Mkutano Mkuu
Karama ya Milele ya Ushuhuda
Mkutano mkuu wa Oktoba 2025


12:17

Karama ya Milele ya Ushuhuda

Kila mwana au binti wa Mungu anaweza kujipatia maarifa ya ndani zaidi, thabiti na ya uhakika.

Wapendwa akina kaka na dada zangu, hivi majuzi nimekuwa nikitafakari juu ya kweli tatu zenye nguvu kutoka kwenye Urejesho. Kweli hizi zimebariki sana maisha yangu. Leo, ningependa kushiriki nanyi jinsi ambavyo kweli hizi zimeniongoza katika safari yangu kuelekea ushuhuda wa hakika wa injili ya Yesu Kristo.

1. Mungu ni Baba Yetu wa Mbinguni Mwenye Upendo

Yeye ni mjuzi wa yote na muweza wa yote. Kupitia Nuru ya Kristo na huduma ya Roho Mtakatifu, ushawishi Wake uko kila mahali. Ni asili yake kutubariki.

Yeye anauona wakati wetu uliopita, wa sasa, na hatma ya milele. Hakuna kinachoweza kufichwa kwake.

Mwaliko wa Rais Russell M. Nelson wa “fikiria selestia” unatuhimiza tuige ono na asili ya Baba yetu wa Mbinguni.

Kwa sababu ya sifa Zake takatifu, Baba yetu wa Mbinguni hutupatia kila zawadi nzuri, kila mmoja akiwa na mtazamo Wake wa milele na ono akilini.

2. Haki ya kujiamulia ni zawadi ya kuamua na kutenda wenyewe

Pia ni jukumu la kuchagua vyema.

Yesu Kristo alilipa gharama ya fursa hiyo kwa damu Yake yenye thamani.

Wakati mwingine tunaweza kuamini kuwa haki ya kujiamulia inamaanisha kufanya chochote tunachotaka. Lakini ukweli kwamba gharama ililipwa inamaanisha kuwa haki ya kujiamulia ni zawadi takatifu.

Sisi ni mawakala, na mawakala wanawajibika kwa jambo fulani. Katika hali hii, tunawajibika kwa uchaguzi tunaofanya kulingana na ujuzi tulionao na karama tunazopewa. Hatuwezi kufanya uchaguzi bila kuwajibika kwa matokeo.

Kwa nini tuna haki ya kujiamulia?

Kuchagua mema.

Kumchagua Kristo.

Kuchagua uzima wa milele—tena na tena.

3. Ushuhuda Wetu Huja Kupitia Nguvu ya Roho Mtakatifu

Ushahidi kutoka kwa Roho Mtakatifu ni mkuu kuliko kuona. Yeye ndiye shahidi mkuu wa Baba na Mwana. Rais Nelson alifunza, “Katika siku zijazo, haitawezekana kunusurika kiroho bila uzoefu wa kuongoza, kuelekeza, kufariji na ushawishi wa daima wa Roho Mtakatifu.”

Akina kaka na akina dada, hii ndiyo sababu kila mmoja wetu anahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu leo.

Ushuhuda kupitia Roho Mtakatifu unaweza kuja kwa njia nyingi. Kama balbu ya mwanga katika chumba chenye giza, unaweza kuwaka kwa kasi na ghafla. Unaweza kuja kama jua hatua kwa hatua na baada ya muda. Unaweza kuja kama miale ya mwanga, mfiduo wa mara kwa mara kwenye akili safi. Vyovyote vile, huja kupitia kwa Roho Mtakatifu.

Kupata Ushuhuda huko Jamaica

Nilikulia katika Jamaika nzuri; ilikuwa ya kufurahisha na ya kupendeza. Hata hivyo, nilipoanza shule ya upili, baadhi ya wanafunzi wenzangu na marafiki hawakuelewa uamuzi wangu wa kuwa mshiriki wa Kanisa la Yesu Kristo. “Ungewezaje kujiunga na kanisa hilo?,” wangeuliza. “Ungewezaje kuamini hadithi hiyo?”—wakirejelea Ono la Kwanza. “Ungewezaje kusoma kitabu hicho?”—wakirejelea Kitabu cha Mormoni. “Je, kweli unaamini hayo yote?” Na “Kwa nini unapoteza maisha yako?”

