Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Familia-Kitovu cha Injili ya Yesu Kristo
Dondoo
Mongolia
Argentina
Mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kitovu chake ni familia. …
Licha ya muktadha huo wa kimafundisho, kuna upinzani. …
Kupungua kwa ndoa na kuzaa watoto kitaifa kunaeleweka kwa sababu za kihistoria, lakini maadili na desturi za Watakatifu wa Siku za Mwisho zinapaswa kufanya vizuri zaidi—sio kufuata—mitindo hiyo. …
Wakati ushawishi wa wazazi unapofifia, Watakatifu wa Siku za Mwisho bado wana jukumu lililotolewa na Mungu la kuwafundisha watoto wao kujiandaa kwa ajili ya hatima ya familia yetu katika umilele (ona Mafundisho na Maagano 68:25). …
Mwokozi wetu Yesu Kristo ni mfano wetu wa mwisho wa kuigwa. … Kumfuata Kristo na kujitolea wenyewe katika kuhudumiana sisi kwa sisi ni tiba bora ya uchoyo na ubinafsi ambavyo sasa vinaonekana kuwa vya kawaida sana.
Wazazi pia wana wajibu wa kuwafundisha watoto wao maarifa ya vitendo mbali na kanuni za injili. …
… Familia hustawi wanapojifunza kama kundi na kushauriana pamoja juu ya mambo yote yenye dukuduku kwa familia na washiriki wake. …
Baraka kuu huja kwa familia ikiwa watasali pamoja, wakipiga magoti usiku na asubuhi kutoa shukrani kwa ajili ya baraka na kusali juu ya mambo yanayoigusa familia nzima. Familia pia zinabarikiwa pale wanapoabudu pamoja katika ibada za Kanisani na katika mazingira mengine ya ibada. miunganiko ya kifamilia pia inaimarishwa na hadithi za familia, kubuni desturi za familia, na kushiriki matukio matakatifu. …
Ninashuhudia juu ya Bwana Yesu Kristo, ambaye ni Mwana wa Pekee wa Mungu, Baba yetu wa Milele. Anatualika kufuata njia ya agano ambayo inatuongoza kwenye muunganiko wa familia ya mbinguni.