Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Utangulizi
Dondoo
Kituo cha Mikutano, Marekani
Wapendwa kaka zangu na dada zangu, tunakutana tunapoomboleza kifo cha Rais wetu mpendwa Russell M. Nelson. Ninazungumza nanyi kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, nafasi ambayo tayari nimekubaliwa katika kila moja ya kata zetu, kigingi, na mikutano mikuu kwa miaka saba na nusu iliyopita.
Tunasonga mbele na mkutano huu mkuu wa nusu mwaka, tukiendelea kama ilivyopangwa na pamoja na wasemaji na muziki uliopangwa na Rais Nelson baada ya miezi mingi ya maandalizi. …
… Rais Nelson alielewa thamani ya mkutano mkuu ili kutoa mwelekeo kwa Watakatifu katika miezi inayokuja. Tunatoa heshima kwake kwa kufuata ratiba ya mkutano iliyopangwa ambayo yeye aliidhinisha. …
Heshima yangu mwenyewe fupi—inayofaa kwenye mkutano huu na kwenye heshima ambazo tayari tumeshatoa—ni hii: Nilimpenda Russell M. Nelson na nimejifunza zaidi kuhusu injili na uongozi kwenye injili kutokana na urafiki wangu wa muda mrefu na uhusiano naye kuliko kutoka kwa kiongozi mwingine yeyote ambaye mimi binafsi nilimjua. Yeye ni mfano wetu wa kuigwa kama mtumishi na mfuasi wa Bwana Yesu Kristo.