2025
Ni Waamuzi Wao Wenyewe
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Novemba 2025


Kikao cha Jumapili Mchana

Ni Waamuzi Wao Wenyewe

Dondoo

alt text

Marekani

Pakua PDF

Lengo la msingi la Uumbaji na uwepo wetu duniani ni kutupatia fursa ya kutenda na kuwa kile ambacho Bwana anatualika kuwa. …

… Hatujabarikiwa na haki ya kujiamulia ya kimaadili kufanya chochote tunachotaka wakati wowote tunapotaka. Badala yake, kulingana na mpango wa Baba, tumepokea haki ya kujiamulia ya kimaadili ya kutafuta na kutenda kulingana na ukweli wa milele. …

Rais Dallin H. Oaks amesisitiza kwamba injili ya Yesu Kristo inatualika sote kujua kitu fulani na kuwa kitu fulani kupitia matumizi mema ya haki ya kujiamulia ya kimaadili. …

[Na bado] kazi zetu na matamanio yetu pekee havituokoi sisi. “Baada ya yote tunayoweza kufanya,” tunapatanishwa na Mungu tu kupitia rehema na neema inayopatikana kupitia dhabihu ya Mwokozi isiyo na mwisho na ya milele ya kulipia dhambi. …

Wengi wetu tunaweza kutarajia kwamba kusimama kwetu mbele ya kiti cha Mwamuzi wa Milele kutakuwa sawa na mashtaka katika mahakama ya kidunia ya sheria. Hakimu ataongoza. Ushahidi utawasilishwa. Hukumu itatolewa. Na kuna uwezekano tutakuwa bila uhakika na wenye hofu hadi tutakapojua matokeo ya mwisho. Lakini naamini maelezo kama hayo sio sahihi. …

Kumcha Bwana si uoga wa wasiwasi kuhusu kuja kwenye uwepo Wake kuhukumiwa. Badala yake, ni matarajio ya hatimaye kujitambua kuhusu sisi wenyewe “mambo kama yalivyo” na “kama vile yatakavyokuwa.” …

Hatimaye, basi, sisi ni waamuzi wetu wenyewe. Hakuna atakayehitaji kutuambia wapi pa kwenda. Katika uwepo wa Bwana, tutakiri kile tulichochagua kuwa katika maisha ya duniani na kujua wenyewe pale tunapopaswa kuwa katika umilele.