Kikao cha Jumapili Asubuhi
Manabii wa Mungu
Dondoo
Ghana
Bwana alishuhudia kwa mwanamke wa Shunemu kwamba Elisha alikuwa nabii wa Mungu, na alitenda kwa kuifungua nyumba yake ili kumpokea.
Sisi pia tunaweza kupokea ushuhuda binafsi wa manabii wa Mungu leo na kuifungua mioyo yetu na akili zetu—nyumba yetu—kwa ujumbe ambao Baba yetu wa Mbinguni anao kwa ajili yetu katika siku hizi za mwisho. …
Nabii ni nani? Nabii ni mtu ambaye Mungu amemwita azungumze kwa niaba Yake. …
Manabii ni waonaji na wafunuzi. Hiyo humaanisha wanaweza kuona kile wengine wasichoweza kukiona, na wanaweza kutoa unabii wa matukio yajayo. … Manabii hupokea amri na mafunuo kutoka kwa Bwana. …
Manabii pia huitangaza injili na ni walimu wenye uvuvio na wajumbe wa Mungu kwa kila mmoja duniani. …
Manabii wanashuhudia kumhusu Kristo—uwepo Wake, huduma Yake, na utakatifu Wake. …
Mwanamke Mshunami ametufunza kwamba tunaweza kuwa na ushuhuda huo kupitia Roho Mtakatifu. Ninawaahidi kwamba pale tunapojua kwamba wao ni wapakwa mafuta wa Mungu, maisha yetu yatakuwa rahisi licha ya changamoto zinazoendelea, kwani tutatii sauti yao kwa ujasiri, imani, na tumaini. Kuisikiliza na kuitii sauti ya nabii ni muhimu kwenye kushikilia kila kitu kizuri hadi Ujio wa Pili wa Mwokozi wetu. …
Nina shukrani kwa mwongozo na juhudi zilizowekwa wakfu za manabii walio hai. … Daima itakuwa kwamba Bwana anawachagua watumishi Wake.