“Kazi ya Mikono ya Bustani ya Ufufuko,” Rafiki, Machi 2026, 8–9.
Kazi ya Mikono ya Bustani ya Ufufuko
Tengeneza bustani ya Ufufuko ili ikukumbushe kwamba Yesu Kristo amefufuka! Weka chungu kidogo cha maua au kikombe kwenye sahani kando ya njia ndogo za vumbi. Funika sehemu ya juu ya chungu cha maua kwa udongo ili ionekane kama kaburi. Kisha tumia kokoto, maua, na vitu vingine kutoka kwenye mazingira ya asili ili kupamba eneo. Unaweza kukata maumbo na kuyaweka katika bustani pia!
Diorama na picha na Anna Oldroyd. Vielelezo na Shawna J. C. Tenney Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.