2025
Kuthamini Maisha
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Mei 2025


Kikao Cha Jumamosi Mchana

Kuthamini Maisha

Dondoo

alt text

Pakua PDF

Wakati mwingine, mashaka magumu sana na yaumizayo sana yanaweza kuambatana na ulinzi wa uhai.

Mara nyingi maneno mawili huambatanishwa kwenye utakatifu wa uhai wa kuzaliwa duniani: uhai na uchaguzi. Uhai ni sehemu ya thamani sana ya mpango mkamilifu wa Baba, na kwa amri Yake tunathamini na tunahifadhi uhai; na tunachagua mwendelezo wa uhai wakati wa ujauzito. Pia tunathamini zawadi ya chaguo la uhuru wa kujiamulia kimaadili—kusaidia kuimarisha chaguzi za haki zilizoidhinishwa na Mungu ambazo huleta furaha ya milele. …

Kutunza na kulinda maisha ambayo hayajazaliwa siyo jambo la kisiasa. Ni sheria ya maadili iliyothibitishwa na Bwana kupitia manabii Wake.

… Acha tuzungumze mara kwa mara kwa imani na huruma kwa vijana wetu katika nyumba zetu, na mmoja na mwingine, katika Muungano wetu wa Usaidizi na mikutano ya akidi za wazee kuhusu sheria ya usafi wa kimwili ya Bwana, utakatifu wa uhai, na matunzo kwa ambao hawajazaliwa na mama zao. …

Kwa yeyote anayesikiliza ambaye amepitia maumivu makali na majuto kwa au kushiriki katika kutoa mimba, tafadhali kumbuka: Ingawa hatuwezi kubadili yaliyopita, Mungu anaweza kuponya hayo yaliyopita. Msamaha unaweza kuja kupitia miujiza ya neema Yake ya upatanisho pale unapomgeukia Yeye kwa moyo mnyenyekevu na wa toba.

Wapendwa akina kaka na dada zangu, kupungua kwa upendo kwa watoto ambao hawajazaliwa ni jambo kubwa ulimwenguni kote. Mungu anathamini uhai. Ni kazi Yake na utukufu kuleta kutokufa na uzima wa milele kwa watoto Wake. Kama wanafunzi wa Yesu Kristo, tunathamini uhai.