Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu
Mkutano mkuu wa Oktoba 2025


3:26

Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu

Akina kaka na akina dada, sasa nitawawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kukubali kwako katika njia ya kawaida. Kama kuna wanaopinga mapendekezo yoyote, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin Harris Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Wale wanaokubali, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Dallin H. Oaks, Jeffrey R. Holland, Henry B. Eyring, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, Ulisses Soares na Patrick Kearon.

Wale wanaokubali, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wote wanaokubali, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna ye yote, kwa ishara hiyo hiyo.

Tunatambua kwamba Sabini wa Maeneo wapya wawili walikubaliwa wakati wa mikutano ya uongozi ya mkutano mkuu na kutangazwa kwenye tovuti ya Kanisa. Tunawaalikeni muwakubali ndugu hawa katika majukumu yao mapya.

Wale wanaokubali, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.

Wale wanaokubali, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Tunawashukuru, akina kaka na akina dada, kwa kura yenu ya kuwakubali kwa niaba ya uongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Maeneo

Sabini wa Maeneo wafuatao walikubaliwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Bhanu K. Hiranandani na Fernando Vivas.