Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2026
“Tembea pamoja Nami”—Acha Tuivunje
Dhima ya mwaka huu ni ya urefu wa maneno matatu, lakini kila moja ya maneno hayo lina mengi ya kutufundisha.
Kama dhima ya vijana kwa mwaka uliopita, “Mtegemee Kristo,” dhima ya mwaka huu—“Tembea pamoja Nami”—ni mfano wa hotuba. Katika maisha haya, wengi wetu hatutakuwa na fursa ya kuona au kutembea na Mwokozi kiuhalisia. Kwa hiyo inamaanisha nini “tembea” pamoja na mtu ambaye kimwili hayuko hapo? Hebu tuivunje hiyo:
Tembea
Bwana alipomwita Henoko kuwa nabii, Yeye alimpatia ahadi: “Maneno yako yote nitayahesabia haki; na milima itakukimbia mbele zako, na mito itageuka kutoka uelekeo wake; nawe utakaa ndani yangu, nami ndani yako; kwa hiyo tembea pamoja nani” (Musa 6:34).
Kama ungeahidiwa kwamba kutembea pamoja na Mungu kulimaanisha Yeye angeunga mkono maneno yako, kuondoa vizuizi katika njia yako, na daima kuwa pamoja nawe—vyema, kwa nini usitembee Naye?
Habari njema: Mmeahidiwa hili, labda hivi karibuni kama Jumapili iliyopita. Unapopokea sakramenti wewe unaahidi, “daima kumkumbuka Yeye na kushika amri Zake”—kwa maneno mengine kutembea pamoja Naye. Na kwa nini unafanya hivi? “Ili [wewe] daima Roho wake apate kuwa pamoja [nawe]” (Mafundisho na Maagano 20:77; mkazo umeongezwa).
Sasa, tambua kwamba Bwana hakumwambia Henoko, “Simama hapa na utazama kuzunguka kote pamoja nami.” Hakusema, “Kaa chini na pumzika nami kwa muda.” Yeye alisema, “Tembea pamoja nami.” Lazima tuifanyie kazi misukumo ya kiroho tunayopokea. Lazima tufanye na kusema kile tunachoamini kuwa ni sahihi.
Kama Rais Marion G. Romney (1897–1988), mshauri katika Urais wa Kwanza, alivyoiweka, “Yeye anaweza tu kuongoza hatua zetu tunaposogeza miguu yetu.”
Lakini tambua kitu kingine ambacho Bwana hakusema. Yeye hakusema, “Kimbia pamoja nami.” Yeye hakusema, “Rukaruka pasipo jitihada yo yote juu ya vizuizi vyako vyote pamoja nami.” Yeye hatuombi sisi “kukimbia kasi zaidi ya nguvu [tulizo nazo]” (Mosia 4:27). Yeye hatarajii sisi tusonge mbele daima kwa kasi ya juu. Yeye hatarajii sisi tusifanye makosa au kukata tamaa. Yeye anataka tu tuendelee.
Pamoja
Tunatembea pamoja na Mwokozi. Siyo mbele Yake. Hakika si mbali Naye!
Unapotembea na mtu fulani, unatembea karibu nao. Lakini katika sitiari hii, tunabakia nyuma kidogo ya Mwokozi. Yeye anaongoza, na tunafuata—kwa karibu.
Unapokuwa katika njia sahihi, njia “haiongozi” kwa Yesu—Yeye yuko kwenye njia hiyo pia! Kumbuka sakramenti! Bwana, kupitia Roho Wake, daima atakuwa pamoja nawe, ilimradi unaendelea kumwalika Yeye.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo hawajali sana kuhusu wapi ulipo kwenye njia hiyo kama Wao wanavyojali ni mwelekeo gani unaoukabili. Watakutana nawe po pote ulipo. Haijalishi unatembea pole pole kiasi gani, aidha.
Mimi
Tunahitaji kuchukua hatua (TEMBEA). Tunahitaji kufanya hivyo kulingana na amri za Mungu na ushawishi wa Roho (PAMOJA). Na tunahitaji kufanya yote haya bila mtu ye yote bali Yesu Kristo (MIMI).
(Kwa vile Yesu Kristo, Baba Yake wa Mbinguni, na Roho Mtakatifu wana umoja katika kusudi—ona Yohana 10:30; 17:21; Mafundisho na Maagano 35:2—ni sahihi kusema kwamba wewe,“ unatembea pamoja na Mungu,” “unatembea pamoja na Mwokozi,” “unatembea pamoja na Roho,” au kitu cho chote cha asili hiyo.)
Kuna sauti nyingi za kuzifuata katika ulimwengu huu. Hakuna uhaba wa washawishi, watu mashuhuri, na wanasiasa ambao wangependa wewe “utembee” pamoja nao (au angalao kuwapa pesa). Kile wengine wanasema kinaweza kuwa cha manufaa, lakini kama tu kinaendana na mafundisho ya Mwokozi.
Tembea pamoja Naye.