Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Tuni Moyo Wako kwa Yesu Kristo: Zawadi Takatifu ya Muziki wa Watoto
Dondoo
Brazili
Ufilipino
Marekani
Nimepata shangwe katika kuunganika na Watakatifu wenzangu kupitia lugha moja ya muziki mtakatifu. Na hususan kupitia nyimbo rahisi za Watoto, Roho Mtakatifu amevuka vizuizi vya lugha na kuujaza moyo wangu kwa minong’ono Yake. …
… Muziki wa Watoto ni mojawapo ya zana za Mungu zilizo nyororo kwa ajili ya kupanda mbegu za ushuhuda katika mioyo ya wanafunzi wadogo zaidi wa Mwokozi. …
… Muziki daima umekuwa kiini cha kuwafundisha watoto injili. Nyimbo za Watoto zinaweza kuwa lugha ya kwanza ya kiroho ya mtoto kwa sababu mapigo yake rahisi, ya kukumbukwa hutoa sauti kwenye kweli za injili. …
Nyimbo za Watoto zinaweza pia kuwa nyenzo zenye nguvu za kufundisha mafundisho. Baadhi ya nyimbo husimulia hadithi za maisha na huduma ya Mwokozi. Zingine hufundisha kuhusu sifa Zake, kama vile imani Yake, tumaini Lake, na hisani Yake. Na nyimbo takatifu zaidi hushuhudia juu ya Upatanisho Wake usio na mwisho na upendo unao tiririka kutokana na tendo hilo la wokovu. …
Wimbo ulioimbwa katika umri wa miaka sita una nguvu ya kubaki nasi—na unaweza kurudi miongo mingi baadaye katika nyakati za uamuzi, jaribu, huzuni, au shangwe.
… Roho anaweza kutumia muziki ili kuchonga kweli za milele katika mioyo yao michanga. Na baada ya muda, watoto wanaweza kuchagua kutuni na kugeuza mioyo yao na maisha yao kumwelekea Yesu Kristo kwa kufanya na kushika maagano matakatifu na Yeye. …
Marafiki wapendwa, ninashuhudia kwamba nyimbo za Watoto hufundisha kweli za milele na mafundisho ambayo hutuongoza kwa Yesu Kristo na injili Yake.