2025
Pokea Zawadi Yake
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Mei 2025


Kikao cha Jumapili Mchana

Pokea Zawadi Yake

Dondoo

alt text

Pakua PDF

Ningependa kuzungumza kuhusu zawadi moja inayojumuisha-yote ya ukweli wa milele ambayo inatoa uwezo wetu wa kupokea mengine yote ambayo Baba anatamani kutupatia—zawadi muhimu ya maarifa ambayo ikikubaliwa kwa ukamilifu na kupokelewa kwa kina ndani ya nafsi, inaweka mazingira ya shangwe na magumu ya maisha, na maswali yetu yasiyojibiwa: Ni kwamba sisi hakika ni watoto wa Mungu. Inastaajabisha! Inashangaza! Na ukweli huu siyo mfano.

… Na njia uliyoko ni mpango Wake wa furaha. … Na lo, anatamani kiasi gani kwamba siku moja urejee Kwake, ili upokee dhamira kuu ya zawadi Zake zote nzuri, uzima wa milele pamoja na Yeye. …

… Mnaweza kuja kwa Kristo kwa kujiamini katika upendo Wake wa ukarimu na kupokea karama Zake zote za shangwe, amani, tumaini, nuru, ukweli, ufunuo, maarifa na hekima—na kichwa chako kikiinuliwa juu, mikono kunyooshwa na viganja vikiwa wazi, tayari kupokea. Na unaweza kupokea zawadi hizi kwa sababu wewe uko salama na umejengwa katika maarifa ya kwamba wewe ni binti mpendwa wa Mungu, wewe ni mwana mpendwa wa thamani wa Mungu, na amekupa wewe zawadi ya Mwanawe mkamilifu mtakatifu ili akukomboe, kukuhalalisha na kukutakasa.

… Ipokee upya zawadi hii au pengine hakika ipokee kwa mara ya kwanza kabisa, na acha ibadilishe kila kipengele cha maisha yako. Hii ni njia iliyo bora zaidi ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili yako kupitia Mwanawe. Wewe upo ili upate kuwa na shangwe!