Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Heri Wapatanishi
Dondoo
Brazili
Kituo cha Mikutano, Marekani
Yesu Akitoka Kaburini, na Dan Burr
Hebu tuzingatie zaidi maeneo haya matatu ambapo Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa leo “anakuwa mpatanishi.
Kwanza ni ndani ya mioyo yetu. …
… Injili ya Yesu Kristo hukuza na kufuma pamoja tabia hizi za kiungu, ikijumuisha upatanishi, ndani ya mioyo yetu, zikitubariki katika maisha haya na yajayo.
Pili, kujenga upatanishi ndani ya nyumba zetu—kwa kutumia mpangilio wa Bwana kushawishi mahusiano kati yetu: ushawishi, uvumilivu, upole, ukarimu, unyenyekevu na upendo usio unafiki. …
… Ili kuwa wapatanishi, tunawasamehe wengine na kwa makusudi kuwainua wengine badala ya kuwashusha chini.
Tatu, upatanishi kwenye jumuiya zetu. …
… Katika mikusanyiko yetu na jumuiya, na tuchague kutazamana kama watoto wa Mungu.
Kwa ufupi, ninatoa mwaliko. … Je, unaweza kuzingatia mpango wa wiki moja, wenye hatua tatu wa mpatanishi?
-
Nyumba isiyo na mabishano: Wakati mabishano yanapoanza, tulia na anza upya kwa maneno na matendo ya ukarimu.
-
Kujenga maelewano mtandaoni: Kabla ya kuposti, kujibu, au kutoa maoni mtandaoni, uliza, Je hili litaleta maelewano? Ikiwa halileti, acha. Usitume. Badala yake, shiriki wema. Tangaza amani mahala pa chuki.
-
Rekebisha na unganisha tena: Kila mwanafamilia angeweza kutafuta uhusiano uliovunjika ili kuomba msamaha, kuhudumu, kurekebisha, na kuunganisha. …
Upatanishi ni sifa kama ya Kristo. …
Tunatimiza jukumu letu la kiungu kama watoto wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo kadiri tunavyojitahidi kuwa wapatanishi.