Kikao cha Jumamosi Jioni
Kuabudu
Dondoo
Kwa hivyo kumsujudia Mungu inamaanisha nini kwako wewe na mimi? …
Kwanza, Vitendo Ambavyo Vinachangia Kuabudu Kwetu
Moja ya aina za kawaida na muhimu zaidi za kuabudu ni kukusanyika katika sehemu zilizotakaswa ili kufanya matendo ya kiibada. …
Kuabudu katika siku ya Bwana huonyeshwa na fokasi maalumu juu ya dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi. … Kwa mwenye kutubu, kupokea sakramenti ni onyesho kuu la kuabudu siku ya Sabato.
… Kama jumuiya ya Watakatifu, tunaimarishana sisi kwa sisi katika kuabudu na katika imani.
Hata hivyo, hatuwezi kusahau matendo ya kila siku ya kuabudu ambayo tunayafanya binafsi na nyumbani. …
Mitazamo na Hisia Zinazopatikana katika Kuabudu
Ibada ya kweli inamaanisha kumpenda Mungu na kuyaweka mapenzi yetu Kwake—ni zawadi ya thamani tunayoweza kutoa. …
Huu ulikuwa mpangilio wa Yesu mwenyewe wa kumwabudu Baba. …
Kuabudu ni kujitahidi kufuata mfano huu mkamilifu. …
Tatu, Upekee wa Kuabudu Kwetu
Chochote kinachochukua kipaumbele juu ya kumwabudu Baba na Mwana kinakuwa ni sanamu. … Lengo la kuabudu kwetu ni la kipekee kwa “Mungu pekee wa kweli, na Yesu Kristo, ambaye [Yeye] amemtuma.”
Mwisho, Haja ya Kufuata mfano wa Baba na Mwana
Mwishowe, jinsi tunavyoishi yawezekana kuwa ndiyo bora, aina halisi zaidi ya kuabudu. Kuonyesha mapenzi yetu inamaanisha kufuata mfano wa Baba na Mwana—tukikuza sifa na tabia zao ndani yetu. …
… Tunapotembea katika njia ya agano, ile “nguvu itakasayo ya uchamungu inadhihirika” ndani yetu.