Kikao cha Jumamosi Mchana
Bwana Anaharakisha Kazi Yake
Dondoo
Chile
Marekani
Kuna ushahidi wa wazi kwamba imani katika Yesu Kristo inaongezeka katika siku yetu. Katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kumekuwa na ongezeko kubwa la waongofu na ushiriki wa waongofu. …
… Bwana anapoharakisha kazi Yake, tunapaswa kuwapenda, kuwalea, na kuwahudumia wale wanaoikubali injili Yake. …
Kwa wale kati yenu ambao ni wapya au wanaorudi kwenye imani, kuna changamoto mnazoweza kukabiliana nazo. Kuwa na subira kwako mwenyewe. …
Kupokea ibada na maagano na kuishi amri ni muhimu. Fokasi kwenye maagano yanayohitajika kwa ajili ya kuinuliwa. …
Kujifunza mafundisho safi ya Yesu Kristo ni kazi ya maisha yote, yote katika kuelewa mafundisho na kuishi maisha kama ya Kristo. Maagano muhimu yanatoa mfumo ambao tunauelezea kama njia ya agano. …
Kama utaweka lengo la kupokea kila agano linalohitajika kwa ajili ya kuinuliwa, utakuwa kwenye njia inayoongoza kwenye ufalme wa selestia. Hekalu na ibada za hekaluni lazima viwe fokasi yetu. …
Sisi sote tunajisikia tusiotosha pale tunapojitahidi kuwa kama Yesu Kristo. Upatanisho Wake unaturuhusu kutubu kila siku tunapokosea. …
Kumfuata Mwokozi na mafundisho Yake hakujawahi kuwa rahisi katika ulimwengu ambao daima upo katika vurugu. … Kwa bahati nzuri, manabii walio hai hutoa mwongozo ambao tunauhitaji mahususi kwa ajili ya siku zetu. …
… Ninatoa ushuhuda wangu wa hakika na wa kweli kwamba Yesu Kristo anaishi, na kwa sababu ya Upatanisho Wake, tunaweza kuwa na umoja pamoja Naye.