Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Tembea pamoja Nami: Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2026
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2026

Tembea pamoja Nami

Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2026

msichana

Vijana kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanaoneshwa katika video ya muziki wa Dhima ya Vijana kwa mwaka 2026.

Wakati unapotembea kwenye moto

Na miguu yako imechakaa na kuogopa,

Kuna chanzo cha maji ya uzima

Ambacho kinaweza kuponya moyo wako uliochoka.

Unaona nyayo za Mwokozi,

Na unahisi nuru Yake inayoongoza.

Anakuita wewe.

Yeye anasema:

[Kiitikio]

Tembea pamoja Nami

Nitatuliza maji yako yaliyo na matatizo.

Tembea pamoja Nami;

Nitahamisha milima yako.

Ee, shika mkono wangu

Unapohisi moyo mzito.

Tembea pamoja Nami,

Nami nitatembea nawe.

Alitembea barabara kuu za jangwani

Kwenda na kumtafuta yule mmoja.

Alimwinua aliyevunjika

Akauonyesha ulimwengu upendo Wake.

Na tunapotembea kando Yake,

Yeye hutupatia nguvu Zake.

Anakuita wewe.

[Kiitikio]

Tembea pamoja Nami

Na nitatuliza maji yako yaliyo na matatizo.

Tembea pamoja Nami

Nitahamisha milima yako.

Ee, shika mkono wangu

Unapohisi moyo mzito.

Tembea pamoja Nami

Nami nitatembea pamoja nawe.

Tembea pamoja na Mwokozi

Je, unapitia wakati mgumu? Je, unaanza kitu kipya, cha kusisimua, au cha kuogopesha kidogo?

Kamwe hupaswi kupitia haya yote peke yako.

Mwokozi wako Yesu Kristo atatembea nawe kupitia cho chote unachokabiliana nacho.

Anakualika kutembea pamoja Naye.