Kikao cha Jumapili Asubuhi
Mtegemee Mungu na Uishi
Dondoo
California
Bolivia
Kituo cha Mikutano, Marekani
Madagaska
Bila shaka, ushauri huu “mtegemee Mungu na uishi” una maana kwetu siyo tu katika umilele lakini pia huleta tofauti yote katika sifa na ubora wa maisha yetu ya duniani.
Hakuna ahadi iliyorudiwa kila mara katika maandiko ya Kitabu cha Mormoni kuliko hii: “Kadiri mtakavyozishika amri zangu mtafanikiwa nchini; lakini kadiri msivyozishika amri zangu mtakatiliwa mbali na uwepo wangu.” … “Kufanikiwa” kulimaanisha kufurahia mwongozo na baraka za mbinguni katika maisha yao. … “Kufanikiwa” kulijumuisha uwezo wa kuinuka kushinda magumu na majaribu. …
… Amri za Mungu na ushauri hupatikana katika maandiko na maneno ya watumishi Wake. Kanuni na mawazo bora yaliyoelezwa katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” ni mfano mkuu. Mwingine ni mwongozo unaopatikana katika kijitabu cha Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana. …
Inaonekana hakuna mwisho wa vyanzo tofauti tofauti watu wanavyotegemea kwa ajili ya maana, furaha, na msaada. Wengi “wanangalia zaidi ya lengo.” … Katika kumtegemea Mungu, tunaweza kupata amani katika shida, na imani yetu inaweza kuendelea kukua hata katika nyakati za shaka na changamoto za kiroho. Tunaweza kupata nguvu katika kukabiliana na upinzani na kutengwa. Tunaweza kupatanisha ukamilifu na uhalisi wa sasa. …
Kumtegemea Mungu humaanisha kwamba Yeye sio tu mojawapo ya vipaumbele; inamaanisha, hakika, kwamba Yeye ndiyo kipaumbele chetu cha juu zaidi.