“Pasaka Kote Ulimwenguni,” Rafiki, Machi 2026, 28–29.
Pasaka Kote Ulimwenguni
Jifunze kuhusu tamaduni kutoka nchi tofauti ili kukusaidia kumkumbuka Mwokozi.
Armenia
Hapa, mayai ya Pasaka yanapakwa rangi nyekundu kama damu ya Yesu Kristo. Siku ya Pasaka, watu wanasema, “Kristo amefufuka kutoka kwa wafu! Heri Ufufuko wa Kristo!” Kisha wanapasua mayai yao kwa pamoja.
Ghana
Watu wengi huvalia mavazi meupe siku ya Pasaka kama sherehe ya Ufufuko wa Yesu Kristo na ushindi juu ya kifo.
Guatemala
Wakati wa Pasaka, watu hufunika mitaa kwa mazulia yenye rangi mbali mbali yaliyotengenezwa kutokana na vumbi la mbao lililotiwa rangi na maua. Mazulia haya yana mpangilio na usanifu mzuri. Baadhi yana picha za Mwokozi.
Ujerumani
Ijumaa Kuu ni “sikukuu ya ukimya” yenye vizuizi vya kisheria juu ya makelele na matukio ya umma. Hii inaruhusu watu kutulia na kutafakari juu ya kile Yesu Kristo alichowafanyia.
Peru
Familia nyingi zinakuwa na karamu yenye vyakula 12 mnamo siku ya Alhamisi au Ijumaa kabla ya Pasaka. Mlo huu unawakilisha Karamu ya Mwisho ambayo Yesu Kristo alikula pamoja na Mitume Kumi na Wawili.
Ufilipino
Katika Jumapili ya Matawi, watu hufuma matawi ya mitende katika miundo ya kupendeza. Hii inawasaidia kukumbuka jinsi watu katika Yerusalemu walivyomkaribisha Yesu Kristo kwa majani ya mitende wakati wa Wiki Takatifu.
Vielelezo na Flavio Remontti. Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.