Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Unganika
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Januari 2026


Unganika

Anavai H.

17, Tahiti, French Polynesia

msichana

Picha na Stéphane Sayeb

Wazazi wangu walitalakiana, na ilikuwa ni tukio la kuvunja moyo ambalo liliathiri moyo wangu mchanga. Ilikuwa vigumu sana kwangu kwa sababu sikutaka wao waachane, lakini nilipata faraja niliyohitaji katika Kristo. Kweli kilikuwa kipawa cha kiroho!

Wakati wa nyakati hizo ngumu, nilipata nguvu katika maneno ya Kristo. Masomo niliyopokea kutoka kwa wazazi wangu na viongozi yalinisaidia kubaki nimefokasi kwenye mafundisho Yake. Injili ikawa ngome ambayo kwayo ningeweza kuchota nguvu—nguvu iliyohitajika kushikilia imani yangu licha ya dhoruba za familia.

Leo, ninaendelea kupata shangwe kupitia injili na kupitia uzoefu wa hekaluni. Ninataka kujifunza zaidi kuhusu Kristo. Ninataka kumjua Yeye vyema zaidi na, juu ya yote, kufuata nyayo Zake. Ninao ushuhuda kwamba Kristo huongoza njia zetu na kwamba Yeye atatusaidia kubaki tumejikita Kwake, licha ya majaribu.