Hekalu la Salt Lake.
Kijisitu Kitakatifu
Kitabu cha Mormoni

Ilikuwa inaumiza, hasa ilipotoka kwa watu niliowajali.

Lakini jambo ambalo hawakujua lilikuwa hili: Nilipata uzoefu kwa Roho Mtakatifu. Ushuhuda huo ulipojaa moyoni mwangu, ulipunguza uchungu wa siku, na “kwa muda mfupi, mtazamo wa mbinguni [ulionekana] mbele ya macho yangu.”

Labda umeulizwa baadhi ya maswali haya. Labda, hata sasa unashambuliwa kama ilivyokuwa kwangu.

Karama na ushuhuda wa Roho Mtakatifu vinapatikana kwa kila mtu.

Jamaika kwangu ni kama Palmyra ilivyokuwa kwa Joseph Smith. Ni Kijisitu changu Kitakatifu. Sijui mahali hasa ambapo Joseph alipiga magoti kusali katika Kijisitu Kitakatifu, lakini ninajua hasa mahali nilipokuwa wakati Kijisitu changu Kitakatifu kilipokuja kuwa halisi. Ilitokea katika Barabara ya Four Grove, Mandeville, Jamaika, bafuni kwangu, saa 12:00 asubuhi siku ya Jumatano miaka mitatu baada ya ubatizo wangu. Uzoefu huu mtakatifu ulitokea kwa sababu wiki mbili mapema dada mmisionari aliyetiwa moyo alinialika kusoma Kitabu cha Mormoni. Dada Audrey Krauss anahudhuria mkutano huu leo ​​pamoja na familia yake, na ninampenda milele.

Mzee Brown akiwa kijana pamoja na mmisionari wa kike

Uzoefu huo ulinibadilisha.

Akina kaka na akina dada, ushuhuda hautolewi kwa matumizi ya muda. Zawadi hii kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo imekusudiwa kuwa ya milele kwa sababu mtoaji ni wa milele. Ushuhuda haupaswi kuwa na tarehe ya mwisho wa matumizi. Haupaswi kudhoofika au kupungua kwa sababu kitu fulani katika maisha yangu kimebadilika au kitu kimebadilika ulimwenguni. Unapaswa kuwa na nguvu zaidi kwa sababu, kama vile talanta ya mtumishi katika mfano wa talanta, ushuhuda wangu binafsi ni zawadi ya kuzidishwa—si kuzikwa.

Nikitazama nyuma hizo siku ngumu za majaribio na mateso ambazo nilizipitia kama mtoto zilinisaidia kupata nafasi pale sasa ninapojua mwenyewe. Siamini tu, au kutumaini, ingawa hizi ni chembe muhimu za imani kwenye njia ya ushuhuda wa kweli. Ninakupongeza kwa kutengeneza njia yako mwenyewe kwa kuuliza maswali, kusoma, kuomba, kufunga na kutafakari. Tafadhali usisimame. Inafaa kila juhudi kufuata njia hii ya ushuhuda. Ni nani utamruhusu au nini utakiruhusu kuuchukua? Ni ushahidi gani mkubwa zaidi unaoweza kupata kuliko ule kutoka kwa Mungu?”

Kila mwana au binti wa Mungu anaweza kujipatia maarifa ya ndani zaidi, thabiti na ya uhakika. Kama Joseph Smith, ambaye alithibitisha ushuhuda wake licha ya upinzani, tunaweza kusema kwa ujasiri, “Nilijua, na nilijua kwamba Mungu alijua, na nisingeweza kukataa, wala kuthubutu kufanya hivyo.”

Akina kaka na dada zangu wapendwa, acha mche mdogo wa ushuhuda ufanye kazi ndani yenu hadi kuchipua kufikia maarifa yenye utukufu wa uhakika.

Kama wewe umebatizwa na kuthibitishwa kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lakini bado unahangaika na, “Sina hakika kama najua,” tafadhali kumbuka ahadi hii katika sala ya sakramenti: “Ili Roho wake apate kuwa pamoja nao daima.” Kwa sababu ya ahadi hii, kila mmoja wetu anaweza kufuata njia ya ushuhuda na maarifa ya uhakika.

