Mkutano Mkuu
Hakuna Anayeketi Peke Yake
Mkutano mkuu wa Oktoba 2025


14:3

Hakuna Anayeketi Peke Yake

Kuishi injili ya Yesu Kristo kunajumuisha kutoa nafasi kwa wote katika Kanisa Lake lililorejeshwa.

I.

Kwa miaka 50, nimejifunza utamaduni, ikijumuisha utamaduni wa injili. Nilianza na biskuti za bahati.

Huko Chinatown ya San Francisco, chakula cha jioni cha familia ya Gong kilihitimishwa kwa biskuti ya bahati na msemo wa busara kama “Safari ya maili elfu huanza kwa hatua moja.”

Bahati katika biskuti ya bahati

Kama mtu mzima, nilitengeneza biskuti za bahati. Nikiwa nimevaa glavu nyeupe za pamba, nilikunja na kuweka katika umbo biskuti za duara zilizopikwa ndani ya jiko.

Kutengeneza biskuti za bahati
Kukunja biskuti ya bahati

Kwa mshangao wangu, nilijifunza biskuti za bahati sio sehemu ya utamaduni wa Kichina. Ili kutofautisha utamaduni wa biskuti za Kichina, Kimarekani na Ulaya, nilitafuta biskuti za bahati katika mabara mengi—kama vile mtu angetumia maeneo mengi kuwasha moto msituni. Mighahawa ya Kichina huko San Francisco, Los Angeles, na New York huandaa biskuti za bahati, lakini si zile za Beijing, London, au Sydney. Ni Wamarekani pekee wanaosherehekea Siku ya Kitaifa ya Biskuti ya Bahati. Matangazo ya Kichina pekee ndiyo hutoa “Biskuti Halisi za Bahati za Kimarekani.”

Biskuti za bahati ni mfano wa kufurahisha, rahisi. Lakini kanuni hiyo hiyo ya kulinganisha desturi katika mazingira tofauti ya kitamaduni inaweza kutusaidia kutofautisha utamaduni wa injili. Na sasa Bwana anafungua fursa mpya za kujifunza utamaduni wa injili kadiri fumbo la Kitabu cha Mormoni na unabii wa mafumbo wa Agano Jipya unavyotimizwa.

II.

Kila mahali watu wanahama. Umoja wa Mataifa unaripoti wahamiaji milioni 281 wa kimataifa. Hawa ni watu milioni 128 zaidi ya mwaka wa 1990, na zaidi ya mara tatu makadirio ya 1970. Kila mahali, idadi kubwa ya waongofu wanapata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kila Sabato, waumini na marafiki kutoka nchi na wilaya 195 za kuzaliwa ukusanyika katika mikusanyiko 31,916 ya Kanisa. Tunazungumza lugha 125.

Kukutana na Watakatifu katika Albania
Kukutana na Watakatifu katika Makedonia Kaskazini
Kukutana na Watakatifu katika Kosovo
Kukutana na Watakatifu katika Uswizi
Kukutana na Watakatifu katika Ujerumani
Kukutana na Watakatifu katika Ujerumani

Hivi majuzi, huko Albania, Makedonia Kaskazini, Kosovo, Uswizi, na Ujerumani nilishuhudia washiriki wapya wakitimiza fumbo la Kitabu cha Mormoni la mti wa mzeituni. Katika Yakobo 5, Bwana wa shamba la mizabibu na watumishi wake huimarisha mizizi na matawi ya mizeituni kwa kukusanya na kupandikiza ile kutoka sehemu mbalimbali. Leo, watoto wa Mungu hukusanyika kama wamoja katika Yesu Kristo, Bwana hutoa njia ya ajabu ya asili kupanua utimilifu wetu wa kuishi na ufahamu wa injili Yake iliyorejeshwa.

