“Karibuni, Marafiki!” Rafiki, Machi 2026, 1.
Karibuni, Marafiki!
Toleo hili ni kuhusu kuifanya familia yako iwe tayari kwa ajili ya Pasaka! Unaweza kutumia Changamoto ya Shughuli za Pasaka (ukurasa wa 14) kwa ajili ya baadhi ya vitu rahisi vya kufanya kuelekea Pasaka. Au fuatana na familia ya Mia kusherehekea kila siku ya Wiki Takatifu (ukurasa wa 12).
Kuna sanaa za kutengeneza (ukurasa wa 38), kurasa za kupaka rangi (ukurasa wa 24), na mchezo mzuri wa kuigiza wa Pasaka (ukurasa wa 16). Andika kutuambia kile familia yako inachokifanya kwa ajili ya Pasaka mwaka huu!
Tunasherehekea Pasaka mara moja tu kwa mwaka, lakini tunaweza kumsherehekea Mwokozi wetu na upendo Wake kwetu mwaka mzima.
Upendo,
Jarida la Rafiki