Rafiki
Mablanketi ya Pasaka
Machi 2026


“Mablanketi ya Pasaka,” Rafiki, Machi 2026, 34–35.

Mablanketi ya Pasaka

Watoto huko Perth, Australia, walishiriki upendo wa faraja wa Yesu kwa kutoa blanketi kwa wanawake wazee katika kata yao. Wakati wa Pasaka huko Australia, joto huanza kupoa kwa ajili ya majira ya vuli kabla ya majira ya baridi kuja. Watoto mara nyingi hupokea jozi mpya za pajama za majira ya baridi pamoja na mayai ya chokoleti asubuhi ya Pasaka. Pajama na mablanketi yenye joto vinaweza kutukumbusha juu ya upendo wa faraja wa Yesu Kristo.

Kielelezo cha gari likiwa na watoto wengi ndani. Moja ya madirisha ya gari hilo lina picha halisi za watoto walioko ndani ya gari

1. Walikwenda dukani pamoja kuchukua mablanketi.

Picha ya watoto wakifanya sanaa ya kazi za mikono

2. Pia walitengeneza sanaa za maua, walipaka rangi mayai ya mbao ya Pasaka, na kupamba kadi zilizokwenda pamoja na mablanketi.

Kielelezo cha nyumba ikiwa na picha halisi ya mvulana akimkumbatia mwanamke mzee
Kielelezo cha nyumba ikiwa na picha halisi ya mwanamke akiwa ameshikilia blanketi lililoviringishwa

3. Kisha wakayagawa mablanketi hayo. Walifurahia kufanya kazi pamoja ili kuleta upendo wa Mwokozi kwa wengine wakati wa Pasaka.

Kielelezo cha bahasha iliyo wazi

Hapa kuna barua ambayo watoto waliipeleka pamoja na mablanketi hayo!

Picha ya mvulana akitabasamu

Nilifurahia kuweza kujiunga na kufanya kitu kwa pamoja. Safari ya ununuzi ilikuwa bora sana, na tulipata kuchagua rangi za mablanketi. Lilikuwa tukio la kuburudisha na la furaha.

Robert D., miaka 9

Picha ya wavulana wawili wakitabasamu

Tulipenda kuona nyuso za tabasamu za wanawake katika kata yetu wakati tulipokuwa tukiwapatia mablanketi hayo.

Mika na Hyrum M., miaka 10 na 8

Picha ya msichana akitabasamu

Nilikuwa na furaha sana kufanya kitu kizuri kwa ajili ya wazee katika kata yetu.

Miley N., miaka 8

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Sophie Loren Moran. Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.