Simamia Ushuhuda Wako

Sasa hapa kuna ukweli mkuu: Kwa njia yoyote ile ushuhuda unatolewa—iwe ni mwangavu kama mawio ya jua au unakuja katika ono tukufu—bado inahitajika uchaguzi kupokea zawadi hii ya thamani.

Kusema “Ninachagua kuamini” hurahisisha kupokea ushuhuda kutoka kwa Mungu. Ikiwa tunaona ushuhuda wetu unadhoofika, kumbuka kwamba ni chaguzi tunazofanya ambazo zinapunguza nguvu ya ushuhuda. Lakini ushuhuda haujaenda popote. Tunahitaji tu kuchagua kuungana nao tena.

Kuchagua kuamini ni njia ya busara na yenye nguvu ya kutumia haki yako ya kujiamulia.

Siwezi kuona njia bora ya kutumia haki yangu ya kujiamulia kuliko kutetea ushuhuda wangu.

Rais Nelson alifundisha: “Ninakusihi wewe kuchukua udhibiti wa ushuhuda wako. Ufanyie kazi. Umiliki. Utunze. Ulee ili kwamba uweze kukua. Ulishe ukweli.”

Kwangu, maneno simamia, fanya kazi, jali, miliki, lea na lisha yanasikika kama wakala aliyepewa usimamizi kwa kitu cha thamani na muhimu.

Katika Kanisa la awali, Parley P. Pratt alihisi kutoridhika na Nabii Joseph Smith na alichagua kumkosoa yeye na Kanisa. Wakati John Taylor ambaye Parley alimfundisha injili alipokuja mjini, Parley alimchukua kando na kumwonya kutomfuata Joseph. John Taylor akamwambia Parley:

“Kabla hujaondoka Kanada, ulitoa ushuhuda wenye nguvu wa Joseph Smith kuwa nabii wa Mungu, … na ulisema ulijua mambo haya kwa ufunuo na kipawa cha Roho Mtakatifu.

“… Sasa ninao ushuhuda uleule ambao wewe uliufurahia wakati ule. Kama kazi ilikuwa kweli miezi sita iliyopita, ni kweli leo. Kama Joseph Smith alikuwa nabii hapo mwanzo, basi hata sasa yeye ni nabii.”

Mimi nashuhudia kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu na kwamba vazi la kinabii alilopokea linaendelea leo. Yesu Kristo anaongoza kazi hii.

Ninawaalika kufikiria kuhusu njia yako ya ushuhuda wa uhakika wa Yesu Kristo na injili Yake. Simamia ushuhuda wako; tumia haki yako ya kujiamulia kwa busara na mtambue mtoaji na sifa Zake zote tukufu. Ninashuhudia kwamba nguvu iko ndani yako. Hakuna mtu anayeweza kukuchagulia. Hakuna mtu anayeweza kuchukua zawadi hii. Unaweza kuchagua kuamini.

Ninaahidi kwamba ukifanya hivi, ushuhuda wako utakuwa “maji ya kisima cha uzima, yakichipuka hata uzima wa milele.” Utakuwa ngao na ushawishi, na pia utakusaidia wewe pindi upitiapo magumu. Utakuwezesha katika kukuza karama za kiroho. Utakusaidia katika kuhudumu na huduma yako binafsi. Utakuwa silaha dhidi ya shetani na ushawishi wake. Ushuhuda wako utakuwa furaha unapouona ukisambaa kwa watoto wako, wajukuu, na vitukuu na kwa wale unaowapenda na kuwahudumia. Utakuwa wenye nguvu unapoushiriki na kuutumia kushuhudia.

Kama unajua, unajua. Ninajua kwamba ninajua. Tunahitaji mashahidi wa kweli wa Yesu Kristo na injili yake. Fika huko! Utafute! Ni jambo la dharura! Hiki ni kipindi cha mwisho—kipindi cha utimilifu wa nyakati.

Yesu Kristo alisema ukweli huu:“Mbingu na dunia zitapita; maneno yangu hayatapita.”

