Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Kama Mtoto Mdogo
Dondoo
Yesu … “akamwita mtoto mdogo kwake, …
“Na akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka, na kuwa kama watoto wadogo, hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.
“Yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni”. …
… Kilikuwa ni kipi kilichomfanya Kristo Mwenyewe kutokwa machozi katika mandhari ororo sana kwenye Kitabu cha Mormoni? Yesu alikuwa akifundisha nini wakati alipoamuru moto toka mbinguni na malaika wenye kulinda kuwazunguka watoto wale, akiwaamuru wakubwa “kuwatazama watoto [wao] wadogo”?
Hatujui kile kilicholeta haya yote, lakini ninafikiria ilikuwa ni kuhusu usafi na utakatifu wao, unyenyekevu wao wa kuzaliwa nao, na kile ambacho kingeweza kuletwa katika maisha yetu kutokana na hayo. …
Lakini watoto kwa dhati wanampenda Yeye, na upendo huo unaweza kubebwa hata katika mahusiano yao mengine katika maisha yao. Kama sheria, hata katika miaka yao ya uchanga, watoto wanapenda kwa urahisi sana, wanasamehe mara moja na kucheka kwa furaha sana hata moyo katili na mgumu unaweza kuyeyuka.
Basi, orodha inaendelea na kuendelea. Usafi? Amini? Ujasiri? Hulka?. …
Akina dada na akina kaka na marafiki, kilicho juu zaidi kwenye orodha ya mtazamo mzuri niujuao ni watoto wachanga na wadogo na vijana wenye sifa kama zile nilizoelezea leo. Ninashuhudia kwamba wao ni sura ya ufalme wa Mungu duniani wakistawi katika nguvu zake zote na uzuri.