“Margo na Paulo,” Rafiki, Machi 2026, 26.
Margo & Paulo
Tamaduni mpya
YAY! Hatimaye wana mayai ya Pasaka! Naweza kupata moja? Tafadhaaaaali?
Sio leo. Utapata moja siku ya Pasaka.
Ninataka kujaribu baadhi ya tamaduni mpya za Pasaka mwaka huu.
“Ee? “Kama nini?”
Rafiki yetu Julia alisema kwamba kabla ya Pasaka, anafunga kwa siku 40, kama Yesu alivyofanya.
Hali kwa SIKU 40?
Pengine anaacha kitu anachokifurahia—kama vile michezo ya video, au chokoleti.
Nini? Hakuna CHOKOLETI?
Baadhi ya watu hufanya dhabihu kama hii ili kumkumbuka Yesu wakati wa Pasaka.
Je, ni lazima mimi pia niache chokoleti?
Kuna njia zingine nyingi za kumkumbuka Mwokozi wakati wa Pasaka.
Ee! Unakumbuka Pasaka yetu huko Uholanzi?
Ee ndiyo! Moto uliokokwa ulitukumbusha kwamba nuru ya Yesu Kristo inashinda giza.
Nadhani marafiki zetu kote ulimwenguni wana desturi nyingi nzuri. Acha tuwaandikie!
Tunapaswa pia kuwatumia chokoleti kadhaa.
Hayo ni makubwa mno kwa ajili ya kutuma.
Oh! Nadhani basi tutalazimika kuyala!
Margo …
Unaweza kupata moja.
Vielelezo na Katie McDee Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.