Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Vigugumizi Sala ya Sakramenti
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Sauti za Vijana

Vigugumizi Sala ya Sakramenti

mvulana akiwa kwenye meza ya sakramenti

Kielelezo na Katelyn Budge

Nina kikwazo cha kusema kwa ufasaha ambacho kinanifanya kuwa na kigugumizi katika hali tofauti tofauti, ikijumuisha wakati nikibariki sakramenti. Mwanzoni, ilikuwa changamoto kweli. Hata nilifikiria kuhusu kutobariki sakramenti tena.

Lakini nilianza kusali kwa Baba wa Mbinguni. Nilisali Kwake daima, nikiomba msaada Wake. Ninashuhudia kwamba Yeye anasikia sala zetu. Baada ya muda, vilianza kupungua.

Mara chache bado ninakuwa na vigugumizi, lakini Mwokozi amekuwa akinisaidia kushinda changamoto hii. Kupitia mateso Yake katika Bustani ya Gethsemane, Yeye anaelewa kile ninachohisi katika hali hii.

Pia ninakabiliana na changamoto hii shuleni. Mwanzoni, ilikuwa vigumu kwa sababu watu walinicheka. Lakini nilihisi upendo wa Mwokozi katika maisha yangu. Alinifariji na kunisaidia.

mvulana

Daniel S. A., miaka 17, Rio de Janeiro, Brazili

Anapenda kucheza mpira wa kikapu, kubariki sakramenti, na kuwa na jioni ya familia nyumbani.