Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Fanya Sehemu Yako kwa Moyo Wako Wote
Dondoo
Ujerumani
Kwa neno jepesi, uanafunzi huhitaji nidhamu. …
… Imani yetu, ambayo ni utiifu wetu kwa Mwokozi, huwa imara pale inapojaribiwa dhidi ya upinzani tunaokutana nao hapa duniani. Imani hustahimili kwa sababu tunaendelea kuilisha, kuendelea kuitumia na kutokata tamaa.
Kwa upande mwingine, ikiwa tunashindwa kutumia imani na nguvu zake za kusadikisha, tunakuwa na uhakika dhaifu wa vitu tulivyoviona vitakatifu hapo mwanzo—ujasiri hafifu kwa vitu tulivyojua awali kuwa ni vya kweli.
Moto wa ushuhuda wa jana unaweza kutupatia joto kwa muda tu.
… Karama zetu hukua na kuongezeka tu pale tunapozitumia. …
Inaweza kuwa kweli kwamba karama zetu za kiroho daima sio za kuvutia, lakini hiyo haimaanishi si za muhimu. …
Basi kila mmoja wetu afanye sehemu yetu ndogo. …
Kumbuka, ni Yesu Kristo ambaye amekwishafanya sehemu ya kuzidi binadamu wakati aliposhinda kifo na dhambi.
Sehemu yetu ni kumfuata Kristo. …
Pale ambapo imani ni dhaifu, anza na tumaini katika Kristo Yesu na nguvu Yake ya kusafisha na kutakasa. …
Tunajua kwamba jitihada zetu pekee haziwezi kutufikisha selestia. Lakini zinaweza kutufanya watiifu na wenye kudhamiria kwa Yesu Kristo, na Yeye atatufikisha selestia. …
… Tuna shukrani kwa hatua tulizopiga jana, lakini tusikwamie hapo. Tunajua bado tuna njia ndefu ya kusonga mbele, lakini haturuhusu hilo litukatishe tamaa.
Hicho ndicho kiini cha sisi ni nani—kama wafuasi wa Kristo.