Kikao cha Jumamosi Jioni
Yesu Kristo na Mwanzo Wako Mpya
Dondoo
Japan
Kituo cha Mikutano, Marekani
Nigeria
Yesu “Alizunguka huko na huko, akitenda mema.” … Ni maelezo pungufu kiasi gani! …
Kila kitu alichosema na kufanya kilitoa mwanzo mpya kwa kila mmoja wa wale aliowaponya, kuwabariki, kuwafundisha, na kuwaondolea dhambi. Hakujiweka mbali nao, na hakika hatajiweka mbali nawe. …
… Sisi sote tunaweza kuwa na mwanzo mpya kupitia Yesu Kristo, na kwa sababu ya, Yesu Kristo. Hata wewe. … Hili ni Kanisa la mianzo mipya! …
Toba inafungua mlango wa mwanzo wetu mpya, mwanzo msafi, na nafasi za pili. …
… Alfajiri mpya, sura mpya, na nafasi mpya ni kiini kirahisi cha habari njema ya injili!
… Adui pekee ndiye anayenufaika na wazo kwamba umezama. Haujazama.
Na mianzo mipya ni zaidi ya dhambi zetu na makosa. … Unaweza kweli kubadilisha mambo kuhusu wewe mwenyewe ambayo yamekuwa yakikukandamiza kwa miaka. …
Kwa wale wanao taabika na dhambi ile ile au kushindwa kule kule mara kwa mara, endelea kusonga mbele. … Na utumaini katika mwanzo mpya ambao uko kwako kila wakati unapomrudia Baba yako katika uaminifu wa moyo. …
… Tafadhali pokea mwanzo wako mpya, hata leo, sasa hivi. Yesu Kristo ni Mwanzilishi na Mtimizaji wa imani yetu, akiandika aya nyingi mpya pamoja nasi. Yeye ni Mwanzo na Mwisho—mwisho wa aibu zetu na mateso na mwanzo wa maisha mapya ndani Yake, akituruhusu kuacha yaliyopita na kuanza tena kwa alfajiri mpya mara nyingi kadiri tunavyohitaji.