Rafiki
Pasaka ya Furaha
Machi 2026


“Pasaka ya Furaha,” Rafiki, Machi 2026, 30–31.

Pasaka ya Furaha

Hadithi ya kweli kutoka Kambodia.

Mama, baba, na msichana mdogo mezani wakiwa na rangi na bakuli la mayai

Leo ilikuwa Pasaka! Familia ya Gloria ilikuwa inakwenda kuchora mayai ya Pasaka na kula tambi za mchuzi.

Baba anarusha rusha yai mikononi mwake huku msichana mdogo akicheka

Pa aliokota yai la moto. “Kuwa makini, Pa!” Gloria alicheka.

Msichana mdogo anatoa ulimi wake nje huku akichora yai

Gloria alipaka yai lake rangi ya zambarau.

Baba anatabasamu wakati akiwa ameshikilia brashi ya kuchorea

“Je, unajua kwa nini tunasherehekea Pasaka?” Pa aliuliza.

Msichana mdogo akitabasamu na kuinua yai lake na brashi juu

“Kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yetu na kufufuka tena,” alisema Gloria.

Mama akizungumza wakati akichora yai lake

“Ndiyo” alisema Mama. “Kwa sababu ya Yesu, tunaweza kuishi pamoja tena milele pamoja Naye siku moja!”

Msichana akitabasamu akiwa na yai lake na brashi

“Nadhani Yesu anatupenda kama sisi tunavyopendana,” Gloria alisema.

Familia ikiwa katika kumbatio la kundi

“Hiyo ndiyo sababu Yeye anataka sisi tuishi pamoja Naye milele!”

PDF ya hadithi

Vielelezo na Gillian Reid. Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.