Akina kaka na akina dada, ushuhuda wa Yesu Kristo haukukusudiwa kamwe kuwa zawadi ya muda. Hakuna chochote kuhusu ushuhuda huo kilicho cha muda—si mtoaji, si zawadi yenyewe, si mfikishaji wa zawadi, si yule ambaye zawadi inamuhusu. Ushuhuda wako na uelezewe kwa njia sawa na hii. Ingawa “mbingu na dunia zitapita,” ushuhuda wako na ushahidi wa injili ya Yesu Kristo havitapita. Sasa ni muda wa kutwaa zawadi hii ya thamani. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, na sisi ni watoto Wake. Yeye alituumba sisi kwa mfano Wake. Yeye ana mwili uliotukuka, Mkamilifu “mwili wa nyama na mifupa wenye kushikika kama wa mwanadamu” (Mafundisho na Maagano 130: 22).

    “Mungu anatujua binafsi, na Yeye anatupenda sana kuliko tunavyoweza kuelewa. Yeye anaelewa majaribu yetu, huzuni, na udhaifu wetu, na Yeye hutoa msaada kupitia hayo. Yeye hufurahia maendeleo yetu na atatusaidia tufanye chaguzi sahihi. Anataka kuwasiliana nasi, na sisi tunaweza kuwasiliana Naye kupitia sala” (Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo [2023], 33).

  2. Ona Mafundisho na Maagano 84:46–47; 88:12–13.

  3. “Kwa sababu tu Mungu ni Mungu, kwa sababu tu Kristo ni Kristo, hawawezi kufanya zaidi ya kutujali na kutubariki na kutusaidia ikiwa tu tutakuja kwao, tukikaribia kiti chao cha enzi kwa upole na unyenyekevu wa moyo. Hawawezi kufanya kinyume zaidi ya kutubariki. Wanapaswa kufanya hivyo. Iko katika asili yao” (Jeffrey R. Holland, “Come unto Me” [Brigham Young University devotional, Mar. 2, 1997], 4, speeches.byu.edu).

  4. Ona Luka 12:2; Moroni 7:22; Ibrahimu 2:8.

  5. “Ninakualika ufuate mazoea ya ‘kufikiria selestia’! “Kufikiria selestia humaanisha kufikiria kiroho. Tunajifunza kutoka kwa Yakobo nabii wa Kitabu cha Mormoni kwamba kufikiri kiroho ni uzima wa milele. (Russell M. Nelson, “Fikiria Selestia!,” Liahona, Nov. 2023, 117).

  6. Ona Topics and Questions, “Agency and Accountability,” Gospel Library; see also 2 Nephi 2:11, 16.

  7. Ona 1 Petro 1:18–20; Ibrahimu 3:22–28.

  8. Ona 1 Wakorintho 6:20.

  9. Ona Mafundisho na Maagano 101:78.

  10. “Injili ya Yesu Kristo ni mpango ambao hutuonyesha jinsi ya kuwa kile ambacho Baba yetu wa Mbinguni anatamani sisi tuwe. …

    “… Hali hii ya kutokuwa na mawaa na wakamilifu itatokana na mwendelezo imara wa maagano, ibada, na matendo, mkusanyiko wa chaguzi sahihi, na kutokana na toba endelevu” (Dallin H. Oaks, “Changamoto ya Kuwa,” Liahona, Jan. 2001, 40, 41; msisitizo umeongezwa); ona pia Musa 7:33.

  11. Ona Moroni 10:4–5.

  12. “Roho haihitaji kuwa na maneno tu; Anaweza kuwasiliana na Roho kwa roho kwa lugha ambayo ni dhahiri kwa sababu haina maneno. Ni mawasiliano ya maarifa safi na akili kutoka kwa Roho, na nimekuja kujua kwamba kwa kweli ndiyo njia bora ya kupata ujuzi. Ina nguvu na hudumu kwa muda mrefu kuliko kugusa au kuona; tunaweza kuja na mashaka juu ya hisia za kimwili, lakini hatuwezi kuwa na shaka wakati Roho Mtakatifu anazungumza nasi. Ni shahidi wa uhakika. Kwa sababu hii, dhambi isiyosameheka ni kumkana Roho Mtakatifu au ushuhuda wa Roho Mtakatifu” (D. Todd Christofferson, “Strong Impressions of the Spirit,” Liahona, June 2013, 49).

