Kikao cha Jumamosi Mchana
Tangazo la Familia—Maneno kutoka kwa Mungu
Dondoo
Marekani
Ninalipenda tangazo la familia. … Tangazo hili lina asili ya kiungu, hivyo lazima tulichukulie kwa unyenyekevu unaostahili maneno yanayotoka kwa Mungu. …
Lilipowasilishwa, tangazo hili halikufungamana na mitazamo ya wengi ulimwenguni. Siyo wakati huo. Siyo kwa sasa. Kuna wale ambao wanaona kasoro katika hili tangazo juu ya familia, ndoa na jinsia. Baadhi wanapendekeza Kanisa liliondoe, lifanye marejeo au hata kuliweka kando tangazo hili.
Tangazo hili juu ya familia, kama Rais Hinckley alivyoeleza, ni mafundisho, wapendwa kaka zangu na dada zangu. Kanuni hizi haziko nje ya hatua bali kikamilifu ndani ya hatua pamoja na njia za Bwana na njia Yake ya agano. Mafundisho ya tangazo hili yalifunuliwa na Bwana wetu Yesu Kristo kwa Mitume Wake wakati huo na sasa. …
Kwa wale wenye mashaka, jua kwamba wewe ni mtoto wa wazazi wa mbinguni, sehemu ya familia ya Baba wa Mbinguni. Hakuna mtu anayekujua vizuri zaidi au anayejali kwa kina zaidi kuhusu wewe kuliko Yeye anavyokujali. Mgeukie Yeye; mimina moyo wako Kwake; mtumainie Yeye na ahadi Zake. …
Tunapata katika tangazo la familia:
“Akina Baba na akina mama wana wajibu wa kusaidiana mmoja na mwingine kama wenza walio sawa.”
Sawa ni neno muhimu. …
Tunapoishi macho yetu yakiwa kwenye utukufu wa Mungu pekee, tunaheshimiana na kusaidiana. …
Baba yetu wa mbinguni ametoa tangazo hili juu ya familia ili kusaidia kutuongoza sisi nyumbani Kwake, ili kutusaidia kujifunza na kujawa na upendo, nguvu, dhumuni na uelewa wa milele.