Mkutano Mkuu
Kupambwa kwa Maadili ya Kuwa na Kiasi
Mkutano mkuu wa Oktoba 2025


15:8

Kupambwa kwa Maadili ya Kuwa na Kiasi

Ninatoa mwaliko kwetu sote wa kuyapamba mawazo yetu kwa maadili kama ya Kristo wa kuwa na kiasi.

Mnamo mwezi Mei 2021, Wakati wa kutembelea kazi ya ukarabati wa hekalu la Salt Lake, Rais Russell M. Nelson alishangazwa na juhudi za waasisi ambao, pamoja na ufinyu wa rasilimali na imani isiyotetereka, walijenga jumba lile takatifu, kazi bora kimwili na kiroho ambayo imesimama imara kwa muda mrefu. Hata hivyo, pia alichunguza matokeo ya mmomonyoko, ambao kwa muda mrefu umesababisha nyufa katika mawe ya msingi wa kwanza wa hekalu na kutokuwa thabiti kwenye uashi, ishara za wazi kwa uhitaji wa uimarishaji wa jengo.

Rais Nelson nje ya Hekalu la Salt Lake

Nabii wetu mpendwa kisha alitufundisha kwamba jinsi ambavyo ilikuwa muhimu kutekeleza viwango vikubwa kuimarisha msingi wa hekalu ili kwamba liweze kuhimili nguvu za asili, sisi pia tunahitaji kuchukuwa hatua zisizo za kawaida—pengine hatua ambazo kamwe hatukuzichuwa hapo mwanzo—kuimarisha msingi wetu wa kiroho katika Yesu Kristo. Katika ujumbe wake wa kukumbukwa, alituacha na maswali mawili mazito kwa ajili ya kufikiria binafsi: “Jinsi gani ulivyo imara msingi wako? Na ni uimara gani unahitajika kwenye ushuhuda na uelewa wako wa injili?”

Injili ya Yesu Kristo inatupa sisi njia takatifu na na zenye uvuvio ili kuzuia mmomonyoko wa kiroho katika nafsi zetu, kwa nguvu ikiimarisha msingi wetu na kutusaidia kuepuka mianya katika imani yetu na udhaifu katika vyote, ushuhuda wetu na uelewa wetu wa kweli takatifu za injili. Kanuni moja ya kipekee inayohusika kwa ajili ya kutimiza azma hii inapatikana katika sehemu ya 12 ya mafundisho na Maagano, ufunuo uliotolewa kupitia Nabii Joseph Smith kwa Joseph Knight, mtu mwenye haki ambaye kwa uaminifu alitafuta kuelewa mapenzi ya Bwana, sio tu kwa badiliko la kuonekana kwa nje, lakini kusimama bila kuyumba katika ufuasi wake—imara kama nguzo za mbinguni. Bwana alitangaza:

“Tazama, ninasema nawe, na pia kwa wale wote walio na hamu ya kuanzisha na kuendeleza kazi hii;

“Na hakuna yeyote awezaye kusaidia katika kazi hii isipokuwa yule aliye mnyenyekevu na aliyejaa upendo, akiwa na imani, matumaini na hisani, akiwa na kiasi katika mambo yote, yatakayoaminiwa katika utunzaji wake.”

Mwongozo wa mwokozi, ulio rekodiwa katika ufunuo huu mtakatifu, unatukumbusha kwamba kuwa na kiasi ni uimarishaji muhimu kwa ajili ya msingi imara katika Yesu Kristo. Ni moja ya maadili yasiyo zuilika, sio tu kwa wale walioitwa kuhudumu lakini kwa ajili ya wote walio fanya maagano matakatifu na Bwana na kukubali kumfuata Yeye kwa imani. Kuwa na kiasi kunapatanisha na kunaimarisha sifa zingine kama za Kristo zilizotajwa katika ufunuo huu: unyenyekevu, imani, tumaini, hisani, na upendo wa kweli ambao unatiririka kutoka Kwake. Zaidi ya hayo, kuendeleza kuwa na kiasi ni njia sahihi ya kulinda nafsi zetu dhidi ya mmomonyoko wa kiroho ambao bado siku zote ni mgumu kuelezea ulio sababishwa na ushawishi wa kiulimwengu ambao unaweza kudhoofisha msingi wetu katika Yesu Kristo.

Miongoni mwa sifa ambazo zinapamba ufuasi wa kweli wa Kristo, kuwa na kiasi kunajitokeza kama taswira ya Mwokozi Mwenyewe, tunda la thamani la Roho, linalo patikana kwa wote wanao jifungua wenyewe kwa ushawishi mtakatifu. Ni maadili ambayo yanaleta upatanishi kwenye moyo, kutengeneza matamanio na hisia kwa busara na utulivu. Katika maandiko, kuwa na kiasi kunawakilishwa kama sehemu muhimu ya maendeleo katika safari yetu ya kiroho, kukituongoza kuelekea subira, uungu, na huruma wakati ikisafisha hisia zetu, maneno yetu, na matendo yetu.

