2025
Kushangiliana
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Novemba 2025


Kikao cha Jumamosi Jioni

Kushangiliana

Dondoo

alt text

Ikwedo

New Zealand

Pakua PDF

Sote tunahitajiana. Nguvu ya kiungu hutokana na umoja, na ndiyo maana Shetani ana nia ya kututenganisha.

Kwa bahati mbaya, kwa baadhi yetu, kuhudhuria kanisani nyakati zingine inaweza kuwa jambo gumu kwa sababu kadha wa kadha. …

Uzoefu wetu kanisani umekusudiwa kutoa miunganiko muhimu na Bwana na kila mmoja wetu ambayo inahitajika sana kwa ajili ya ustawi wetu kiroho na kihisia. …

Upendo kama wa Kristo na kujaliana ni mambo ya juu zaidi na matakatifu. …

… Sisi sote ni sehemu ya familia ya Mungu, na Yeye anawapenda watoto Wake wote. Yeye anatamani kwamba watoto Wake wampende Yeye na pia wapendane.

Maisha ya Mwokozi yalikuwa mfano wa kupenda, kukusanya, na kuinua hata wale ambao jamii iliwahukumu kama waliokataliwa na wachafu. Mfano Wake ndiyo tulioamriwa kuufuata. …

Kutakuwa na nyakati katika maisha ya kila mmoja wetu ambapo tutakuwa watu tunaohitaji usaidizi na kutiwa moyo. Hebu tuweke ahadi sasa ya daima kufanya hivyo kwa kila mmoja. …

Kwa kila mmoja wenu anayeweza kuhisi amebaki nyuma katika mbio hizi za maisha, safari hii ya duniani, tafadhali endelea kusonga mbele. Ni Mwokozi pekee anayeweza kuhukumu ni wapi unapaswa kuwa katika wakati huu, na Yeye ni mwenye huruma na mwenye haki. …

Weka macho yako kwa Mwokozi. Yeye ni fimbo yako ya chuma. Usimwache Yeye. Ninashuhudia kwamba Yeye yu hai na wewe unaweza kumtumaini Yeye. Ninashuhudia pia kwamba Yeye anakushangilia.