Mkutano Mkuu
Familia-Kitovu cha Injili ya Yesu Kristo
Mkutano mkuu wa Oktoba 2025


17:23

Familia-Kitovu cha Injili ya Yesu Kristo

Mafundisho yetu na imani yetu katika familia za milele vinatuimarisha na kutuunganisha.

Wapendwa kaka na dada zangu, asanteni kwa sala zenu kwa niaba yangu. Nimezihisi.

I.

Mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho hujikita kwenye familia. Cha muhimu kwenye fundisho letu kuhusu familia ni Hekalu. Ibada zinazopokelewa humo hutuwezesha kurudi kama familia za milele kwenye uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni.

Mpaka mkutano mkuu wa April 2025, Rais Russell M. Nelson alikuwa amekwishatangaza ujenzi wa mahekalu mapya 200. Alipenda kutangaza mahekalu mapya kwenye hitimisho la kila mkutano mkuu, nasi tulifurahia pamoja naye. hatahivyo, kwa idadi kubwa ya mahekalu ambayo kwa sasa yapo kwenye hatua za awali sana za upangaji na ujenzi, ni vyema kwamba tupunguze utangazwaji wa mahekalu mapya. Hivyo, kwa idhini toka Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, hatutatangaza hekalu lolote jipya kwenye mkutano huu. Tutaendelea na utoaji wa ibada za hekaluni kwa waumini wa Kanisa kote ulimwenguni, ikijumuisha lini na wapi pa kutangaza ujenzi wa mahekalu mapya.

Sehemu ya ujumbe wangu ambao nimetoka kuutoa iliandikwa baada ya kifo cha Rais wetu mpendwa Russell M. Nelson. Sehemu ambayo sasa inafuatia iliandikwa na kuidhinishwa wiki kadhaa kabla, lakini bado inawakilisha mafundisho yangu, niliyopokea toka kwa Bwana.

II.

Tangazo la familia, lililotangazwa miaka 30 kamili iliyopita, linatamka kwamba “familia imeamriwa na Mungu” na “ni kitovu cha mpango wa Muumbaji kwa ajili ya hatima ya milele ya watoto Wake.” Pia linatamka “kwamba amri ya Mungu kwa watoto Wake ya kuongezeka na kuijaza dunia bado ina nguvu.” Na, “Tunatamka tena kwamba Mungu ameamuru kwamba nguvu takatifu za uumbaji zinapaswa kutumiwa tu kati ya mwanaume na mwanamke, waliooana kisheria kama mume na mke.” Kama–Mzee wakati huo Russell M. Nelson alivyo wafundisha hadhira ya BYU, kwamba familia ni “ya muhimu sana katika mpango wa Mungu. … Ukweli ni kwamba, dhumuni la mpango huu ni kuinuliwa kwa familia.”

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linajulikana vyema kama Kanisa ambalo kitovu chake ni familia. Ndiyo! Uhusiano wetu na Mungu na dhumuni la maisha yetu ya duniani vinafafanuliwa katika muktadha wa familia. Injili ya Yesu Kristo ni mpango wa Baba yetu wa Mbinguni kwa manufaa ya watoto Wake wa kiroho. Kwa ukweli tunaweza kusema kwamba mpango wa injili kwanza ulifundishwa kwetu katika baraza la familia ya milele, unatekelezwa kupitia familia zetu za duniani, na hatima inayo kusudiwa ni kuwainua watoto wa Mungu katika familia za milele.

III.

Licha ya muktadha huu wa kimafundisho, kuna upinzani. Nchini Marekani tunateseka kwa kupungua kwa thamani ya ndoa na uzaaji wa watoto. Kwa takriban miaka mia moja wastani wa kaya zinazoongozwa na wanandoa umeshuka, na vile vile kiwango cha watoto kuzaliwa. Ndoa na kiwango cha watoto kuzaliwa cha waumi wa Kanisa letu ni chanya zaidi, lakini pia vimepungua sana. Ni muhimu kwamba Watakatifu wa Siku za Mwisho wasipoteze uelewa wao juu ya dhumuni la ndoa na thamani ya watoto. Hiyo ndiyo kesho tunayoitafuta. “Kuinuliwa ni suala la kifamilia,” Rais Nelson ametufundisha. “Ni kupitia tu ibada okozi za injili ya Yesu Kristo familia zinaweza kuinuliwa.”

Kushuka kwa takwimu hizi za kitaifa za ndoa na uzaliwaji wa watoto zinaeleweka kwa sababu za kihistoria, lakini maadili na desturi ya Mtakatifu wa Siku za Mwisho vinapaswa kuwa bora zaidi—siyo kufuata—mitindo hiyo.