Wafuasi wa Kristo wanao jitahidi kuendeleza sifa hii Kama ya Kristo wanakuwa kwa asili kubwa wanyenyekevu na waliojaa upendo. Nguvu tulivu inainuka ndani yao, na wanakuwa wenye uwezo mzuri wa kuzuia hasira, kutunza subira, na kuwatendea wengine kwa uvumilivu, heshima, na hadhi ya utu, hata wakati upepo wa shida ukivuma kwa nguvu kubwa. Wanajitahidi kutokutenda kwa wazo lolote la ghafla bali kuchagua kutenda kwa busara ya kiroho, ikiongozwa na unyenyekevu na kwa ushawishi wa upole wa Roho Mtakatifu. Kwa njia hii, wanaathirika kidogo kwa mmomonyoko wa kiroho kwa sababu, kama Mtume Paulo alivyofundisha, wanajuwa kwamba wanaweza kufanya mambo yote katika Kristo, awatiaye nguvu hata katika uso wa majaribu ambayo yangeweza kutikisa ushuhuda wao Kwake.

Katika Waraka wake kwa Tito, Paulo aliwasilisha ushauri mtakatifu kuhusu sifa za wale wanao tamani kumwakilisha Mwokozi na kufanya mapenzi Yake kwa imani na kujitolea kwa dhati. Alisema wanapaswa kuwa wakarimu, wenye busara, na watakatifu—sifa ambazo kwa uwazi zina akisi ushawishi wa kuwa na kiasi.

Hata hivyo, Paulo alionya kwamba wanapaswa kuwa “wasio wakaidi, wasio wepesi wa hasira, … [na] wasio wagomvi.” Tabia kama hizo ni kinyume na mawazo ya Mwokozi na zinazuia ukuaji wa kweli wa kiroho. Katika muktadha wa kimaandiko, “kutokuwa mkaidi” ni mtu anayekataa kutenda kwa kiburi na majivuno; “kutokuwa mwepesi wa hasira” ni mtu anayeepuka shurutisho la asili la kutokuwa na uvumilivu na kukwazika ; na “kutokuwa mgomvi” inahusu yule anaye kataa mabishano, jeuri, na tabia ya kikatili kwa maneno, kimwili na kihisia. Tunapojitahidi kubadili tabia yetu kwa imani na unyenyekevu, tunaweza kuwa tumefungwa imara kwenye mwamba imara wa rehema Yake na kuwa safi na vifaa vilivyo safishwa katika mikono Yake mitakatifu.

Hana na Samweli

Katika kutafakari juu ya haja ya kujenga maadili ya kuwa na kiasi, Nina kumbushwa juu ya maneno ya Hana, mama wa nabii Samweli—mwanamke wa imani ya ajabu ambaye, hata baada ya majaribu makubwa, aliimba wimbo wa shukrani kwa Bwana. Alisema, “Usiseme zaidi kwa kiburi mno; usiache ufidhuli utoke nje ya mdomo wako: kwani Bwana ni Mungu wa elimu, na kwa matendo yake yame pimwa.” Wimbo wake ni zaidi ya sala—ni mwaliko wa kujialika kutenda kwa unyenyekevu, kujidhibiti, na wastani. Hana anatukumbusha kwamba nguvu ya kweli ya kiroho haioneshwi katika msukumo wa vitendo au maneno ya majivuno bali katika kuwa na kiasi, fikra za kimawazo zilizolinganishwa na hekima za Bwana.

Mara nyingi, ulimwengu hukuza tabia zilizozaliwa na ushari, ufidhuli, kukosa uvumilivu, na kutokuwa na kiasi, mara nyingi ukitetea tabia kama hizo kwa misukumo ya maisha ya kila siku na mwelekeo kuelekea uthibitishaji na urahisishaji. Tunapo geuza mtazamo wetu mbali kutoka maadili ya kuwa na kiasi na kutojali uungwana wa kuwa na kiasi na ushawishi wa Roho Mtakatifu katika njia yetu ya kutenda na kuzungumza, tunaanguka kirahisi kwenye mtego wa adui, ambao bila kutatarajia unatuongoza kutoa maneno na kuchukuwa mitazamo itakayo tuletea masikitiko makubwa ama katika jamii, familia au hata mahusiano yetu ya kikanisa. Injili ya Yesu Kristo inatualika kutumia maadili haya hususani katika nyakati za changamoto, kwani ni katika fursa hizi hasa kwamba tabia ya kweli ya watu inadhihirishwa. Kama Martin Luther King Jr. wakati fulani alivyosema, “Kipimo cha mtu sio pale anaposimama katika nyakati za faraja na za kufaa, bali pale anaposimama nyakati za changamoto na za kutatanisha.”

Kama watu wa ahadi, tumeitwa kuishi mioyo yetu ikiwa na mizizi imara katika ahadi takatifu tulizo zifanya kwa Bwana, kwa uangalifu tukifuata mpangilio alio uanzisha kupitia mfano Wake mtimilifu Kama malipo, Ameahidi, “Amin, amin, nawaambia, kwamba haya ni mafundisho yangu, na yeyote atakayejenga juu yake hujenga juu ya mwamba wangu, na milango ya jehanamu haitamshinda.”

