Mkutano Mkuu
Utangulizi
Mkutano mkuu wa Oktoba 2025


3:34

Utangulizi

Sasa tunasonga mbele na huu mkutano mkuu wa nusu mwaka, tukiendelea kama ilivyopangwa na tukiwa na wanenaji na muziki kama ilivyopangwa na Rais Nelson baada ya miezi ya maandalizi.

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, tunakutana tukiomboleza kifo cha mpendwa wetu Rais Russell M. Nelson. Ninazungumza nanyi kama Rais wa Akidi ya wale Kumi na Wawili, katika nafasi ambayo tayari kwayo nimekuwa nikiidhinishwa katika kila mkutano wa kata, kigingi, na mkutano mkuu kwa miaka saba na nusu iliyopita.

Tunasonga mbele na huu mkutano mkuu wa nusu mwaka, tukiendelea kama ilivyopangwa na tukiwa na wanenaji na muziki kama ilivyopangwa na Rais Nelson baada ya miezi ya maandalizi. Nyongeza tu ni, maelezo ya utangulizi wangu, na kuzungumza kwangu badala ya Rais Nelson katika kikao cha kufunga cha Jumapili mchana.

Hii ni mara ya kwanza katika karibia miaka 75 kwamba Rais wa Kanisa amefariki siku chache kabla ya mkutano mkuu. Hii imetubidi tupange jinsi tungefanya mikutano muhimu ya uongozi kuhusiana na mkutano mkuu vile vile vikao vya mkutano mkuu, wakati huo huo kuratibu mazishi yake punde iwezekanavyo. Rais Nelson alielewa thamani ya mkutano mkuu ya kutoa mwelekeo kwa Watakatifu katika miezi ijayo. Tunamheshimu kwa kufuata ratiba ya mkutano iliyopangwa aliyoidhinisha.

Katika huu wakati wa majonzi, tayari tumefanya mkutano wa kutoa heshima kwa Rais Russell M. Nelson kabla ya mikutano ya mkutano mkuu na kisha kuratibu mazishi punde iwezekanavyo baada ya mkutano mkuu. Haya yote yamefanywa kwa ruhusa ya familia ya Rais Nelson na Akidi ya Mitume kumi na Wawili.

Kwa vile kila mmoja wetu ambaye amepagiwa kuzungumza katika mkutano mkuu angependa kuchukua muda tuliopangiwa kutoa heshima binafsi kwa Rais Nelson, kwa hivyo tunawaomba wanenaji wetu wote wa mkutano mkuu kutoa heshima hizo kwa muda mfupi sana, wakiahirisha kutoa heshima fafanuzi hadi wakati wa mazishi, ambayo tayari tumeanza kupanga.

Heshima fupi zangu mwenyewe—zinazofaa kwa mkutano huu na heshima ambazo tayari tumetoa—ni hii: Ninampenda Russell M. Nelson na nimejifunza zaidi kuhusu injili na uongozi wa injili kutoka kwa urafiki wangu wa muda mrefu na ushirika naye kuliko kutoka kwa kiongozi mwingine yoyote ambaye nimemjua kibinafsi. Yeye ni mfano wetu kama mtumishi na mfuasi wa Bwana Yesu Kristo. Juu ya mambo haya ninashuhudia, katika jina la Yesu Kristo, amina.