Yeye akituandaa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, Yesu anasimulia mifano ya karamu kuu na karamu ya harusi. Katika mifano hii, wageni waalikwa hutoa visingizio vya kutokuja. Bwana anaagiza watumishi wake ‘watoke upesi kwenye barabara na vichochoro vya jiji’ na “barabara kuu na viunga” ili ‘kuwaleta humu’ maskini, vilema, viwete, na vipofu. Kuzungumza kiroho, huyo ni kila mmoja wetu.

Maandiko yanasema:

“Mataifa yote yataalikwa” kwenye “karamu ya nyumba ya Bwana.”

“Itengenezeni njia ya Bwana, … ili ufalme wake upate kuenea juu ya dunia, ili wakazi wake wapate kuupokea, na kuwa tayari kwa siku zijazo.”

Leo wale walioalikwa kwenye karamu ya Bwana wanatoka kila mahali na tamaduni. Wazee kwa vijana, matajiri na maskini, wenyeji na wa kimataifa, tunafanya mikusanyiko yetu ya Kanisa ionekane kama jumuiya zetu.

Kama Mtume mkuu, Petro aliona mbingu ikifungua ono la “shuka kubwa iliyosokotwa katika pembe nne, … ambamo ndani yake mlikuwa na … wanyama wa kila namna.” Petro alifundisha: “Kwa kweli natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo. … Katika kila taifa mtu amchaye [Bwana] na kutenda haki hukubaliwa naye.”

Msamaria Mwema

Katika fumbo la Msamaria mwema, Yesu anatualika tuje kwa kila mmoja wetu pamoja na Kwake katika nyumba Yake ya wageni—Kanisa Lake. Yeye anatualika sisi kuwa majirani wema. Msamaria mwema anaahidi kurudi na kulipa uangalizi wa wale walio katika nyumba Yake ya wageni. Kuishi injili ya Yesu Kristo kunajumuisha kutoa nafasi kwa wote katika Kanisa Lake lililorejeshwa.

Roho ya “chumba katika nyumba ya wageni” inajumuisha “hakuna anayeketi peke yake.” Je, unapokuja kanisani, ukiona mtu yuko peke yake, tafadhali utamsalimia na kuketi naye? Huenda hii isiwe desturi yako. Mtu huyo anaweza kuonekana au kuzungumza tofauti na wewe. Na bila shaka, kama biskuti ya bahati inaweza kusema, “Safari ya urafiki wa injili na upendo huanza na salamu ya kwanza na hakuna mtu anayeketi peke yake.”

“Hakuna anayeketi peke yake” pia inamaanisha hakuna anayeketi peke yake kihisia au kiroho. Nilienda na baba aliyevunjika moyo kumtembelea mwanawe. Miaka mingi mapema, mwana huyo alifurahi kuwa shemasi mpya. Hafla hiyo ilijumuisha familia yake kumnunulia jozi yake ya kwanza ya viatu vipya.

Lakini kanisani, mashemasi walimcheka. Viatu vyake vilikuwa vipya, lakini si vya mtindo. Kwa aibu na kuumia, shemasi huyo mchanga alisema kamwe hangeenda tena kanisani. Moyo wangu bado umevunjika kwa ajili yake na familia yake.

Katika barabara za vumbi kuelekea Yeriko, kila mmoja wetu amechekwa, ameaibishwa na kuumizwa, labda amedharauliwa au kunyanyaswa. Na kwa viwango tofauti vya nia, kila mmoja wetu pia amepuuza, hajaona au kusikia, labda ameumiza wengine kimakusudi. Ni kwa sababu tumeumizwa na kuwaumiza wengine ndiyo maana Yesu Kristo anatuleta sisi sote kwenye nyumba Yake ya wageni. Katika Kanisa Lake na kupitia ibada na maagano Yake, sisi tunakuja kwa mmoja na mwingine na kwa Yesu Kristo. Tunapenda na kupendwa, kutumikia na kutumikiwa, kusamehe na kusamehewa. Tafadhali kumbuka, “dunia haina huzuni ambayo mbingu haiwezi kuponya”; mizigo ya dunia kuwa nyepesi—furaha ya Mwokozi wetu ni ya kweli.

