2025
Kujichukulia Jina la Yesu Kristo
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Novemba 2025


Kikao cha Jumapili Mchana

Kujichukulia Jina la Yesu Kristo

Dondoo

alt text

Nigeria

Pakua PDF

Tunaweza kuona angalau milingano mitano ya mchakato ambao kupitia huo tunajichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo. …

Mlingano wa Kwanza ni utambulisho. … Tunapojichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo, tunaunganisha jina letu pamoja na Lake. Tunajitambulisha Naye. …

Jambo linalohusiana kwa karibu na utambulisho ni mlingano mwingine—ukumbusho. … Kwetu sisi, kushiriki sakramenti kila wiki kunatusaidia kumkumbuka Yesu Kristo kwa wiki nzima. …

… Hata wakati tunapo jihusisha na mambo mengine, bado tunamkumbuka Yeye, kama tunavyokumbuka majina yetu wenyewe, bila kujali kingine chochote tunachokizingatia.

Ukuaji wa kukumbuka kile alichotufanyia Mwokozi ni mlingano wa tatu—kufuata mfano. … Kwetu sisi, kadiri tunavyojitambua na kumkumbuka Yesu Kristo, ndivyo tunavyotaka kuwa zaidi kama Yeye. …

Kumuiga Yesu Kristo kunatuongoza kwenye mlingano wa nne—mfungamano na madhumuni Yake. Tunaungana Naye katika kazi Yake. …

… Kutenda mambo haya manne kunatuongoza kwenye mlingano wa tano—uwezeshaji. Tunafikia nguvu na baraka za Mungu katika maisha yetu. …

Tunapofanya maagano ya ziada na Mungu, tunajichukulia juu yetu wenyewe kwa ukamilifu zaidi jina la Yesu Kristo. Kama matokeo yake, Mungu anatubariki zaidi kwa nguvu Zake. …

… Njooni kwa Baba Yetu wa Mbinguni. Jichukulie juu yako jina la Yesu Kristo. … Utakuwa mrithi aliyetukuka katika ufalme wa Baba yetu Mbinguni, mshirika wa urithi pamoja na Mzaliwa Wake wa Kwanza, Mwokozi wetu mpendwa na Mkombozi.