2025
Kumfuata Kristo
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Mei 2025


Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Upatanisho wa Yesu Kristo Hutoa Uokoaji wa Mwisho

Dondoo

alt text

Pakua PDF

Tukio hili la waanzilishi linawapa Watakatifu wa Siku za Mwisho desturi ya kihistoria ya kipekee na urithi wa pamoja wenye nguvu za kiroho. …

Wengi wa Watakatifu wa mikokoteni ya mkono walipitia magumu lakini waliepuka matukio mabaya makubwa. Lakini kombania mbili za mikokoteni ya mikono, kombania ya Willie na kombania ya Martin, zilipitia baa la njaa, kupigwa na hali ya hewa ya baridi kali na vifo vingi. …

Rais Brigham Young alikuja kujua kwa mara ya kwanza juu ya hali hiyo hatarishi ya kombania hizi mbili mnamo Oktoba 4, 1856. …

Aliomba maaskofu kutoa timu 60 za nyumbu, magari 12 ya kukokotwa na farasi au zaidi, na tani 12 (kilo 10,886) za unga, na kutangaza, “Nendeni na muwalete wale watu ambao sasa wako mbugani.”

… Pasingelikuwa na uokoaji huu wa wakati muafaka, wengi zaidi wangeangamiana. …

Pasipo Upatanisho, hatuwezi kujiokoa wenyewe kutokana na dhambi na kifo. …

Wakati huu wa majira ya Pasaka, fokasi yetu ni juu ya Mwokozi na dhabihu Yake ya kulipia dhambi. Upatanisho unatoa matumaini na nuru wakati ambapo kwa wengi huona giza na woga. …

Ninashiriki mapendekezo matatu ambayo nafikiri yanahusika kipekee kwa siku yetu.

Kwanza, usidharau umuhimu wa kufanya kile tunachoweza ili kuwaokoa wengine kutokana na changamoto za kimwili na hususani za kiroho.

Pili, kwa shukrani kubali Upatanisho wa Mwokozi. …

Ushauri wangu wa tatu ni kutenga muda endelevu wa kutafakari kwa uaminifu Upatanisho wa Mwokozi. Kuna njia nyingi za kufanya hili katika maadhimisho yetu binafsi ya kidini. Hata hivyo, kuhudhuria mkutano wa sakramenti na kupokea sakramenti ni muhimu hasa.

Lililo na umuhimu sawa ni uhudhuriaji wa mara kwa mara hekaluni pale inapowezekana. …

… Upatanisho wa Yesu Kristo hutoa uokoaji wa mwisho kutoka kwenye majaribu tunayokabiliana nayo katika maisha haya.