Rafiki
Kushiriki Habari Njema
Machi 2026


“Kushiriki Habari Njema,” Rafiki, Machi 2026, 36–37.

Kushiriki Habari Njema

Hadithi ya kweli kutoka Kenya.

Vielelezo vya miti ya miembe, nyumba za mapaa ya makuti, na mwanamke akimpa mvulana mdogo sahani ya asusa

Jumapili moja angavu ya Pasaka, Ryan aliamka mapema na kukimbilia jikoni. Aliweza kunusa harufu ya nazi na viungo kutoka kwenye mahanjumati Mama aliyokuwa ametengeneza punde tu. Ryan alichukua na kung’ata moja ya donati za motomoto, za pembe tatu, laini kama sufi. “Mama! “Ni Pasaka. Je, tunaweza kutazama sinema ya Yesu leo?” aliuliza kwa tabasamu bashasha.

Mama alimtazama na kutabasamu. “Bila shaka!”

Kaka mdogo wa Ryan, Liam, alikimbia nje wakati Mama na Ryan walipokaa chini ili kutazama sinema hiyo.

Kielelezo cha mwanamke na mvulana wakiwa wamekaa pamoja na wakiangalia TV

Walimwona Yesu Kristo akifanya miujiza na kuwahudumia watu. Kisha wakati watu walipomuumiza Yesu, macho ya Ryan yalijawa na machozi.

“Mama, kwa nini walimfanyia hivyo Yesu?” aliuliza kwa huzuni.

“Yeye alichagua kuteseka kwa niaba yetu,” Mama alisema. “Yeye alitupenda sasa sisi, Ryan. Yeye alikufa ili sisi tuishi tena.”

Wakati sinema ilipoonyesha Ufufuko wa Yesu Kristo, Ryan alitabasamu. “Tazama, Mama! Yu hai tena!”

“Uko sahihi,” Mama alisema. “Amefufuka! Kama vile tu malaika alivyosema katika Biblia.”

Baadaye, Ryan alikwenda nje kucheza. Alimwona Liam akicheza kwa vijiti chini ya mwembe.

Kielelezo cha mvulana akitembea hadi kwa mdogo wake, ambaye amekaa chini ya mwembe

“Liam! Ninataka nikuambie hadithi nzuri,” Ryan alisema.

Liam alisubiri wakati Ryan akiketi chini ya mwembe. “Je, ni kuhusu magari?”

“Hapana. Nzuri zaidi ya magari!” Ryan alisema. “Ni kuhusu Yesu: Alikufa, lakini kisha akawa hai tena”

“Kweli?” Liam aliuliza.

“Ndiyo! Malaika alisema, ‘Hayuko hapa, Amefufuka!’ Hiyo inamaanisha sisi pia tunaweza kuishi tena.”

“Kumbe!” Liam alisema. “Hakika Yesu ni mwenye nguvu.”

Ryan alikubali kwa kichwa. Alifikiria kuhusu ni kiasi gani Yesu alimpenda yeye. Ilifanya moyo wake uhisi kujaa na wenye furaha. Alikuwa ameshiriki habari njema na familia yake, na hiyo ilifanya Pasaka yake kuwa maalum zaidi.

Wavulana wawili wakiwa wamekaa chini ya mti wa mwembe
PDF ya hadithi

Vielelezo na Margarida Esteves. Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.