  13. Ona Yohana 5:32; 2 Nefi 31:18; 3 Nefi 11:36.

  14. Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 96. Katika hotuba hiyo hiyo alisema:

    “Ninawahimiza kuwa na uwezo zaidi wa kiroho kuliko sasa ili kupokea ufunuo binafsi. …

    “Ee, kuna mengi zaidi Baba yako wa Mbinguni anataka wewe uyajue. Kama Mzee Neal A. Maxwell alivyofundisha, “Kwa wale wenye macho ya kuona na masikio ya kusikia, ni wazi kwamba Baba na Mwana wanatoa siri za ulimwengu!’ …

    “… Chagua kufanya kazi ya kiroho inayohitajika ili kufurahia karama za Roho Mtakatifu na kuisikia sauti ya Roho kila mara na kwa uwazi zaidi” (95, 96).

  15. Ona David A. Bednar, “Roho wa Ufunuo,” Liahona, Mei 2011, 87–90; Alexander Dushku, “Miale na Mwangaza,” Liahona, Mei 2024, 14–16.

  16. “Ushuhuda,” Nyimbo za Dini, na. 69

  17. Ona Hesabu 11:29; Yakobo 1:5.

  18. Ona Mafundisho na Maagano 20:28; Musa 1:3.

  19. Ona Mathayo 25:14–30. Ushahidi wa kiroho nilioupata kutoka kwa Roho Mtakatifu … haujapita bado. Na kwa hakika, umekuwa imara zaidi. Vitu nilivyojifunza katika ujana wangu kuhusu kanuni za msingi za injili ya Yesu Kristo zimekuwa ni msingi wangu imara katika maisha yangu yote.” (Dieter F. Uchtdorf, “Rutubisha Mizizi, na Matawi Yatakua,” Liahona, Nov. 2024, 101).

  20. Mafundisho na Maagano 6:23.

  21. Joseph Smith—Historia ya 1:25.

  22. Ona Alma 32:27, 30, 37–38, 41.

  23. Ona Mafundisho na Maagano 20:77.

  24. Ona Mafundisho na Maagano 88:33.

    “Kisha pengine kuna sehemu muhimu sana, ni kule kupokelewa kwa zawadi. … Kwa kweli kupokea zawadi, tunakuja kuithamini kwa ajili yetu wenyewe, kuiweka katika matumizi kamili katika maisha yetu na kisha tunamkumbuka kwa shukrani mtoaji.

    “Kupokea zawazi siyo mchakato baridi bali ni mchakato wa kusudi na wa maana ambao unaenda mbali zaidi ya kufungua kifurushi. Kupokea ni kuthamini na kuunganika na vyote viwili zawadi na moyo wa mtoaji katika njia ambayo inaimarisha muunganiko kati ya yule mtoaji na mpokeaji” (Patrick Kearon, “Pokea Zawadi Yake,” Liahona, Mei 2025, 121–22).

  25. Russell M. Nelson, “Choices for Eternity” (worldwide devotional for young adults, May 15, 2022), Maktaba ya Injili.

  26. Ona Mafundisho na Maagano 70:3–4.

  27. Saints: The Story of the Church of Jesus Christ in the Latter Days, vol. 1, The Standard of Truth, 1815–1846 (2018), 280-81.

  28. Ona Mosia 4:9–12.

  29. Mafundisho na Maagano 63:23; msisitizo umeongezewa.

  30. Ona Alma 5:46–48. Joseph Smith alifundisha kwamba “wokovu hauwezi kuja bila ufunuo. Ni bure kwa mtu yeyote kuhudumu bila ufunuo huo. … Hakuna mtu ambaye ni mtumishi wa Yesu Kristo bila kuwa nabii. Hakuna mtu anayeweza kuwa mtumishi wa Yesu Kristo ila yeye awe na ushuhuda wa Yesu, na hii ni roho ya unabii” (The Joseph Smith Papers, volume C-1 [2 November 1838–31 July 1842] [addenda], 12, josephsmithpapers.org; tahajia, herufi kubwa, na matamshi ni ya kisasa).

  31. “Tunasimama kwenye kilele cha enzi, kushangazwa na hisia za ukuu na taadhima ya historia. Hiki ndicho kipindi cha mwisho ambacho kwacho vyote vilivyopita vimeelekeza.” (Gordon B. Hinckley, “At the Summit of the Ages,” Liahona, Jan. 2000, 90).

  32. Mathayo 24:35.

  33. Ona Moroni 10:30.