Katika uvulana wangu miaka 80 iliyopita, niliishi katika shamba la babu na bibi yangu katika mazingira ambayo karibia yote yaliyofanyika katika siku yalikuwa chini ya maelekezo ya familia. Hapakuwa na televisheni au vifaa vya kielektroniki kuondoa umakini wetu kwenye shughuli za familia. Kinyume chake, katika jumuiya za kisasa za mjini, waumini wachache wanapata uzoefu endelevu wa shughuli zinazojikita kwenye familia. Maisha ya mjini na usafiri wa kisasa, burudani zilizopangiliwa, na mawasiliano ya kasi vimefanya iwe rahisi kwa vijana kuzifanya nyumba zao kama mabweni, mahali ambapo wanalala na kula mara chache na mahali ambapo hakuna uelekezi wa wazazi kuhusu shughuli zao.

Ushawishi wa wazazi pia umepunguzwa kwa kupitia njia ambazo waumini wengi wa sasa wa Kanisa wanatimiza mahitaji yao. Katika nyakati zilizopita, moja ya ushawishi mkubwa ulioziunganisha familia ni uzoefu wa kushughulika pamoja katika kutimiza lengo la pamoja—kama vile kuandaa mashamba au kujikimu kimaisha. Familia ilikuwa kikundi kilichoundwa na kuendeshwa cha kuzalisha uchumi. Leo, familia nyingi ni vikundi vya ufujaji wa uchumi, ambapo hakuitajiki shahada ya juu ya muundo wa familia au ushirikiano.

IV.

Kadiri ushawishi wa familia unavyopungua, Watakatifu wa Siku za Mwisho bado wana jukumu kutoka kwa Mungu la kuwafundisha watoto wao kujiandaa kwa ajili ya hatima ya familia yetu katika umilele (ona Mafundisho na Maagano 68:25). Wengi wetu lazima tufanye hili wakati si familia zetu wote ni za kitamaduni. Talaka, kifo, na utengano ni uhalisia. Nilipitia hilo katika familia ambayo nililelewa.

Familia ya Oaks

Baba yangu alifariki wakati nikiwa na umri wa miaka saba, hivyo mimi, kaka yangu mdogo na dada yangu tulilelewa na mama mjane. Katika hali ngumu sana, yeye aliendelea kusonga mbele. Alikuwa pekee yake, na aliye vunjika, lakini ufundishaji wake wenye nguvu wa mafundisho ya Kanisa lililorejeshwa ulituongoza. Jinsi gani alisali kwa ajili ya msaada wa kimbingu katika kuwalea watoto wake, na alibarikiwa! Tulilelewa katika nyumba yenye furaha ambamo marehemu baba yetu daima alikuwa uhalisia. Mama alitufundisha kuwa tulikuwa na baba na yeye alikuwa na mume na daima tutakuwa familia kwa sababu ya ndoa yao ya hekaluni. Baba yetu hakuwepo kwa muda tu kwa sababu Bwana alikuwa amemuita kwenye kazi tofauti.

Najua kwamba familia nyingine nyingi hazina furaha hii, lakini kila mama asiye na mume anaweza kufundisha juu ya upendo wa Baba wa Mbinguni na baraka za matokeo ya ndoa ya hekaluni. Wewe pia unaweza kufanya hili! Mpango wa Baba wa Mbinguni unahakikisha uwezekano huu kwa kila mtu. Sisi sote tunayo shukrani kwa ajili ya ndoa ya hekaluni na kwa baraka tarajiwa za kuunganishwa kama familia ya milele. Kama mama yangu, tunapenda kunukuu ahadi za Lehi kwa mwanawe Yakobo kwamba Mungu “ataweka wakfu mateso yako kwa faida yako” (2 Nefi 2:2). Hilo linatumika kwa kila familia ya Mtakatifu wa Siku za Mwisho, iliyo kamili au isiyo kamili kwa sasa. Sisi ni kanisa la kifamilia

Mafundisho yetu na imani yetu katika familia za milele vinatuimarisha na kutuunganisha. Katu sitosahau ahadi ya babu yangu mzaa mama, wakati sisi watoto tulipokuwa tukiishi kwenye shamba lake jirani na Payson, Utah. Alinipa habari mbaya kwamba baba yangu alikuwa amefariki mbali huko Denver, Colorado. Nilikimbilia ndani kwenye chumba cha kulala na kupiga magoti pembeni ya kitanda, nikilia kwa uchungu wa moyo. Babu alinifuata na akapiga magoti pembeni yangu na kusema, “Nitakuwa baba yako.” Ahadi hiyo nyororo ni mfano wenye nguvu wa kile babu na bibi wanachoweza kufanya ili kujaza pengo wakati familia zinapo poteza au wanapomkosa mwanafamilia.

Wazazi—mmoja au waliooana na wengine kama babu na bibi wanaojaza pengo hilo kwa watoto—ndio walimu wakuu. Ufundishaji wao wenye ufanisi zaidi ni kupitia mfano. Mduara wa familia ni mahali sahihi pa kuonyesha na kujifunza maadili ya milele kama vile umuhimu wa ndoa na watoto, dhumuni la maisha, na chanzo cha kweli cha shangwe. Pia ni mahali bora zaidi pa kujifunza masomo mengine muhimu ya maisha, kama vile ukarimu, msamaha, udhibiti binafsi, na thamani ya elimu na kazi ya uaminifu.

