Rafiki
Igizo la Pasaka
Machi 2026


“Igizo la Pasaka,” Rafiki, Machi 2026, 16-23.

Igizo la Pasaka

Unaweza kuigiza programu hii pamoja na familia yako na marafiki ili kusimulia hadithi ya Pasaka. Unaweza hata kuvaa kama vile watu walivyokuwa wakivaa huko Yerusalemu wakati wa maisha ya Mwokozi.

Unapoigiza programu hii, fikiria ingekuwaje kama ungekuwa pale pamoja na Yesu. Ungejsikiaje? Baada ya programu, zungumza kuhusu kile ulichojifunza na kuhisi.

Onyesho la 1

Jumapili ya Matawi ya Mitende

Wanafunzi wanasimama katika mstari kutengeneza njia kwa ajili ya mshika picha na kupunga majani yao ya mitende.

Msimuliaji: Jumapili kabla ya Yesu Kristo kufa, Alikuja Yerusalemu kwa punda. “Na alipokuwa amekuja … , umati wote wa wanafunzi walianza kushangilia na kumsifu Mungu kwa sauti kuu kwa kazi zote kubwa ambazo wameziona.”1

Mshika picha akitembea katika njia akiwa ameshikilia picha ya 1 (Yesu Kristo akiwa juu ya punda). Wanafunzi walipiga kelele “Hosana!” mara kadhaa huku wakipunga majani ya mitende.

Mwanafunzi wa 1: “Heri Mfalme ajaye katika jina la Bwana: amani mbinguni; na utukufu kwa aliye juu.”2

Msimuliajii: “Na alipokuwa amekuja katika Yerusalemu, mji wote ulisisimka, wakisema, Huyu ni nani?”3

Mwanafunzi wa 2: “Huyu ni Yesu nabii wa Nazareti ya Galilaya.”4

Kila mtu anaimba ubeti wa tatu wa “Beautiful Savior” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 62–63).

Onyesho la 2

Karamu ya Mwisho

Msimuliaji: Siku ya Alhamisi, Yesu Kristo alikusanyika na wanafunzi Wake na kuwapatia sakramenti.

Mshika picha anashikilia picha ya 2 (Yesu kwenye Karamu ya Mwisho). Wanafunzi wanaketi kuzunguka picha na kuitazama picha ya Yesu.

Msimuliaji: “Na walipokuwa wakila, Yesu alichukuwa mkate, akaubariki, na kuumega na kuwapa, na alisema, Twaeni, mle: huu ni mwili wangu.”5

Kwa staha, mmoja wa wale wanafunzi anainua juu mkate.

Msimuliaji: “Na akatwaa kikombe, na baada ya kushukuru, akawapa wao: nao wote wakanywa. Na akawaambia, Hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi.”6

Kwa staha, mmoja wa wanafunzi anainua kikombe.

Msimuliaji: Yesu pia aliwafundisha jambo muhimu. Alisema, “Amri mpya ninawapa, Mpendane; kama nilivyowapenda ninyi. … Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”7

Kila mmoja anaimba “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136).

Onyesho la 3

Bustani ya Gethsemane

Msimuliaji: “Kisha Yesu akaja pamoja nao mahali palipoitwa Gethsemane, na akawaambia wanafunzi Wake, Kaeni hapa, wakati naenda na kusali pale.”8

Wale Wanafunzi wanaketi pamoja kwenye upande mmoja wa jukwaa. Mshika picha anasimama upande mwingine wa jukwaa, akiwa ameinua juu picha ya 3 (Yesu akisali katika bustani).

Msimuliaji: “Na [Yesu] akaenda mbele kidogo, na kuanguka kifulifuli, na kuomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke: walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.”9

Wale wanafunzi wanalala chini wakiigiza kulala usingizi.

Msimulizi: Wakati Mwokozi akisali, wanafunzi Wake walilala. Yesu aliteseka katika bustani peke yake. Alihisi maumivu yetu yote na huzuni ili aweze kutuelewa na kutusaidia. Aliteseka ili kulipia adhabu ya dhambi zetu.

Kila mtu anaimba “Gethsemane (Nyimbo za Dini—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani, na. 1009).

onyesho la 4

Msalaba

Msimuliaji: Baada ya Yesu kumaliza kusali, askari walimchukua na kumfunga. Ingawa hakufanya kosa lolote, viongozi waliamua kumuua.

Mshika picha ananyanyua juu picha ya 4 (Mwokozi akiwa msalabani). Wale wanafunzi wanapiga magoti katika duara, wakitazama juu kwenye picha.

Msimuliaji: Alipokuwa ananin’ginia msalabani, Yesu alisema, “Baba, uwasamehe; kwa maana hawajui watendalo.”10 Hata katika maumivu Yake makubwa, Alikuwa mfano kamili wa upendo na msamaha.

Kila mtu anaimba “Nje ya Yerusalemu” (Nyimbo za Dini, na. 107).

Onyesho la 5

Kaburi

Msimuliaji: Baada ya Yesu Kristo kufa, mwili Wake ulilala kaburini kwa siku tatu. Katika siku ya tatu, Mariamu Magdalena na wanawake wengine walikuja kutembelea kaburi. “Wakalikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi. Na wakaingia ndani, na wasiuone mwili wa Bwana Yesu.”11

Mariamu na wale wanawake kwa huzuni wanatembea jukwaani na kuangalia kote, wakiwa wamwkanganyikiwa.

Msimuliaji: Malaika wawili walitokea na kuzungumza na wale wanawake.

Malaika wa 1 na Malaika wa 2 wanapanda kwenye jukwaa karibu na Mariamu .

Malaika wa 1: “Usiogope … kwani najua mnamtafuta Yesu, aliyesulubiwa.”12

Malaika wa 2: “Hayupo hapa: kwani amefufuka.”13

Msimuliaji: “Nao wakaondoka haraka … kwa woga na shangwe kuu; na walikimbia ili kuwaletea wanafunzi [wengine] neno.”14

Mariamu na wale wanawake kwa shangwe wanakimbia kutoka jukwaani ili kushiriki habari njema kwa kila mtu.

Mariamu: Amefufuka! Yesu Kristo yu hai!

Mshika picha ananyanyua juu picha ya 5 (Kristo aliyefufuka). Kila mtu anarudi kwenye jukwaa.

Msimuliaji: Mwokozi wetu alifufuka tena asubuhi ya Pasaka. Kwa sababu ya Yesu Kristo, kila kitu kilibadilika. Tunaweza kuwa na tumaini, amani, na furaha. Kwa sababu Yeye yu hai, Yeye yu pamoja nasi leo na siku zote.

Kila mtu anaimba “Jesus Has Risen” (Friend, Apr. 2025, 18–19).

Ukurasa wa PDF ukiwa na kielelezo cha watoto waliovalia mavazi ya Kibiblia na kushikilia majani ya mitende

Vielelezo na Róisín Hahessy Michoro na Dan Burr Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.

  1. Luka 19:37

  2. Luka 19:38

  3. Mathayo 21:10

  4. Mathayo 21:11

  5. Marko 14:22

  6. Marko 14:23–24

  7. Yohana 13:34–35

  8. Mathayo 26:36

  9. Mathayo 26:39

  10. Luka 23:34

  11. Luka 24:2–3

  12. Mathayo 28:5

  13. Mathayo 28:6

  14. Mathayo 28:8