Kikao cha Jumamosi Mchana
Mamlaka ya Kiungu, Wavulana Adhimu
Dondoo
Januari hii, nilipokuwa nimeketi katika mkutano wa sakramenti, zaidi ya wavulana dezeni moja walikubaliwa kupandishwa katika Ukuhani wa Haruni. Nilihisi ulimwengu ukibadilika chini ya miguu yetu.
Ilinishangaza kwamba kote ulimwenguni, kulingana na saa za nchi husika, katika mikutano ya sakramenti kama ule, makumi elfu ya mashemasi, walimu na makuhani walikuwa wakikubaliwa ili kutawazwa kwenye huduma za ukuhani za maisha yote ambazo zingetanuka kwa urefu na upana kwenye ukusanyaji wa Israeli. …
Utawazo huu unawaingiza wavulana hawa kwenye huduma ya maisha yote kadiri watakavyojikuta wenyewe katika nyakati zenye matokeo na sehemu ambapo uwepo wao na sala zao na nguvu za ukuhani wa Mungu walio nao vitakuwa na umuhimu. …
Bwana anawakabidhi leo wenye ukuhani wa Haruni wa siku za leo kufanya mambo yale yale waliyoyafanya hapo kale: kufundisha na kuhudumu katika ibada—yote kutukumbusha juu ya Upatanisho Wake.
Wakati mashemasi, walimu na makuhani wanaposaidia kwenye sakramenti, wanapokea baraka za sakramenti kama vile mwingine yeyote: kwa kushika agano wanalolifanya pale wao binafsi wanapopokea mkate na maji. Lakini katika utekelezaji wa majukumu haya matakatifu, wanajifunza pia zaidi kuhusu wajibu wao na majukumu ya ukuhani. …
Matarajio hayo makini yanahitaji maandalizi makini. …
Nina shukrani milele kwamba wenye Ukuhani wa Haruni, pamoja na nguvu zake, ibada na wajibu, wanatubariki sote kupitia funguo za “huduma za malaika, na za injili ya toba, na za ubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi” (Mafundisho na Maagano 13:1).