Kikao cha Jumamosi Jioni
Dhabihu ya Upendo ya Yesu Kristo
Dondoo
Talitha Cumi, na Eva Timothy
Kama umetenda dhambi nzito na uko katika mchakato wa kutubu au una hamu ya kutubu kikamilifu na kuhisi furaha isiyoelezeka ya msamaha, tafadhali jua kwamba muujiza huu unakusubiri. …
Kugeuka kutoka kwenye dhambi, kumgeukia Mungu, na kuimarisha imani yako katika Yesu Kristo ni mwanzo mzuri. Kuwasilisha mapenzi yako kwa unyenyekevu kwa Mungu hujumuisha kuisema dhambi nzito kwa askofu wako au rais wa tawi, lakini msamaha wako kamili unatoka kwa Mwokozi. …
Hamu ya kweli ya kurudi kwa Mungu inaambatana na azimio la kuwa mwaminifu kabisa kwa Baba yako wa Mbinguni, kwako mwenyewe, kwa wale waliodhuriwa, na kwa kiongozi wako wa ukuhani. …
Hamu yako inakuongoza kutaka kurekebisha kile ulichovunja. Hata hivyo, ukitambua baadhi ya mambo yako nje ya uwezo wako wa kurekebisha, unaomba kwa dhati kwamba Bwana, kupitia neema Yake, atasaidia kuwaponya wale ambao wameumizwa katika matokeo ya matendo yako. …
Unapotafuta msamaha wa Bwana, kuwa mvumilivu pale unaposubiria idhini Yake kamili. …
Kwenu ninyi ambao mmejeruhiwa vibaya na dhambi nzito za mtu mwingine, ninatamani kushiriki upendo na huruma ya Mwokozi, faraja na amani Yake.
… Ninawapa uhakikisho wangu wa dhati kwamba Mwokozi anakujua na anakupenda. Mfikie Yeye. Yeye ndiye faraja na nguvu yako; Atawatuma malaika Zake kukubeba juu.