Katika 1 Nefi 19, tunasoma: “Hata Mungu wa Israeli mwenyewe [wanamkanyagia] chini ya miguu yao; … wanamdharau. … Kwa hivyo wanampiga kwa mijeledi, na anavumilia; na wanamchapa, na anavumilia. Naam, wanamtemea mate, naye anavumilia.”

Rafiki yangu Profesa Terry Warner anasema kuhukumu, kupigwa mijeledi, kumpiga, na kutemewa mate havikuwa matukio ya hapa na pale ambayo yalitokea tu wakati wa maisha ya kibinadamu ya Kristo. Jinsi tunavyotendeana—hasa wenye njaa, wenye kiu, wale walioachwa peke yao, ndivyo tunavyomtendea Yeye.

Katika Kanisa Lake lililorejeshwa, sisi sote ni bora wakati hakuna anayeketi pekee yake. Tusikubaliane tu au tuvumilie tu. Tuwakaribishe kwa dhati, tuwatambue, tuwatumikie, tuwapende. Na kila rafiki, dada, kaka asiwe wa kutoka nchi za nje au mgeni bali mtoto nyumbani.

Mwanamke akiwa peke yake kanisani

Leo wengi huhisi upweke na kutengwa. Mitandao ya kijamii na akili mnemba inaweza kutuacha tukiwa tunatamani ukaribu wa binadamu na mguso wa kibinadamu. Tunataka kusikia sauti za kila mmoja wetu. Tunataka kuwa wa na wema wa kweli.

Kuketi pamoja na marafiki kanisani

Kuna sababu nyingi ambazo tunaweza kuhisi kwamba hatufai kuwa kanisani—kwamba, tukizungumza kwa njia ya kitamathali, tunaketi peke yetu. Tunaweza kuwa na wasiwasi juu ya lafudhi yetu, nguo, hali ya familia. Labda tunajiona kuwa hatutoshi, harufu ya moshi; tunatamani usafi wa maadili; tumeachana na mtu na kuhisi kuumizwa na wenye aibu, tuna wasiwasi kuhusu sera hii au ile ya Kanisa. Tunaweza kuwa waseja, tumetalikiana, wajane. Watoto wetu wana kelele; hatuna watoto. Hatukuhudumu misheni au tulirudi nyumbani mapema. Orodha inaendelea

Mosia 18:21 inatualika kufuma mioyo yetu pamoja katika upendo. Ninakualikeni sisi tupunguze wasiwasi, tusihukumu sana, tusitake mengi kutoka kwa wengine—na, inapohitajika, tusiwe wagumu juu yetu wenyewe. Hatuumbi Sayuni kwa siku moja. Lakini kila “salamu,” kila ishara ya urafiki, huileta Sayuni karibu zaidi. Hebu tumwamini Bwana zaidi na tuchague kwa shangwe kutii amri Zake zote.

III.

Kimafundisho, katika nyumba ya imani na ushirika wa Watakatifu, hakuna anayeketi peke yake kwa sababu ya agano la kuwa wa katika Yesu Kristo.

Alifundisha Nabii Joseph Smith: “Imesalia kwetu kuona, kushiriki na kusaidia kupeleka mbele utukufu wa Siku za Mwisho, ‘kipindi cha utimilifu wa nyakati … ,’ wakati Watakatifu wa Mungu watakapokusanywa mahali pamoja kutoka katika kila taifa, na kabila, na watu.”

Mungu “hafanyi lolote ila kwa manufaa ya ulimwengu; … ili awavute wanaume wote [na wanawake] kwake. …

“… Anawakaribisha wote kuja Kwake na kupokea wema Wake; … na wote ni sawa mbele ya Mungu.”