Hata hivyo, waumini wengi wa Kanisa wanao wapendwa wanafamilia ambao hawakumbatii maadili na matarajio ya injili. Waumini hao wanahitaji upendo na uvumilivu wetu. Katika kuhusiana kwetu sisi kwa sisi, tunapaswa kukumbuka kwamba ukamilifu tunao utafuta hauishii tu kwenye hali za duniani zenye msongo wa mawazo. Fundisho kuu katika Mafundisho na Maagano 138:57–59 linatuhakikishia kwamba toba na ukuaji wa kiroho vinaweza kuendelea katika ulimwengu wa kiroho ambao unafuatia maisha ya duniani. Muhimu zaidi, familia zinapo ungana ili kuimarishana, wote tunapaswa kukumbuka kwamba dhambi na mapungufu yasiyotabirika sisi sote tunayopitia duniani vinaweza kusamehewa kupitia toba kwa sababu ya Upatanisho mtukufu na wenye kuokoa wa Yesu Kristo.

V.

Mwokozi wetu Yesu Kristo ndiye mfano wetu wa mwisho. Tutabarikiwa kama tutafanya maisha yetu kwa mfano wa mafundisho Yake na dhabihu-binafsi. Kumfuata Kristo na kujitoa wenyewe katika huduma ya sisi kwa sisi ni tiba bora kwa ajili ya uchoyo na ubinafsi ambavyo sasa vinaonekana kuwa vya kawaida.

Wazazi pia wanao wajibu wa kufundisha watoto wao elimu kwa vitendo licha ya kanuni za injili. Familia zinaungana wanapo fanya mambo yenye kuleta tija kwa pamoja. Bustani za familia zinajenga uhusiano wa familia. Matukio ya furaha ya kifamilia yanaimarisha mshikamano wa familia. Kupiga kambi nje ya nyumba, shughuli za michezo, na burudani nyingine ni vya thamani sana kwa kuziunganisha familia. Familia zinapaswa kubuni mikusanyiko ya kifamilia ili kuwakumbuka mababu, mikusanyiko ambayo inatuongoza hekaluni.

Wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto katika ujuzi wa msingi wa maisha, ikijumuisha kufanya kazi zinazohusiana na ardhi na nyumbani. Kujifunza lugha ni maandalizi muhimu kwa ajili ya huduma ya umisionari na maisha ya kisasa. Walimu wa masomo haya wanaweza kuwa wazazi au babu na bibi au wanafamilia wengine. Familia zinachanua wanapojifunza kama kikundi na kushauriana pamoja juu ya masuala yote yahusuyo familia na wanafamilia.

Baadhi wanaweza kusema, “Lakini hatuna muda wa lolote kati ya haya.” Ili kupata muda wa kufanya kile kilicho cha muhimu, wazazi wengi wataona kwamba wanaweza kuifanya familia yao kuwa hai kama wao wote watazima teknolojiazao. Na wazazi, kumbukeni, kile watoto hao wanachotaka hasa wakati wa chakula cha jioni ni muda wa kuwa nanyi.

Baraka kuu huja kwenye familia kama wanasali pamoja, wakipiga magoti usiku na asubuhi ili kutoa shukrani kwa ajili ya baraka na kusali kuhusu mashaka yao ya pamoja. Familia pia zinabarikiwa wanapo abudu pamoja katika ibada za kanisa na pia katika mazingira ya ibada fupi. Mapatano ya kifamilia pia yanaimarishwa kwa hadithi za familia, kubuni desturi za familia, na kushirikishana matukio matakatifu. Rais Spencer W. Kimball alitukumbusha kwamba “hadithi zenye mwongozo wa kiungu kutoka katika maisha yetu wenyewe na zile za watangulizi wetu … ni zana za kufundishia zenye nguvu.” Mara nyingi ni vyanzo bora vya mwongozo wa kiungu kwa ajili yetu na wazao wetu.

Ninashuhudia juu ya Bwana Yesu Kristo ambaye ni Mwana wa Pekee wa Mungu Baba yetu wa Milele. Yeye anatualika tufuate njia ya agano ambayo inaongoza kwenye kukusanyika tena kwa familia yote ya mbinguni. Nguvu za kuunganisha za ukuhani, zikielekezwa na funguo zilizorejeshwa katika Hekalu la Kirtland, huzileta familia pamoja milele (see Mafundisho na Maagano 110:13–16). Kwa sasa zinatumika katika idadi inayokua ya mahekalu ya Bwana kote ulimwenguni. Hii ni kweli. Acha tuwe sehemu ya hili, nina sali, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Maktaba ya Injili.

  2. Russell M. Nelson, “Thanks for the Covenant” (Brigham Young University devotional, Nov. 6, 2005), 3, speeches.byu.edu.

  3. Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Kufungua Mbingu kupitia Kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia,” Liahona, Okt. 2017, 18.

  4. Spencer W. Kimball, “Therefore I Was Taught,Ensign, Jan. 1982, 4.