Mwokozi

Msifadhaike Mioyoni Mwenu, na Howard Lyon, kwa heshima ya Heavenlight

Huduma ya Mwokozi duniani ilidhihirika kwa maadili ya kuwa na kiasi katika vipengele vyote vya tabia Yake. Kupitia mfano wake mkamilifu, alitufundisha “uwe mvumilivu wakati wa mateso, usiwashutumu wenye kukushutumu.” Alipokuwa anafundisha kwamba hatupaswi kuruhusu hasira kwa sababu ya mapingamizi na mabishano, Alitangaza: “Lazima mtubu, na kuwa kama watoto wadogo.” Pia Alifundisha kwamba wote wanaotamani kuja Kwake kwa moyo wa lengo moja lazima wapatane na wale ambao wanawakasirikia au na wale walio na kinyongo nao. Kwa tabia ya kuwa na kiasi na moyo wa huruma, alituhakikishia kwamba tunapotendewa kikatili, bila huruma, kwa ufidhuli, au kwa dharau, upole wake hautatuacha, na maagano ya amani yake hayataondolewa kutoka kwenye maisha yetu.

Miaka michache iliyopita, mimi na mke wangu tulipata fadhila takatifu ya kukutana na baadhi ya waumini waaminifu wa kanisa katika Jiji la Mexico. Wengi wao, ama binafsi au kupitia wapendwa wao, walikuwa wamevumilia majaribu yasiyo elezeka, ikiwa ni pamoja na utekaji, mauaji, na misiba mingine ya kuvunja moyo.

Tulipotazama ndani ya nyuso za Watakatifu wale, hatukuona hasira, uchungu, au nia kwa ajili ya kisasi. Badala yake, tuliona unyenyekevu wa kimya. Mwonekano wa sura zao, ingawa zilionesha ishara ya huzuni, zilitoa tamanio angavu la uponyaji na faraja. Ingawa mioyo yao ilikuwa imevunjika kwa mateso, Watakatifu hawa walisonga mbele kwa imani katika Yesu Kristo, wakichagua kutoacha mateso yao kuwa mianya katika imani yao au kusababisha kutokuwa thabiti katika ushuhuda wao wa injili.

Mwishoni mwa mkusanyiko ule mtakatifu, tulisalimiana na kila mmoja wao. Kila salamu ya kushikana mikono, kila kumbatio, likawa ushuhuda wa kimya kwamba kwa msaada wa Bwana, tunaweza kuchagua kujibu kwa kuwa na kiasi kwenye kuvunjika moyo na changamoto za maisha. Ukimya wao na mfano wao wa kutojitanguliza ulikuwa kama mwaliko kutembea njia ya Mwokozi kwa kuwa na kiasi katika vitu vyote. Tulijihisi kama tulikuwa katika uwepo wa malaika.

Yesu Kristo, mkuu wa vyote, aliteseka kwa ajili yetu mpaka alitokwa damu kutoka kila kinyweleo, hata hivyo kamwe hakuruhusu hasira iwake moyoni Mwake, wala maneno ya shari, maneno ya kuchukiza, au maneno ya kukufuru yatoke kwenye mdomo wake, hata katika mateso kama hayo. Pamoja na kuwa na kiasi kikamilifu na unyenyekevu usio na kifani, Hakujifikiria bali juu ya kila mmoja wa watoto wa Mungu—waliopita, waliopo, na wa baadae. Mtume Paulo alishuhudia juu ya tabia ya unyenyekevu ya Kristo wakati alipotangaza: “Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.” Hata katikati ya mateso yake makubwa, Mwokozi alionesha kuwa na kiasi kuliko kamili na kwa kiungu. Alitangaza,“Hata hivyo, utukufu na uwe kwa Baba, na Mimi nikachukua na kukamilisha maandalizi yangu kwa ajili ya watoto wa wanadamu.”

Akina kaka na dada zangu wapendwa, Ninatoa mwaliko wa kweli kwetu sote kupamba akili zetu na mioyo yetu kwa maadili kama ya Kristo ya kuwa na kiasi, kama jibu takatifu kwa wito wa kinabii wa mpendwa Rais wetu Russell M. Nelson. Tunapo jitahidi kwa imani na bidii kufuma kuwa na kiasi katika matendo na maneno, ninashuhudia kwamba tutaimarisha na kuweka nanga maisha yetu kwa usalama zaidi juu ya msingi hakika wa Mkombozi wetu.

Kwa dhati natoa ushuhuda wangu kwamba utafutaji wa daima wa kuwa na kiasi unasafisha nafsi yetu na kutakasa moyo wetu mbele ya Mwokozi, taratibu ukitusogeza zaidi Kwake na kututayarisha, kwa tumaini na amani, kwa ajili ya siku ile ya utukufu tutakapo kutana na Yeye kwenye Ujio Wake wa Pili. Nina shiriki maneno haya matakatifu katika jina takatifu la Mwokozi wetu, Yesu Kristo, amina.