Uongofu katika Yesu Kristo unatuhitaji tumvue mtu wa asili na utamaduni wa kiulimwengu. Kama Rais Dallin H. Oaks anavyofundisha, tunapaswa kuacha utamaduni wa kimila na desturi yo yote ambayo ni kinyume na amri za Mungu na kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Anaeleza, “Kuna utamaduni wa kipekee wa injili, seti ya viwango na matarajio na desturi zinazofanana kwa waumini wote wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.” Utamaduni wa injili unajumuisha usafi wa kimwili, kuhudhuria kanisani kila wiki, kujiepusha na vileo, tumbaku, chai, na kahawa. Inajumuisha uaminifu na uadilifu, kuelewa tunasonga mbele sio juu au chini, katika nafasi za Kanisa.

Ninajifunza kutoka kwa waumini na marafiki waaminifu katika kila nchi na tamaduni. Maandiko yanapofunzwa katika lugha nyingi na mitazamo ya kitamaduni huongeza kina cha uelewa wa injili. Maonyesho tofauti ya sifa kama za Kristo huongeza kina cha upendo na ufahamu wangu juu ya Mwokozi wangu. Wote wanabarikiwa tunapofafanua utambulisho wetu wa kitamaduni, kama vile Rais Russell M. Nelson alivyofundisha, kama mtoto wa Mungu, mtoto wa agano, mwanafunzi wa Yesu Kristo.

Amani ya Yesu Kristo imekusudiwa kwetu sisi kibinafsi. Hivi majuzi, kijana mmoja aliuliza kwa dhati, “Mzee Gong, bado mimi ninaweza kwenda mbinguni?” Alijiuliza ikiwa angeweza kusamehewa. Nilimuuliza jina lake, nikasikiliza kwa makini, nikamwalika yeye kuzungumza na askofu wake, nikampa kumbatio kubwa. Aliondoka akiwa na matumaini katika Yesu Kristo.

Nilimtaja mvulana huyo katika mazingira mengine. Baadaye nilipokea barua ambayo haijatiwa sahihi ambayo ilianza, “Mzee Gong, mke wangu na mimi tumelea watoto tisa … na kuhudumu misheni mbili.” Lakini “Siku zote nilihisi singeruhusiwa katika ufalme wa selestia … kwa sababu dhambi zangu kama kijana zilikuwa mbaya sana!”

Barua iliendelea, “Mzee Gong, uliposimulia kuhusu kijana huyo kupata tumaini la msamaha, nilijawa na shangwe, nikianza kutambua kwamba yawezekana [ningeweza kusamehewa].” Barua hiyo inamalizia, “Hata ninajipenda mwenyewe sasa!”

Agano la kuwa wa linaongezeka kina tunapokuja kwa kila mmoja wetu na kwa Bwana katika nyumba Yake ya wageni. Bwana hutubariki sisi sote inapokuwa hakuna anayeketi peke yake. Na nani anayejua? Pengine mtu tunayeketi karibu naye anaweza kuwa rafiki yetu bora wa biskuti ya bahati. Na tutafute na kuweka nafasi kwa ajili yake Yeye na sisi kwa sisi kwenye karamu ya Mwana-Kondoo, ninasali kwa unyenyekevu katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona “Fortune Cookies Didn’t Come from China,” Royal Examiner, Dec 26, 2021, royalexaminer.com/fortune-cookies-didnt-come-from-china; “National Fortune Cookie Day,” Days of the Year, daysoftheyear.com/days/fortune-cookie-day.

  2. Mchakato wa utatuzi wa kitamaduni unaweza pia kusaidia kutofautisha kile kinachoweza kuchukuliwa kuwa utamaduni wa injili, utamaduni wa kitaifa wa mahali hapo, na utamaduni wa kisasa wa ulimwengu.

  3. International Organization for Migration, World Migration Report 2024, 21, publications.iom.int/books/world-migration-report-2024. “Katika mwaka 2022, kulikuwa na wakimbizi milioni 117 duniani, na wakimbizi milioni 71.2 wa ndani ya nchi” (World Migration Report 2024, xii).

