Kikao cha Jumapili Asubuhi
Kupambwa kwa Maadili ya Kuwa na Kiasi
Dondoo
Estonia
Chile
Bwana alitamka: …
“Na hakuna yeyote awezaye kusaidia katika kazi hii isipokuwa yule aliye mnyenyekevu na aliyejaa upendo, akiwa na imani, matumaini na hisani, akiwa na kiasi katika mambo yote, yatakayoaminiwa katika utunzaji wake.”
Mwongozo wa mwokozi, uliorekodiwa katika ufunuo huu mtakatifu, unatukumbusha kwamba kuwa na kiasi ni uimarishaji muhimu kwa ajili ya msingi imara katika Yesu Kristo.
Miongoni mwa sifa ambazo zinapamba ufuasi wa kweli wa Kristo, kuwa na kiasi kunajitokeza kama taswira ya Mwokozi Mwenyewe, tunda la thamani la Roho, linalo patikana kwa wote wanaojiweka kwenye ushawishi wa kiungu.
Wafuasi wa Kristo wanaojitahidi kuendeleza sifa hii Kama ya Kristo wanakuwa kwa asili kubwa wanyenyekevu na waliojaa upendo.
… Injili ya Yesu Kristo inatualika kutumia maadili haya hususani katika nyakati za changamoto, kwani ni katika fursa hizi hasa kwamba tabia ya kweli ya watu inadhihirishwa.
Huduma ya Mwokozi duniani ilidhihirika kwa maadili ya kuwa na kiasi katika vipengele vyote vya tabia Yake. …
Yesu Kristo, mkuu wa vyote, aliteseka kwa ajili yetu mpaka alitokwa damu kutoka kila kinyweleo, hata hivyo kamwe hakuruhusu hasira iwake moyoni Mwake, wala maneno ya shari, maneno ya kuchukiza, au maneno ya kukufuru yatoke kwenye mdomo wake, hata katika mateso kama hayo.
… Tunapojitahidi kwa imani na bidii kufuma kuwa na kiasi katika matendo na maneno, ninashuhudia kwamba tutaimarisha na kuweka nanga maisha yetu kwa usalama zaidi juu ya msingi thabiti wa Mkombozi wetu.