juu ya siku zijazo.”

Kwa hiyo ramani hii inawezaje kukusaidia kutafiti kutokuwa na uhakika kwa maisha?

Mimi nimetoka wapi?

Mungu ni Baba yako wa Mbinguni. Uliishi na Yeye kabla haujazaliwa. Yeye anakupenda!

Mzee Alan T. Phillips wa Sabini alielezea, “Wewe sio tunda la bidhaa ya asili lililotokana na ajali, au yatima wa badiliko la dunia, au jambo la matokeo ya maada jumlisha na muda jumlisha na nafasi. Panapokuwa na usanifu, kuna msanifu.”

Maisha yanapokuwa magumu, ni faraja kujua kwamba uko hapa kwa kusudi na unatazamwa na Baba wa Mbinguni mwenye upendo.

Ninakwenda Wapi?

Hauko hapa kutangatanga bila kusudi—unao mwisho wa safari! Baba wa Mbinguni anakutaka wewe uje nyumbani Kwake na uwe kama Yeye. Aliandaa mpango wa wokovu ili uweze kupokea baraka zote za ufalme Wake (ona Mafundisho na Maagano 14:7).

Kujua mpango wa Baba wa Mbinguni kutakusaidia maisha yako yote. “Unapochukua mtazamo mrefu” na kufikiria selestia, chaguzi nyingi zinakuwa rahisi kufanya—ikijumuisha kuchagua kumfuata Yesu Kristo.

Je, Ninafikaje Huko?

Mbali na kutupatia sisi hatima, mpango wa wokovu pia unaonyesha njia ya kufika huko.

Yesu Kristo ni mfano mkamilifu wa kufuata njia ya kurudi nyumbani. Kama utamtazama Yeye—na kutembea pamoja Naye—Atakusaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni na kuwa zaidi kama Yeye. Kama Mzee Sergio R. Vargas wa Sabini alivyo elezea, “Ndani kabisa ya kila mmoja wetu ni hamu ya kurejea nyumbani kwetu mbinguni, na Yesu Kristo ndiye mfumo wetu wa mwongozo wa mbinguni. Yeye ndiye njia.”

Vipi Kama Nikipotea?

Hata kwa ramani, unaweza kufanya makosa ya njia isiyo sahihi. Bado utafanya makosa. Lakini usiwe na wasiwasi! Baba wa Mbinguni alitupatia Mkombozi ili daima uweze kutubu, kurudi Kwake, na kuwa zaidi kama Yeye. Kumbuka: “Hatubaki kwenye njia ya agano kwa kutofanya kosa kamwe. Tunabaki kwenye njia ya agano kwa kutubu kila siku.”

Unapojifunza mpango wa wokovu, kumbuka kwamba ulisanifiwa kwa upendo. Baba wa Mbinguni anakutaka uje nyumbani. Na kama utafuata ramani Yake, Yeye atakusaidia kufika huko.