  4. Ona Yakobo 5.

  5. Kila lugha na tamaduni zina maneno na istilahi zinazoelezea mambo ya moyoni. Utimilifu wetu wa maisha wa injili Yake iliyorejeshwa hupanuka tunapojifunza kutoka kwa kila mmoja wetu. Hivi majuzi Akina Dada Annalie (aliyetoka Munich) na Suzy Myers, Mzee Erich na Dada Christiane Kopischke, na Mzee Jörg na Dada Julia Klebingat walishiriki maneno ya kipekee ya Kijerumani ambayo yanasema na moyo. Hisia ambazo maneno haya yanaelezea huenda zaidi ya utaratibu wa juu. Zinaenda zaidi ya utaratibu au wajibu. Hisia hizi zinazungumza juu ya moyo; uhusiano wa ukunjufu na wa karibu, ya furaha ya kiroho katika nafsi zetu za kiuungu. Maneno haya maalum katika Kijerumani ni pamoja na Gemütlichkeit na gemütlich, Heimat, Heimweh, Geborgenheit, Zuflucht, Herzensangelegenheit, Herzensmensch, and Schummerstunde (neno adimu na la kishairi kutoka kaskazini).

  6. Luka 14:21, 23. Vivyo hivyo, katika mfano wa karamu ya harusi, wageni walioalikwa wasipokuja, mfalme aagiza watumishi wake waende kukusanya “wote [watakaopata]” katika “barabara kuu.” (Mathayo 22:9).

  7. Mafundisho na Maagano 58:9; ona pia Mafundisho na Maagano 58:6–8, 10–12.

  8. Mafundisho na Maagano 65:35; (ona pia Mafundisho na Maagano 33:17)

  9. Matendo 10:11–12, 34–35; ona pia Matendo 10:9–10, 13–18, 24–33, 44–48; 11:1–18; 15:6–11.

  10. Picha ya sisi kuja pamoja kwa sisi kwa sisi pamoja na Yeye katika nyumba yake ya wageni inaonyeshwa ndani 3 Nefi 18:32. “Hakuna mtu anayeketi peke yake” katika sehemu zetu za ibada, na kuendelea kwetu kuhudumiana kwa uchangamfu, kwa hakika kunaweza kuwa njia ambayo kwayo sisi na wao “kurudi na kutubu, na kumwendea [Yeye] kwa makusudi kamili ya moyo, naye [Yeye] atawaponya; na [sisi] tutakuwa njia ya kuwaletea wokovu.”

  11. Mafundisho na Maagano 104:15, 17 inatukumbusha, “Vitu vyote ni vya [Bwana]” na “dunia imejaa, na viko vya kutosha na vibaki.” Ipasavyo, maskini na tajiri ni kila mmoja kusaidia wote kuinuliwa na kuwa chini. Vile vile, Mfalme Benyamini anauliza, “Je, sisi sote si ombaomba?” Kwa hivyo matajiri na maskini kila mmoja anawajibika kwa hiari “kupeana mali mliyo nayo mmoja kwa mwingine” (Mosia 4:19, 21; ona pia Mosia 4:25–27).

  12. Katika “Come, Ye Disconsolate” (Hymns, no. 115), Thomas Moore anaandika: “Njooni kwenye kiti cha rehema, mpige magoti kwa bidii. Hapa leteni mioyo yenu iliyojeruhiwa; hapa semeni maumivu yenu. Dunia haina huzuni ambayo mbingu haiwezi kuponya.”

  13. 1 Nefi 19:7, 9. Katika Mahubiri ya Mlimani, Bwana anasema, “Na kwa yeye akupigaye juu ya shavu moja pia mpatie lingine; na akunyang’aye vazi lako usimkataze kuchukua koti lako pia” (Luka 6:29).

