2025
Kujiamini katika Uwepo wa Mungu
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Mei 2025


Kikao cha Jumapili Mchana

Kujiamini katika Uwepo wa Mungu

Dondoo

alt text

Pakua PDF

Tunapofanya na kushika maagano na Mungu, tunaweza kuwa na imani ambayo imezaliwa na Roho. Bwana alimwambia Nabii Joseph Smith kwamba kujiamini kwetu kunaweza “kuwa imara katika uwepo wa Mungu.” …

Ninapoongelea juu ya kuwa na kujiamini mbele ya Mungu, ninamaanisha kuwa na kujiamini katika kumkaribia Mungu hivi sasa! …

Sasa, ni kwa jinsi gani tunapata kujiamini kama huku? …

… Kwa maneno ya Bwana mwenyewe, hisani na wema hufungua njia ya kuwa na imani mbele za Mungu! …

Kwanza, hisani. …

Hisani ya kweli kwa watu wote ni sifa bainifu ya wapatanishi! Ni muhimu kwamba tuwe na hisani katika mahubiri yetu, kwa umma na faragha. …

Acha tumsihi Baba yetu wa Mbinguni ajaze mioyo yetu na hisani kuu—hasa kwa wale ambao ni vigumu kupenda—kwani hisani ni zawadi kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo. …

Sasa, acha tuzungumze kuhusu wema. Bwana anatuambia kupamba mawazo yetu bila kukoma kwa wema. … Wema hufanya kila kitu kuwa bora na chenye furaha zaidi! … Wema utakuweka huru kutokana na mawazo yenye wasiwasi, ya kusumbua. …

… Fursa kubwa mbele yetu ni kuwa watu ambao Mungu anahitaji tuwe. …

… Ninawaalika kuchukua hatua za makusudi kukua katika kujiamini kwenu mbele za Bwana. Kisha, tunapokwenda kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa kujiamini zaidi, tutajazwa na shangwe zaidi, na imani yako katika Yesu Kristo itaongezeka. Tutaanza kupata uzoefu wa nguvu za kiroho ambazo zinashinda matumaini yetu makubwa.