  14. Ona Mathayo 25:35–40.

  15. “Si mgeni tena, bali mtoto wa nyumbani” (“My Shepherd Will Supply My Need,” Hymns—For Home and Church, Gospel Library).

  16. Injili ya Yesu Kristo inapita muda na utamaduni. Ni ushuhuda wa ajabu kwangu kwamba Kitabu cha Mormoni kinafundisha utimilifu wa injili ya Yesu Kristo katika muktadha wa mazingira ya kitamaduni ya kale katika Amerika.

  17. Kama ilivyofundishwa na Nabii Joseph Smith na washauri wake katika Urais wa Kwanza katika Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 513; ona pia Waefeso 1:10.

    Leo waumini wa Kanisa wanaishi katika hali mbalimbali za kisiasa, kijamii, na kiuchumi. Kata na matawi yetu yanatofautiana kwa ukubwa na rasilimali za uongozi. Kanuni za “kufanana na kuzoea” zinaweza kusaidia kuimarisha familia na Kanisa Lake lililorejeshwa katika njia za injili popote tunapoishi (ona Handbook 2: Administering the Church [2010], 17.0).

  18. 2 Nefi 26:24, 33, msisitizo umeongezwa; ona pia 2 Nefi 29; Alma 29:8. Mafundisho na Maagano 90:11 kina ahidi “kwamba kila mtu atasikia utimilifu wa injili katika ulimi wake mwenyewe, na katika lugha yake mwenyewe.” Ahadi hii inatimizwa tunapoleta pamoja ndimi za lugha na lugha ya kitamaduni ya injili katika nyumba zetu na Kanisani.

  19. Ona Dallin H. Oaks, “Kutubu na Kubadilika,” Liahona, Nov. 2003, 37–40.

  20. Dallin H. Oaks, “Toba na Badiliko,” 39.

  21. Ona Dallin H. Oaks, “Toba na Badiliko,” 38–39.

  22. Ona Makala ya Imani 1:13. Matawi na mizizi mbalimbali inapofungamana kama moja katika Yesu Kristo, tunapata zaidi ambayo ni “wema wa maadili, wa kupendeza, au wenye sifa njema au wenye kusifiwa.” Tunawaona wa kwanza mwisho na wa mwisho kwanza. Tunafurahi wanafunzi wanapofundisha na walimu wanapojifunza. Wote wanaelewa, wanajengwa, na kufurahi pamoja (ona Mafundisho na Maagano 50:22).

  23. Ona Russell M. Nelson, “Choices for Eternity” (worldwide devotional for young adults, Monday, May 15, 2022), Gospel Library.

  24. Jedediah M. Grant, ambaye alihudumu katika Urais wa Kwanza pamoja na Brigham Young, aliripoti ono la ulimwengu wa roho ambalo lilijumuisha aina nyingi za maua mazuri yanayostawi pamoja, labda kama sitiari ya umoja na uzuri katika utofauti. “Nimeona bustani nzuri katika dunia hii lakini sijapata kuona yoyote ya kulinganisha na zile zilizokuwepo pale” alisema. “Niliona maua ya aina nyingi, na mengine yakiwa na maua kutoka hamsini hadi mia ya rangi mbalimbali yakiota kwenye bua moja.” Alipitia “uzuri na utukufu wa ulimwengu wa roho ambapo roho waadilifu wamekusanyika pamoja” (“Remarks, at the Funeral of President Jedediah M. Grant, by President Heber C. Kimball,” Deseret News, Dec. 10, 1856, 317).

    Rais David O. McKay pia alirekodi ndoto au ono la mji wa milele wa Mungu ambapo aliona miti, matunda, vichaka, na maua katika kuchanua kikamilifu. “Nilionekana kutambua kwamba miti yenye matunda yenye kupendeza, vichaka vilivyo na majani yenye rangi ya kuvutia, na maua yenye kuchanua vizuri vilienea kila mahali” (Teachings of Presidents of the Church: David O. McKay [2003], 1).